Kitu gani kimekufurahisha na kukufariji siku ya leo

Kitu gani kimekufurahisha na kukufariji siku ya leo

SinaMdaa

Member
Joined
Jul 11, 2023
Posts
37
Reaction score
78
Habarini wadau.

Kama ilivyo ada leo mapema asubuhi kichovu nikijongea stendi kudandia usafiri kuelekea kwenye mihangaiko ya kila siku, maana sikuizi unalala umechoka unaamka umechoka sijui labda ni mapambano ya kila siku bila kujali weekend ama laa! inapalekea tunakuwa wachovu kiasi hichi.

Sasa bwana nikiwa nimesimama nasubiria civilian ije nikimbizane mara kaja mtoto mdogo wa shule like miaka 8 ivi, kaka naomba univushe, basi nikiwa nimemshika kamkono kake kadogo namvusha nimejiuliza hivi haka ka malaika Kwa nini kamenichagua mimi niliyekuwa katikati ya umati wa watu kama 30 hivi .

Sijui Kwanin lakini kile kitendo kimenifariji sana na kufanya siku yangu ya neema

Vipi wewe mdau kitu gani kimekufurahisha na kukufariji leo?
 
Kukumbuka Mungu wangu, nilipofungu tu macho, imenipa furaha na faraja. Nimesema Mungu wangu, Asante 🔥
 
Play list ya ngoma nizipendazo nimeikuta sehemu dah nimesahau shida kwa muda aise.
 
Back
Top Bottom