Kitu gani ulikikuta kwenye nyumba au ghetto kikakushangaza sana?

KUNA MWANA GHETTO KWAKE ALIKUWA ANAMILIKI FIRST AID KIT
 

Asee umenikumbusha ile nyumba nilienda nikafikia 'sebleni' kwanza muundo wa ndani wa ile nyumba sijawahi kuona mahali popote

Kilichonishangaza ni rangi zile za kupakaa kucha zilizopangwa pembeni ya kuta za pale ndani (nimeshindwa kuelezea ukapata picha halisi lakini nilishangaa)
 
Rangi za kupaka kucha! inaonekana zilikuwa nyingi sana kiasi cha kushangaza!
Hio sebule ina muundo gani huo never seen before! 😳
 
nilienda kumsalimia mamdogo hapo kigogo, mumewe ni fundi garage sasa siku hiyo alisema ana udhuru atachelewa kurudi tukaenda kurundikana chumbani kwa huyo mama mm na wanawe,

nikaangusha nguo ikabidi niiname niokote macho yakatua uvunguni aisee utasema stoo, uvungu umejaa jeki skui like mnaita rim mi spana na minnati ya kumwaga dishi ndani limejaa plugs kuuliza nilishindwa mpaka nimeondoka kaniachia maswali kibao, had leo sidhan anajua kama niliona vile vitu kule uvunguni yani hata nyoka ageingia agejichimbia freeesha akaanzisha na familia kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…