Kitu gani ulikifurahia maishani ukaja kukuta sivyo

Babumawe

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2014
Posts
2,556
Reaction score
2,571
Ni kitu gani katika maisha yako uliwahi kukifurahia kabla lakini ukaja kukuta sivyo kabisa na matarajio kiasi cha kukukata stimu kabisa.

Mfano mimi kipindi tunasoma boarding nakumbuka ilikuwa jumatano iyo siku inakuwaga siku ya kula pilau pale shuleni sasa bhana siunajua mambo ya boarding zikifikaga siku za pilau na nyama mnakuwaga mnaona muda hauendi kwa jinsi mnavyongojea kufinya ubwabwa,

sasa nakumbuka tupo zetu hosteli ndani tunasubiria time ifike tu tukafinye zetu kichele, basi muda wote tupo ndani kule tunacheza miziki balaa full mijasho yaani full kujitupatupa na minyimbo ya TMK wanaume " hakuna kulala hakuna kulala hatakama hujala hatakama hujala" yaani ilikuwa full shangwe, sasa bhana time ikafika kwenda zetu dining tukakuta MAKANDE. bhana tulikaa chini tumenyong'onyea yaani ilikuwa kama kuna msiba.
 
🤣🤣 Dah!
 

[emoji12] [emoji12]
 
Mimi ndoa bana,
Niliifurahia mwanzoni sana,semina zake mpaka kuiishi kwa muda hivi,
Ila kwa sasa,huwa sishauri mtu Kuoa au kuolewa,
I’ll remain divorced the rest of my life,
Hii ni exclusive kabisa toka kwangu.
Nafikiri usipo pata mtu sahihi kwenye ndoa, hakika hauto ipata furaha milele
 
Nilitarajia yule mpenzi wa kwanza aliyenitoa bikra nikiwa chuo kuwa one and only man katika maisha yangu

Lakini alikuja akaniacha kabla hata ya kumaliza chuo chenyewe mammmmmmae zake boya yule
Mwali, naona umeianza Christmas kwa uchungu zaidi....😂😂
Anyway, pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…