Mtu Mbadi
JF-Expert Member
- Feb 28, 2024
- 403
- 457
Dah interview yangu ya kwanza kuingia oral na nikakandwa (TFS), nilijichanganya sana kwenye swali la explain about yourself.. ... sitakagi hata kukumbuka... Basi kutokana na kuwa nilikuwa sijui vizur namna ya kulijibu hili swali nikaanza pale kutaja jina langu freshi, sasa kwenye elimu sasa ndo nilipojichanganya nazani, nikaanza elimu yangu ni Chuo kikuu nimesoma Bachelor of nini nini hapo, ambapo safari hii ilianzia mwaka X darasa la kwanza na kumaliza mwaka X darasa la saba, baada ya hapo mwaka X nikajiunga na secondary mwaka X mpaka mwaka X , then nikajiunga Advance shule X mwaka X mpaka mwaka X , then baada ya hapo nikajiunga na Chuo mwaka X na kumaliza mwaka X ... yaan sikusema kuwa nina skills flan, na experience flan flan.. ni kama tu nilikuwa nawahadthia hadithi yangu na sio kama vile proffesional flan... Basi kazi ile siku ipata japokuwa nilipiga fresh written plus maswal mengine yote ya oral niliyajibu vizuri... baada ya kutoitwa kazini ndo nikajajua namna ilinibidi nilijibu swali hili ambalo huwa linaonekana simpo Kumbee sio.Ulishawahi kuona yale Mazingira ya kushindwa jambo au kukosa fursa kabla hata hujaipata, basi kuna wakati unaweza kujikuta umefeli Interview hata kabla ya kupewa Majibu na Kampuni husika
Umeshawahi kupatwa na hali hii? Nini kilitokea?