Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

ignore cause ignorance
kupuuza kunasababisha Ujinga.

Achana nae mjinga huyo.
 
Nipo wilaya ya Mbarali ambapo shughuli kuu ni kilimo Cha mpunga. Ekari Moja ukiihudumia vzuri kabisa inaweza kukutolea gunia 25-28 za debe Tisa. Ila Kuna miamba inakutolea Hadi 40 ukizingatia kwamba kanuni za ulimaji ni zile zile hakuna mpya Yani unachofanya wewe na Mimi nafanya vilevile au kukuzidi kabisa.
Mara nyingi Hawa jamaa unakuta wanakuwa wa mwisho kutoa mazao Yao shambani, mtatoa woooote yeye anakuwa wa mwisho. Hii kitu sikuwahigi kuielewa but ukiwaza vizuri unaona kabisa kwamba Kuna namna nyuma ya pazia, nayo ni hallucination??

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Nawajua wale si wanaishi kidodi pale, zamani wakati naenda ifoza likizo za primary nilikuwa nashangaa makaburi yapo sebleni. Yaani ukifungua mlango ule unaotazama road unashangaa kaburi holoo badala ya makochi aua viti.
 

Umejielezea vzuri ILA umeniangusha kusema kuna namna nyuma ya pazia!

Ulipaswa uthibitishe namna nyuma ya pazia kwa kutupa positive link up na wao kupata mazao mengi zaidi ya wengine regardless wamefata kanuni Sawa.

Shida ninapowashinda ni mimi naelezea jinsi mtu anavyofanikiwa kwa kufanya kazi.

Siwezi kuelezea kilimo sina experience nayo

Njia rahisi ya wewe kuprove wrong nachoongea ni kunipa sababu shida mnaishia kusema nyuma ya pazia.
 
Inakuaje niko sahihi kwa kitu ambacho si cha kweli ikiwa uhalisia ni kwamba wewe gari unalo na si kwamba hauna gari kama ambavyo mimi navyosema?

Kanuni ni hii

"Everyone is innocent until proven guilty"
Thibitisha kuna mtu kafanikiwa kwa uchawi?
 
[emoji38]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipe mfano.. halisi Sasa...hela zinapotea ndio. Uchawi umeingiaje Sasa? Kwani hela hazipotei? Zinapotea. So uchawi umetoka wapi.
Inaonyesha ndio mara ya kwanza hata kusikia kuhusu chuma ulete, hujui hata naongelea nini, ndio maana nasema mnapinga kitu ambacho hata hamkielewi.
 
Pamba bado unazo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nicheki dm tumsaidie huyo ndg yako
 
Mwili hujitibu wenyewe, soma biology o level utanishkuru. unaweza usinywe dawa na upone. Kunywa maji mengi it's also a healing mechanism. Hamna uchawi hapa. Anything else?
Nimekuuliza unajua tiba ya kutumia maji tu ya kunywa? Badala ya kujibu unaanza kusema mara mwili unajitibu wenyewe mara hakuna uchawi, mbona unakuwa kama umewehuka?

Umewahi kusikia tiba kwa kutibu maradhi mbalimbali kwa kutumia maji tu ya kunywa?
 
Kanuni ni hii

"Everyone is innocent until proven guilty"
Thibitisha kuna mtu kafanikiwa kwa uchawi?
Kwahiyo hata wewe unayesema hakuna uchawi yawezakuwa uchawi upo kweli?

Ok wewe umeweza kuthibitisha mafanikio ya mtu kwa sababu ya kufanya kazi tu? Hebu tuweke uchawi pembeni, kuna watu tunawaona wanafanya kazi na wana maendeleo ila unawezakukuta nyuma ya pazia kuna ujambazi au rushwa na ukwepaji kulipa kodi. Je nikisema huyu mtu mafanikio yake ni huko kukwepa kulipa kodi nitakuwa nakosea?
 
Anayeamini uwepo wa Mungu na anayeamini uwepo wa uchawi WOTE wapo kundi moja la Metafizikia!
Unadhani bas wanakuelewa. Watu wamesoma kwenye GS haya mambo ila hawajui coz wanasomea vyeti. Mtu unasoma ufanye mtihani ufaulu ukitoka hapo hata mdogo wako kumsaidia huwezi...ndo shida ya watanzania. Afu mnalaumu elimu jau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…