Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Niliishi nyumba moja magomeni mikumi kwa miaka 7 na wenye nyumba ni wachawi bibi na babu, usiku wa manane nikiamka kwenda uani (kilikua choo cha nje) naskia wanacheza ngoma na kuimba hapo sebuleni kwao,
Siku moja bibi akaniambia wameletewa nyama pori wakanipa hapo sikula kile chakula nkakiweka ili asubuhi niweke kwa mfuko nkamwage maana sikuzielewa zile nyama zilikua kama zimekaushwa hivi ila ukiipasua kati ni mbichi kabisa na waliniwekea nyama nyingi sana, asibuhi mapema naamka nimwage chakula nkakuta nyama zote hazipo na hakukua na panya mle ndani,
Siku nyingine nilisafiri kwenda kijijini nkamuomba babu alale chumbani kwangu ili kusiibiwe (chumba kilikua cha nje) kipindi hicho vibaka wa usiku walikua wanaiba sana, na mara nyingi nilikua nawaona wanachungulia dirishani,
Sasa kurudi safari nilikaa huko kama wiki 2 nkakuta kapeti limetoboka toboka sanaa kama mtu karukaruka na viatu vyenye ncha kali sana nkajua tu hawa washenzi walihamishia ngoma zao chumbani kwangu nkavunga tu wala sikuuliza maisha yakaendelea.
 
duh
 
Nikiwa shule msingi miaka ya nyuma nikitoka shule Mwadui shinyanga ndani ya mgodi nilipishana na mtu tulipokaribiana nilishangaa kuna nguvu inanilazimisha kumpisha yule mtu umbali wa mita 5 pembeni mwa barabara hadi baada ya kupishana ndipo nikarudi barabarani. Hadi leo sijapata majibu yule mtu alikuwa na nguvu gani. Maana watu huwa wanapishana nusu mita au mita.
 
Uliwezaje kukaa na hao watu mud wote huo bila kudhurika??
 
Pana nyumba niliishi mwanga kigoma sebuleni kwa mwenye nyumba pana karatasi juu Ina maandishi ya kiarabu imening'izwa ukitaka kuisoma inageuka. Pili usiku juu ya Bati unasikia vishindo kabisa mtu anatembea au kucha zinakwaruza bati. Kuna siku tunaongea na binti yake akaropoka kwamba hata ukiingiza mwanamke ndani usiku sisi tutajua.
 
Kuku mzima anatamkiwa maneno mpaka nakufa hapohapo
 
Siki moja Ungejaribu kumvusha huyo binti chumban kwako uone kitatokea nn
 
Sasa hapo ndio uchawi au
 
Ila kweli we ndio yule mchawi haendi kwa mentali yani huna habari
 
Ilishawahi kunitokea kama hiyo mwaka 2010 oktoba. Sema mimi uvumilivu ukanishinda nilitoka nduki kubwa sana kwa sababu nilivyokuwa napishana naye nikawa nashindwa kuongea halafu kama akili inapotea hivi.
 
Nina visa name shuhuda nyingi mno
 
Una kinga kubwa kiroho aisee huyo hakuwa mtu bali roho baya lililotumwa kukuziba njia ili ugongwe na gari ufe malengo ya mbaya wako yatimie afurahi kuwa kakuweza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…