Kitu gani ulikutana nacho au kukifanya kwenye Interview ukajua ushakosa Kazi

Niliulizwa swali moja la kijinga basi nami nilijibu ujinga mbele ya jopo la waheshimiwa mpaka mkurugenzi wa taasisi hiyo akasema haa!
Kuja kuuliza wale wazee mule ndani ni kina nani?

Nilivyopewa taarifa/nyadhifa zao nikaenda zangu kulala kwa kujua tayari nishaliwa manyoya.

Wiki mbili mbele napokea simu ya wito. Nikasema naenda kushtakiwa.
 
Na ulipofika..?!😅
 
😄😄😄 So ukupata?
 
Tumeitwa kwenye interview siku ikafika, nimeingia pale mapokezi nakuta wenzangu wamekaa pale, huku tukipiga story mbili tatu ghafla anatokea boss wa ofisi, anatusalimia wote, baadae anamgeukia mdada mmoja anamuuliza wewe ndie mtoto wa mzee fulani.....

Japo interview ilienda poa lakini ikawa kila nikimkumbuka yule mtoto wa mzee fulani stimu nakosa, mwishowe kimya kikatawala nikaona isiwe kesi bora niingie zangu kwenye kilimo.

Mungu ni mwema nalima na maisha yanaenda mjini kama yanavyomuendea yule mtoto wa mzee fulani..
 
Niliulizwa swali moja la kijinga basi nami nilijibu ujinga mbele ya jopo la waheshimiwa mpaka mkurugenzi wa taasisi hiyo akasema haa!
Kuja kuuliza wale wazee mule ndani ni kina nani?

Nilivyopewa taarifa/nyadhifa zao nikaenda zangu kulala kwa kujua tayari nishaliwa manyoya.

Wiki mbili mbele napokea simu ya wito. Nikasema naenda kushtakiwa.
😁😁😁 Ikawaje sasa mkuu
 
Mwaka 2003 niiitwa interview ya taasisi ya kuzuia rushwa (PCB). Nikasafiri toka mkoani, kufika pale maswali mawili niliyoulizwa nikajua nimeyakosa pale pale ukiacha mengine niliyokuwa nikibahatisha bahatisha.
Swali la 1 lilikuwa niseme ni tukio gani kubwa lilitokea mwaka 1922 na likapelekea kubadilisha mustakabali mzima wa historia ya nchi yetu, nikajibu ni kuasisiwa kwa Tanganyika African Association (TAA) kumbe ilikuwa ni kuzaliwa kwa Mwl J. K. Nyerere
Swali la 2 ilitakiwa nieleze ugonjwa wa anthrax, nikajichanganya nikawaambia unatokana na mashambulizi ya mabomu huko mashariki ya kati.
 
Mimi huamini bora uji portray kama unayo kazi kuliko umeenda interview kama job less so, katika randomly answering nikajibu

"......in my previous companies.....and....in Company which am working right now"

Oyaa msisitizo wa swali uliotokea hapo na zile facial expressions Like

"So sasahivi upo unafanya kamouni...."

"Why unataka change kazi"

Nikaona hapa nimezingua tiali, alafu kampuni tamu ile ina ofisi kali pia zipo Prime area DSM hata mshahara utakuwa mzuri.
 
Niliulizwa kwa sasa unajishughulisha na nini nikawatajia wakaniuliza kwahiyo ukiipata hii kazi bado utaendelea na shughuli yako hiyo nikawambia ndio wakauliza utawezaje nikawambia ntabalance, nikaona mjerumani wa watu kwenye pannel pua na chini ya macho kunakua pekundu nikajua hapa nimejichanganya tayari.
 
Mwaka huo huo wa 2003 nilikwenda interview kiwanda cha AZAM, kile cha pale TAZARA/BUGURUNI. Ndio kilikuwa kinajiandaa kuanza production, bado kipya kabisa. Baada ya kukagua vyeti vyangu wakaniuliza kama kweli nimewahi kufanya kazi kwenye sekta ya usagaji wa nafaka. Nikawaambia nilishafanya kwa muda kidogo, hapo ndio ni kama nimejichanganya jumla.
Yule muhindi akanipa plain paper na penseli akinitaka nimchoree mchoro wa hiyo mashine ilikuwaje. Kiukweli sikuwa nimewahi kufanya kazi kwenye viwanda ukiachia mbali kuziona hizi mashine za huku mitaani tu. Yaani nilifikiria nikaamua kuchora tu hizi mashine za mitaani, ila nikaichora kubwa ikajaa karatasi zima, yule Muhindi akauangalia ule mchoro akatikisa kichwa akaondoka kimya tu.
 
Ulishawahi kuona yale Mazingira ya kushindwa jambo au kukosa fursa kabla hata hujaipata, basi kuna wakati unaweza kujikuta umefeli Interview hata kabla ya kupewa Majibu na Kampuni husika

Umeshawahi kupatwa na hali hii? Nini kilitokea?
Ndio iliwai kunitokea hali ya kuitwa kweny usahili nikajibu maswal Kwa ufasaha kabisa,baada ya mda niliambiwa nitapewa majibu ila sikupigiwa simu,nikaamua kumtafta HR akaniambia subiri sikukata tamaa,sikupewa jibu ikanibidi niende Moja Kwa moja ofisini ndio wakanambia nimeshinda interview nenda tutakuita,nikaenda nasubiri sikuitwa ikanibidi nipige simu majibu yakawa yaleyale, Mimi huyo sasa nikaamua kuchukua mkataba wa general activities kweny hiyo kampuni ili nipate hiyo fursa ase nilifanikiwa
 
Mwaka 2003 niiitwa interview ya taasisi ya kuzuia rushwa (PCB). Nikasafiri toka mkoani, kufika pale maswali mawili niliyoulizwa nikajua nimeyakosa pale pale ukiacha mengine niliyokuwa nikibahatisha bahatisha.
Swali la 1 lilikuwa niseme ni tukio gani kubwa lilitokea mwaka 1922 na likapelekea kubadilisha mustakabali mzima wa historia ya nchi yetu, nikajibu ni kuasisiwa kwa Tanganyika African Association (TAA) kumbe ilikuwa ni kuzaliwa kwa Mwl J. K. Nyerere
Swali la 2 ilitakiwa nieleze ugonjwa wa anthrax, nikajichanganya nikawaambia unatokana na mashambulizi ya mabomu huko mashariki ya kati.
hahahah
 
Back
Top Bottom