Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kuona Bwana Maduhu nyanda a.k.a Kiranga akipinga uchawi baada ya kwenda USA kwa Dada yake na anapolala sebuleni kwa dada yake wakati ni msukuma wa Misoji Geita alipokuwa anacheza ngoma za majoka huku akifanya Chagulaga. Hapa pamenifanya niamini uchawi wa kizungu upo.
 
Sawa mimi nachagua kuwa na mihemko naona inanisaidia zaid.Na pia ndio my generation..i cant live the past where am no existing
 
Nimeuliza kwanini hizo hallucinations huwatokea sana walinzi wa mashuleni, madereva wa magari makubwa, wavuvi huko baharini na kuna baadhi ya maeneo ubakuta kuna njia hujulikana sana kwamba hutokea sana hizo hallucinations. Kitaalamu hiyo ikoje maana unaweza ukawa wewe ni mgeni ukapita eneo bila kujua kama huwa kunatokeaga mauzauza ila nawe unajikuta unapatwa hiyo hallucination je hiyo ikoje?

Binafsi nakumbuka wakati niko mdogo kipindi cha likizo nilikuwa naenda kwa ndugu kutembea huko, sasa tatizo kulikuwa na chumba hicho ambacho ndio kilikuwa cha watoto wa kiume ila ilikuwa mimi nikilala basi siwezi kuumaliza usiku yani lazima tu nitaota ndoto mbaya na kupiga kelele hadi nahamishwa chumba na kwenda kulala chumba kingine.
Baadaye nikaja kujuwa kuwa kile chumba kiliwahi kutumika na mganga kwamba kilikuwa kilinge.

Lakini tukio kama hilo pia lishawahi kuwa linamtokea rafiki yangu nae alipanga chumba akawa anaona mauzauza na ndoto mbaya baadaye wapangaji wenzake wakaja kumwambia kuwa hiko chumba ndio kilivyo kilikuwa kinatumika na mganga.

Mtaalamu haya unayazungumziaje?
 
Kila mtu anapima huo upepo au kwamba anakubali uwepo wa upepo kwa sababu tu unapimika kwamba usingepimika asingekubali uwepo wa upepo?
 
Basi msipende kulihusisha hilo neno uchawi kwenye kuzungumzia kutokuendelea kwa afrika, waarabu wametupita kimaendeleo na ndio wanaamini dini na uchawi pia.
 
Sawa mimi nachagua kuwa na mihemko naona inanisaidia zaid.Na pia ndio my generation..i cant live the past where am no existing
Uko sahihi kufanya Uchaguzi. Ila spiritually hakuna mpaka huo wa Past or Future, hakuna mipaka hata ya nafasi ya hapa na pale, maana hicho mkiitacho Mungu ni Ukamilifu(Limitless). Jana ni Leo na Leo ni Jana, ni katika udhaifu wa mwili tu ndio tunaona hilo.
Hivyo katika kuchagua udhaifu wako hiyari ni yako.
 
Sawa... So how do u know it's uchawi...
Mimi binafsi sijasema kuwa ni uchawi ule au siobuchawi, hivyo mtazamo wangu ni kuwa yaweza kuwa moja wapo kati ya hayo mawili kuwa ni kiwewe tu cha kawaida au pia ni ushirikina kwa sababu michezo hiyo ipo.
 
Mbona unajichanganya mara utajiri wao ni kwa sababu ya mafuta tu na sijui ule uwekezaji ni wa wazungu mara tena waarabu wamesoma na wengi hawaamini uchawi siku hizi, sasa hapo mie nielewe lipi kuhusu hao waaarabu?
 
😂Kwa Nini wasipatie mda wote. Kwa Nini mganga huyo huyo aliyetatua tatizo la mmoja mwingine akienda anashindwa. Au huyo mwingine hakuwa na Imani...😂ehe tuambie mkuu
Haujafafanua wanabahatisha vp? Kabla mie sijajibu maswali yako kwanza elezea nielewe ni vp wanabahatisha maana ni neno tata kwa hapo, kwa sababu kubatisha kunaweza kuwa umejaribu kitu fulani na ikatokea kama matokeo ambayo ulikuwa unatamani yatokee ila kwa bahati tu hukuwa na uhakika itatokea hivyo au hukuwa ukijua unachofanya kama kitaleta hayo matokeo.

Au ni vp hasa huko kubahatisha?
 
Mkuu,

Nimekukosea nini mpaka ukanipa maneno haya ya uongo na ya kunidhalilisha hivi?

Au unatafuta kiki kwa kutumia jina langu tu?
 
Miaka ya nyuma kidogo nilikuwa naishi Kwa shangazi yangu Sengerema mtaa mmoja unaitwa migombani sasa Kuna Mzee mmoja alikuwa anafanya kazi buhindi forest na makazi yake makuunyalikuwa katwe kahunda.Sikunmoja akaja kuniomba niwe mwangalizi wa nyumba yake na akanipa chumba kuwa nalala pale.Sasa pale kulikuwa na wapangaji wawili mpangaji mmoja alikuwa single mother alikuwa muuza ndizi ila alikuwa kasafiri kwenda Itabagumba.Mpangaji mwingine alikuwa jamaa mmoja aliyekuwa anaendesha gari ndogo za kutoka sengerema mpaka Nyakariro-kome mchangani alikuwa na mke wake na walikuwa na mtoto mmoja.Sasa Huyu dreva alikuwa ni Malaya sana kiasi kwamba Kuna muda alikuwa anarudi nyumbani usiku wa manane au asirudi.Siku zimeenda mke wake akawa anakuja nyumbani kutueleza Kuna wachawi wanamchezea,tukawa tunaishia kumpuuza tu.Siku Moja majira ya saa nne na nusu usiku akaja nyumbani anahema huku akisema huwa tunampuuza twende tukashuhudie.Tulivyofika akafungua mlango wa chumba chake Ile kufungua tunaona neti inajitupa kutoka upande mmoja wa chumba na kuelekea upande mwingine Kwa Kasi.Basi wenzangu wakarudi nyumbani Kwa mshangao Mimi pia nikafungua chumba changu nikalale.Akaomba aingie na mwanae kwenye chumba changu ili wamsubiri mmewe.Ile anaingia tu zikapita kama dak.2 mlango ukapigwa balaa.Na ikafuatiwa na milio ya paka humo chumbani....Ni simulizi ndefu sana nisiwachoshe ila uchawi upo.....
 
So uchawi unachagua wenye familia..Mara umri Mara Kijiji now wenye familia tu. Mbona Kama mnahamisha goli tu... In short pole kwa lolote unalopitia katika maisha yako, Ila Kuna watu wanapata matatizo na kutafuta majibu halisi na msaada wa kweli...it's better na wewe ufanye hivyo kuliko kutafuta mchawi au jini la kumsingizia
 
😅So tunabishana Kama jua lipo...skia, ☺️Kama hulioni jua unaona majini yako, nenda mirembe
 
😂😂😂Unajikosha Sana, eti Simba ana dini...😂skia usifananishe Sayansi na story za kutungwa sawa..kuwa na heshima Kama huna elimu kalale
 
Sijui umeongea Nini ila...haya bana
 
Bado ni story tu...why uchawi uchague watu..walinzi naweza elezea ni uchovu, au something lyk that I'm not a mental doctor hayo maswali mengi muulizeni muhimbili. Coz I'm sure hata mirembe watu wa hivi wapo. Ni psychology tu..mbona watu kibao duniani wanaishi mpaka wanakufa hawaoni kitu..so unachagua watu au..why specific groups of ppo..Mara Kijiji Mara watu wenye shida Mara watu wenye kazi zenye uchovu Kama ma lorry au walinzi...why not a normal person
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…