Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

ukikutana na mada za kufundisha mambo ya Kiroho unazipita kama huzioni.
Sasa ikija vita ya kiroho ndo hivo.. tunakupoteza tu.
 
Wajibu ni wako, kama unataka tu kuthibitsha sema upelekwe. Itakugharimu nauli yako tu utakutana na wagonjwa wa juzi, Jana na hata wa leoleo. Nawe utaasses majeraha yao, kisha utafuatilia matibabu na uponaji wao.

Zingatia: Sikusema week mbili, NI MOJA TU.


Hizo stori nimeshazisikia kuna mtu kapelekwa huko lindi alipata ajali ya pikipiki kaenda hakuna kitu kilichofanyika ikabidi arudi hospital

Wanajf ni rai yangu kuangalia hawa watu utapeli umekuwa mkubwa sana matapeli ni wengi.

BE AWARE OF SCAMMERS.
 
Story hizi nizakweli kabisa na ninaamini uchawi upo, na hakuna mtu wa kuniaminiaha uchawi haupo uchawi upo.

Kisa 1. Mwaka 2013 nipo Secondary shule moja inaitwa Shinyanga secondary (Shybush) nilikuwa natoka nje ya bweni kukojoa ile naangalia chini nikaona panya wawili wananizuia kupita nikienda huku wananifata nikienda kule wananifata ilikuwa ni getini sasa nikaona hapa sito ingia nikawaruka nikaingia ndani ya bweni kuja kujikuta nimejigonga ukutani bega likashtuka.

Kisa 2. Mwaka huo huo 2013 tukafunga nikaenda mwadui kwa baba yangu mdogo, ile natoka nakatiza uwanja wa Mwadui katikati kipindi hicho kulikuwa hamna fence akatokea mwewe kama mlisikia mwewe kabeba Ng'ombe Sumbawanga basi ndio ilitaka kunikuta yule mwewe alifika na kunipiga kichwani ni kama nataka kubebwa hivi. Niliona nikama nimetuliwa na tofali kichwani kumbe mwewe.
Nilikuja kujishika kichwani kumbe nimekwaluliwa [emoji24][emoji24] huyo mwewe alinifata mpaka nilipo kuwa naenda, nikafika namuona tu yupo juu anazungukia maeneo yale basi nikaingia nikakaa kama saa hv ndani ile natoka nikamkuta anazungukia tu maeneo yale [emoji23][emoji23] nikatoka hapo nikaenda sehemu ambayo huwa nalala aisee bdo alinifata tu mpaka hapo nikaingia ndani nayeye nikamuacha anazunguka juu nikalala zangu mpaka usiku ndio nikatoka.

Kisa 3. Niliajiriwa kijiji x nikawa nimeenda kama Muuguzi, Akatokea mjamzito nikamzalishe sasa akawa anashida fulan za uzazi nikatoka nje nikamuite mwenzangu ili tupeane ushauri jinsi ya kumsaidia ile navuka barabarani namuonga mtu kavaa kaniki nyekundu na nyeusi nikajikaza nikasema sasa huyu namsalimia badi nikawa nimemsalimia masna alikuwa bize anainama mara anainuka nikawa nageuka geuka nyuma yupo pale pale nilivyo enda na kurudi hayupo.

Visa nilivyo pambana navyo ni vingi ila niishie hapo, na sio Hallucinations.
 
Ndio...watu wanaoamini uchawi most of them ni watu wa uswahilini, au vijijini watu ambao hawana elimu au fikra za kisayansi...wanaendeshwa kwa hisia na upepo wa fikra za jamii.

Ngoja nikupe story ndugu nina kishamba changu maeneo ya machimbo kwa mzee limboa chanika mbele ya kwa mstaafu simon siro.

Kuna huyo mama anaendekeza sana haya mambo na mtoto wake,
Ile sehemu wengi ni wastaafu wamenunua mashamba tena wanajeshi na maaskari na yeye ndo alikuwa mtu wa mwanzoni maeneo hayo.

sasahivi kuna majumba makubwa ni yeye pekee amebaki na nyumba ya udongo. Mpaka chumvi anaomba

Funny enough akaanza kuwadanganya watu kwamba ndani kwake kuna madini ety majini yamemuonyesha ikabidi awaite vijana wa machimbo.

Ndugu yangu simbampole walichimba shimo refu ndani siyo nje na hakuna kilichopatikana.

Hawa watu wengi huwa Wana matatizo ya akili. Ila kadri siku zinavyoenda wataelimika
 
Kiboko ya wachawi ni nguvu ya Mungu tu iliyopo ndani ya damu ya Yesu.........washauri ndugu zake wampeleke kwenye kanisa lolote akaombewe apokee uponyaji.
 
Sijasema computer fictions jamani afu unakera kinoma....unazunguka hapa hapa. Nimekuambiaje, tafuta breaking the magician codes au video zinazoelezea mazingaombwe na wewe uelewe. Kama hutaki acha, Baki kuamini kuwa ni uchawi. Ile ni talent Kama zingine tu, Kama mtu kujua kudance lazma ujifunze skills fulani
Kwanza Mimi sijasema Mazingaombwe ni Uchawi... Ila ni wewe unayefikiri Uchawi ni sawa hayo Mazingaombwe.
Ninachokuambia hiyo Talent kwa asiyeijua ndio anaita Uchawi. Kama wewe na wenzako msivyojua talent ya matibabu pasi na kushika mgonjwa, Mtaita Uchawi.

Ni wewe ndio uliyeniambia nitazame Behind The Scenes, kama sio unafikiria Mazingaombwe ni Movie za Mazombi, sema basi behind the scene zake uliziona wapi?
 
W
Si ndo Sayansi yenyewe...hayo matibabi asilia ni Sayansi...Sayansi sio lazma uchomwe sindano...hujui Sayansi ni Nini ndo maana unaongea ujinga tu..hujui hata uchawi wenyewe unaoongelewa huku ni Nini...hatuongelei kutibu kutumia miti... tunaongelea watu kutokewa na majini usiku...so rejea kichwa husika please
Wewe hujui Uchawi ni nini na yaweza kuwa unauishi.

Nilikuuliza je Umeshawahi kwenda kwa mganga wa kienyeji, ukajibu ufuate nini!
Sasa labda nikujuze, WAGANGA WA KIENYEJI(TIBA ASILIA) NI MIONGONI MWA WATU WAFAHAMIKAO KUWA WACHAWI.

Ukifikiri Tiba Asilia ni wa Kina Ndodi tu, umepotea. Tiba Asilia ina ramli, INA masharti ya njia panda, ina tunguli, ina makaburi, ina manuizi, nyota, nyungu, nk....

Ushamba ni mzigo!
 
Si ndo Sayansi yenyewe...hayo matibabi asilia ni Sayansi...Sayansi sio lazma uchomwe sindano...hujui Sayansi ni Nini ndo maana unaongea ujinga tu..hujui hata uchawi wenyewe unaoongelewa huku ni Nini...hatuongelei kutibu kutumia miti... tunaongelea watu kutokewa na majini usiku...so rejea kichwa husika please
Uchawi si kuloga tu kupata hela, Uchawi ni kufunga mwizi asiibe, Uchawi ni kufunga mke asichepuke, Uchawi ni kuchanja mifugo iongezeke, Uchawi ni kujua usalama wa safari yako, Uchawi ni kujua wabaya wako, Uchawi ni kutibu magonjwa yako, Uchawi ni kinga, Uchawi ni silaha, Uchawi ni kila kitu...

Sasa nitafute Tujaribu hilo la Wizi, nikuelekeze mahali ambako utatumia sayansi yako ya kukaririshwa ukaibe, kama utatoka salama.

Umesema una watoto, lakini ajabu unawaza kama watoto wako.
 
Hizo stori nimeshazisikia kuna mtu kapelekwa huko lindi alipata ajali ya pikipiki kaenda hakuna kitu kilichofanyika ikabidi arudi hospital

Wanajf ni rai yangu kuangalia hawa watu utapeli umekuwa mkubwa sana matapeli ni wengi.

BE AWARE OF SCAMMERS.
Kama unaamini stori za kusikia dhidi ya stori za kuthibitisha mwenyewe, umefanya chaguo jema.
 
🤣Bac mkishajulikana kuwa official doctors nitaenda. So far Nina Imani na ujuzi wa madaktari waliosomea mwili wa binadamu kwa miaka 7 na miaka mingi ya uzoefu
Hujakutana na maswaibu wewe! Unaweza kwenda na dalili zote za kisukari hospital hao madaktari wako waliosoma miaka 7 wengine 10 kila wakipima hawaoni ugonjwa..pima pima hawaoni ugonjwa ila una dalili zote za mgonjwa wa kisukari..mwisho wa siku hao hao madaktari wanawaambia go back to the roots..

Hapo sasa ndipo yanapoingia mambo ya Kiroho ambayo ni beyond human scope ni wachache wenye kuyafahamu.Sasa hapo ni wewe kwenda kuombewa au kwenda kutibiwa kienyeji.

Wanakuambia Ukiujua ulimwengu wa Kiroho unavofanya kazi Utamiliki na kutawala..maana mambo yote unayoyaona mwilini chanzo chake ni Ulimwengu wa roho.

Nyongeza: Maisha yetu wanadamu tunayoishi na mambo tunayofanya yameanzia rohoni yawe ya mafanikio, umasikini,kukuharibia maisha e.t.c..hata magonjwa unayoona mfano mtu kisukari, kansa, ukimwi, e.t.c akienda kuombewa au kwa waganga unasikia watu wamepona chanzo cha hayo yote utatuzi/solution yake ni Rohoni.
Mganga au mchawi wana access na mambo ya rohoni.Ndo maana wao wakiamua kuua mtu au kukamata wezi huji kusikia anakuja physcially anatega kwa sayansi yake na unajaa.

Take care, Usibishe usivovijua
 
Sijasema computer fictions jamani afu unakera kinoma....unazunguka hapa hapa. Nimekuambiaje, tafuta breaking the magician codes au video zinazoelezea mazingaombwe na wewe uelewe. Kama hutaki acha, Baki kuamini kuwa ni uchawi. Ile ni talent Kama zingine tu, Kama mtu kujua kudance lazma ujifunze skills fulani
Hakuna unalojua wewe!Bure kabisa...! Nashangaa hata watu wanaokujibu! Unaweza ukawa una type upo sebleni kwa shemeji hapo unaangalia katuni..!
 
1. Pope kafanyaje?
2. Huyu mdada ni tricks za magic Kama nyingine tu...jifunze code zao utaelewa video zipo kibao YouTube Kuna Hadi vipindi vya breaking the magician code...vinaelezea mazingaombwe Yanavyofanywa hata we ukijifunza unafanya ni akili tu
3. Halloween ni tradition, ni kama Christmas..kule wenzetu Christmas wanaita happy holidays na ni sikukuu coz of tradition.. Halloween kwao si kwamba wanalogana na kufanya uchawi...no wanahave fun kuvaa nguo za kichawi na kutembeleana ni sikukuu tu haina uchawi.
Bado hujaprove kwamba jamii za wazungu zinaamini uchawi.
1:Kazi ya huyo pope ilikua ni kutoa majini na wachawi

2:Trick gani?? Leta hiyo video itakayoprove hizo tricks za huyo dada acha kuongea kwa maneno
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]We ungepata chance ya kupata million 500 ya bure ungekataa...hamna kitu Kama hicho...ni wivu tu wa maendeleo. Eti hutaki shortcuts...
Every action has an equal and opposite reaction, ukiielewa hii vizuri hutawaza kuhusu 500 ya Bure Wala shortcuts

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom