Kitu gani kilisababisha usijiunge na UDSM?

Kitu gani kilisababisha usijiunge na UDSM?

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni chuo bora Tanzania. Kiko mbali mno kwa ubora kulinganisha na vyuo vingine. Kikubwa zaidi ni kuwa wanaodahiliwa Mlimani ni vipanga watupu. Bila Div One & Two ni ngumu mno kuwa mwanafunzi wa UDSM. Ni ndoto ya watanzania wengi kusoma pale. Hata mimi ilikuwa ndoto yangu kusoma pale ila haikuwezekana. Nitaeleza kwanini.

Kwa upande wangu nilishindwa kujiunga na UDSM kwa sababu kwenye maombi yangu sikuambatanisha baadhi ya vitu hivyo maombi yangu kutofanyiwa kazi. Nakumbuka siku chache kabla ya Marticulation exam pale Arusha Tech ndo nilipokea majibu kuhusu makosa niliyofanya wakati wa kutuma maombi. Ikabidi nikajiunge na chuo kingine ambacho bado hawakuwa wamefika deadline ya kutuma maombi.

Je, wewe kwanini ulishindwa kusoma UDSM undergraduate?
Sikuwahi kuwa na wazo wala ndoto ya kusoma UDSM.
 
Enzi zetu udsm ndio kila kitu, vyuo vingine bora vilivyokuwepo ni mzumbe na sua.
 
Mahali napotafutia ugali kuna two graduates wa udsm kwa miaka tofauti,mmoja katoka udsm 2021 mwingine 2015 ila huyu dogo wa 2021 ni wa moto sio poa,yuko nondo sana….huyu wa 2015 had najiuliza udsm aliingiaje make ni zaidi ya mweupe,mjanja mjanja na maneno n mengi….Anyways sie wengine tumesoma uswekeni hukomikoani lakin tulikua na ndoto za kusoma mliman tukakosa nafasi (ufaulu mdogo)
 
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni chuo bora Tanzania. Kiko mbali mno kwa ubora kulinganisha na vyuo vingine. Kikubwa zaidi ni kuwa wanaodahiliwa Mlimani ni vipanga watupu. Bila Div One & Two ni ngumu mno kuwa mwanafunzi wa UDSM. Ni ndoto ya watanzania wengi kusoma pale. Hata mimi ilikuwa ndoto yangu kusoma pale ila haikuwezekana. Nitaeleza kwanini.

Kwa upande wangu nilishindwa kujiunga na UDSM kwa sababu kwenye maombi yangu sikuambatanisha baadhi ya vitu hivyo maombi yangu kutofanyiwa kazi. Nakumbuka siku chache kabla ya Marticulation exam pale Arusha Tech ndo nilipokea majibu kuhusu makosa niliyofanya wakati wa kutuma maombi. Ikabidi nikajiunge na chuo kingine ambacho bado hawakuwa wamefika deadline ya kutuma maombi.

Je, wewe kwanini ulishindwa kusoma UDSM undergraduate?
Kusoma sheria miaka 4
 
Mzee wangu alipingana na aina ya maisha ya UDSM. Hii ni baada ya binamu zangu mmoja kupata ujauzito akiwa mwaka wa 1 na mwingine wa kiume ku disco sababu ya ulevi uliokithiri.
Kwahiyo aliogopa na wewe ungepewa mimba? 😥
 
😄😄 huu uzi wa kujiburudisha tu maana baada ya chuo hata aliyesoma chuo cha Nyuki Tabora anaweza kumkimbiza wa UDSM kimaisha...
Wote wa UDSM MU UDOM MUST SAUTI TEKU mwisho VETA kuchukua ujuzi 😹😹
 
Kila nikitaka kuandika jibu nililodhamiria nafsi yangu inanikataza sababu nahisi nakuheshimu.
Kwanini? Nimeona umesema baba yako aliogopa sababu dada yako alipewa mimba. Au nimesoma vibaya mkuu?
 
Back
Top Bottom