Kitu gani/mambo gani yanapendwa na watu lakini wewe hayakushawishi kukuvutia/kuyapenda?

Kitu gani/mambo gani yanapendwa na watu lakini wewe hayakushawishi kukuvutia/kuyapenda?

1.Sipendi kumlazimisha mtu hasa jinsia ya KE.
2.Sipendi mambo ya kufatiliana kila mtu na njia yake
 
Kuna channel Azam inaitwa sinema zetu....huwa nahisi malaria nikilazimika kutazama
 
kukesha club kila siku, kunywa pombe kupita kiasi, kuvuta sheesha, waendesha altezza na subaru kwa fujo wananikera, threesome, mwanaume kukutongoza na kuanza kukuchukia ukimkataa(fala kabisa) nikikumbuka mengine ntarudi kuongeza. Ila baada ya kukua nimekuja kuelewa tuko duniani na kila mtu ana tabia yake na mfumo wake wa maisha. Na huwa siwahukumu ila ukitaka unichefue uniulize kwanini sipendi usichopenda.
 
Simu ya Iphone jamani, huwa nashangaa watu wanavyopienda na kuzishobokea. Sijawahi hata kushawishika kuitumia wala kuipenda hata nikiiona . Mimi na Samsung daima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom