Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Mkuu nimeiweka tena link ya youtube utoe maelezo naona bado upo kimya
Okay nimecheki sijamaliza kwanini alichoose from judges hiyo picha iliyotokea na judges ilikuwa edited na tayari ilikuwa imeandaliwa.
Angecfanya hivyo kwa audience wa nyuma watatu tungemkubalia lakini tumeshaelewa alichofanya hakuna kitu hapo
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
Kichaa chake hakina uhusiano na kitisho alichopewa. Alikuwa ni mtu wa kuwa kichaa, au alipata woga na wasiwasi kwa kuogopa kulogwa na ikawa na effect kwake kiakili.
 
Niliishi nyumba moja magomeni mikumi kwa miaka 7 na wenye nyumba ni wachawi bibi na babu, usiku wa manane nikiamka kwenda uani (kilikua choo cha nje) naskia wanacheza ngoma na kuimba hapo sebuleni kwao,
Siku moja bibi akaniambia wameletewa nyama pori wakanipa hapo sikula kile chakula nkakiweka ili asubuhi niweke kwa mfuko nkamwage maana sikuzielewa zile nyama zilikua kama zimekaushwa hivi ila ukiipasua kati ni mbichi kabisa na waliniwekea nyama nyingi sana, asibuhi mapema naamka nimwage chakula nkakuta nyama zote hazipo na hakukua na panya mle ndani,
Siku nyingine nilisafiri kwenda kijijini nkamuomba babu alale chumbani kwangu ili kusiibiwe (chumba kilikua cha nje) kipindi hicho vibaka wa usiku walikua wanaiba sana, na mara nyingi nilikua nawaona wanachungulia dirishani,
Sasa kurudi safari nilikaa huko kama wiki 2 nkakuta kapeti limetoboka toboka sanaa kama mtu karukaruka na viatu vyenye ncha kali sana nkajua tu hawa washenzi walihamishia ngoma zao chumbani kwangu nkavunga tu wala sikuuliza maisha yakaendelea.
Sijaona kitu chochote kinachoonyesha ni wachawi.
 
Okay nimecheki sijamaliza kwanini alichoose from judges hiyo picha iliyotokea na judges ilikuwa edited na tayari ilikuwa imeandaliwa.
Angecfanya hivyo kwa audience wa nyuma watatu tungemkubalia lakini tumeshaelewa alichofanya hakuna kitu hapo
Kwanini hukumaliza??Nna uhakika umeimaliza.... Umeelewa nni hapo?

Asingemchagua judges ungesema huyo audience wanafahamiana??

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Zipo nyingi angalia mpaka mwisho alafu kosoa si umetaka tukuonyeshe uchawi???
 
Kuna Siku nililala ndani peke yangu, muda wa saa moja asubuhi najiandaa kuamka nikasikia kishindo juu ya bati kama mtu karusha bonge la jiwe . Nikaamka haraka haraka kwenda kuchungulia nje ni nani karusha hilo jiwe. Kwa bahati mbaya sijamkuta mtu. Nikazunguka nje nyumba nzima kulitafuta lilipodondokea sikuliona nikaangaza juu ya bati sikuliona. Nikaamua nirudi ndani kuendelea na ratiba zingine nakuta mlango umefungwa ndani kwa komeo. Nikaita nikidhani kuna mtu nilipishana naye kipindi nazunguka nyumba yeye kaingia ikawa kimya. Nikahisi jambo lisilo la kawaida ikabidi nitafute fundi tukafanikiwa kubomoa mlango. Tumekagua vyumba vyote hatukuona mtu.
Kuna popo wakubwa au bundi wanaweza kuponyokwa na windo walilobeba. Kuhusu mlango ulikuwa unafunga kwa kutumia nini? Kitasa? Komeo?
 
Kwanini hukumaliza??Nna uhakika umeimaliza.... Umeelewa nni hapo?

Asingemchagua judges ungesema huyo audience wanafahamiana??

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Zipo nyingi angalia mpaka mwisho alafu kosoa si umetaka tukuonyeshe uchawi???

Nimetazama scenario ya pili tazama camera jinsi zilivyo alipozunguka nyuma obviously hapo mtu alikuwepo ndani ya kikabati hata vitabu vilikuwepo hapo hapo hata mshumaa umewashwa camera hazionyeshi ndani.
Hiyo ni michezo ya kuigiza tu
Inahitaji mazoezi ya muda mrefu

sijaona hata moja la ajabu zaidi ya play kuwa staged
 
Kwanini hukumaliza??Nna uhakika umeimaliza.... Umeelewa nni hapo?

Asingemchagua judges ungesema huyo audience wanafahamiana??

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Zipo nyingi angalia mpaka mwisho alafu kosoa si umetaka tukuonyeshe uchawi???

Mimi nafahamu uchawi ni vitu vya kufikirika ambavyo kwangu havina ukweli mfano mtu kuyayuka, kugeuka kuku n.k
Claim yangu nataka mtu athibitishe kuwa yupo mtu kafanikiwa na uchawi

Na swali kama unaamini riana sacred anaweza fanya hayo mambo in reality na siyo kitu kipo staged kafata nini kuanzia audition mpaka ku perform kama si pesa?
Muda mwingine jiulize maswali basic tu ambayo hayahitaji elimu kubwa
 
Kuna popo wakubwa au bundi wanaweza kuponyokwa na windo walilobeba. Kuhusu mlango ulikuwa unafunga kwa kutumia nini? Kitasa? Komeo?
Mlango haukuwa na kitasa . Ni komeo tena la kulala. Ambalo lipo katikati ya mlango kinapokaa kitasa
 
Mimi nafahamu uchawi ni vitu vya kufikirika ambavyo kwangu havina ukweli mfano mtu kuyayuka, kugeuka kuku n.k
Claim yangu nataka mtu athibitishe kuwa yupo mtu kafanikiwa na uchawi

Na swali kama unaamini riana sacred anaweza fanya hayo mambo in reality na siyo kitu kipo staged kafata nini kuanzia audition mpaka ku perform kama si pesa?
Muda mwingine jiulize maswali basic tu ambayo hayahitaji elimu kubwa
Sasa hayo yote yanafanyika kwenye stage na mashabiki wakiwepo unafuatiliaga AGT wewe au unakaza fuvu???

Unasema kwenye box kulikua na mtu mbona amelifungua hakuna mtu?? Hata angekuwepo angeweza kuenea???

Hata huku watu wa mazingaombwe wapo

Yess tuseme kafuata hela inahusianaje??
 
Mlango haukuwa na kitasa . Ni komeo tena la kulala. Ambalo lipo katikati ya mlango kinapokaa kitasa
Inawezekana katika kutoka na wenge ukaubamiza ukajifunga. Sidhani kama kuna uchawi wowote hapo. Vitu kama michanga au mawe kuanguka mabatini hata mimi zamani nilikuwa napatwa wasiwasi lakini nikajafanya utafiti nikajua kuwa popo na bundi huwa wanaangusha vitu usiku. Hasa popo wanaangusha vitu vinavyolia kama mchanga kwenye bati ila siyo mchanga ni majimaji (mavi?)
 
Sasa hayo yote yanafanyika kwenye stage na mashabiki wakiwepo unafuatiliaga AGT wewe au unakaza fuvu???

Unasema kwenye box kulikua na mtu mbona amelifungua hakuna mtu?? Hata angekuwepo angeweza kuenea???

Hata huku watu wa mazingaombwe wapo

Yess tuseme kafuata hela inahusianaje??
Ni wewe hukuona tu sababu tayari upbeat na appearance ya riana imekufanya ukose focus.

Umefika sabasaba kumuona jamaa anajikunja kama tairi? Akaulizwa inachukua muda gani akasema yeye ni miaka saba mpaka kufanya hivyo.vipi ishindikane mtu kuwepo pale na camera ziamishwe na light ziwe dark in a sec tatizo akili YAKO ilishaamini uchawi lakini ni huoni tu kaa tazama taratibu.

Kwanini afate pesa na anao uwezo wa kuonyesha kitabu kisichoandikwa kikawa na maandishi na kuwasha mshumaa kwa kuangalia kwa njia ambazo wewe umeona kawasha ILA obviously hakuna alichofanya zaidi ya kuwepo na mtu hapo.
The last part ya kujitazama kwenye kioo ni kama movie za horror zinavyotengenezwa.
 
Tuje kwenye sayansi, kwanini sayansi imeshindwa kutuonyesha upepo upoje ni unavuma tu sayansi haiwezi kufanya chochote kuhusu upepo, kwanini tusiifanye dunia ikawa usiku tu au ikawa mchana tu, au tukasimamisha mda au tuurudishe mda nyuma. Hatuwezi kufanya jua lichomoze magharibi? why science has nothing to do with this?
(Nb usije ukasema hiyo yenyewe ni sayansi)
🤣🤣🤣Sayansi kazi yake sio kufanya miujiza. Kazi ya Sayansi ni kuelezea why things happen in the laws of nature. Niambie Nini hujui kuhusu upepo? Jua halichomozi popote because dunia inazunguka jua not otherwise na bible na Quran hawakujua Hilo mpaka Sayansi, 🤣,kwa vitu ulivyosema they are impossible. Na Kama unasema ni proof ya uchawi bac tumia uchawi kufanya hivyo vitu afu utuite sawa
 
Back
Top Bottom