Kitu gani unakumbuka zamani ukiwa mdogo mkicheza mpira wa 'manailoni'?

Kitu gani unakumbuka zamani ukiwa mdogo mkicheza mpira wa 'manailoni'?

Kama huna kiwango kama watu hawatoshi we ndo unachaguliwa ila ujue hawachelewi kukufanya sub au unakaa kipa.

Kama we ni mwenye mpira na siyo mbabe kumaliza mechi unadaka mpira unatoka nduki kuelekea nyumbani.

Kama huna namba lazima unifanye rafiki wa mwenye mpira kinafki.

Wenye hasira ambao hawakupata nafasi mpira ukitoka badala ya kurudisha wanauongezea spidi uende mbali wachukue wenyewe.

Aisee kulikuwaga na raba za kike zinaitwa LOSSO zinakamba unafunga hadi juu ya henka,mi nilikuwa naiba za dada yangu naenda kupiga nazo mpira

Sent using Jamii Forums mobile app
Zilikua nyeusi hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa nikipendwa na mademu nilikuwa messi wa kipindi hichi wanakushangilia mpaka wanajifunua
 
aisee mm nlikua nna timu mbili nachezea,ya mtaa ninapoishi na nyngne mtàa wa pili washkaj nnaosoma nao.kimbembe itokee mechi izo timu zinakutana nlikua naonekana msaliti upande mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah kuna jamaa alikuwa anaitwa zakaria yeye ndo alikuwa mmiliki wa mpira shida alikuwa anapenda sana chenga na mchoyo wa pasi kibaya akipoteza mpira hakabi anasimama tu tulikuwa tunamaindi sana tatizo ukimtoa anabeba mpira wake anasepa mechi inaishia hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah nakumbuka hiyo kitu.
Yaani Ilikuwa hakuna jezi,mnaanza kucheza kwanza halafu wanaoanza kufungwa ndio wanavua mashati,so hiyo ndio inakuwa kama jezi waliovua na waliovaa(mashati).
Dah nilikuwa sipendi tuanze kufungwa maana nilikuwa sipendi kukaa tumbo wazi.

Dah kitambo sana.
 
Baada ya fainali ya world cup 2006.kesho yake nilipiga penati panenka kama ya zidane jana yake.huwa sisahau hili tukio.kuna babu alinizawadia 10000.
 
Wakati naanza kuchezea gozi nikiwa kinda tu Nina miaka kumi kulikuwa linanisumbua kutuliza mpaka mkufunzi wa timu yetu ya redlex kids alikuwa anapata tabu kunielekeza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unazingua boss uliwezaje

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikuwa kawaida tu na sikuwahi kufanyia mazoezi.ile mikasi ya ronaldo alipokuwa man u !tumeipiga sana kitaa.pia mwaka 96 nikiwa kama na miaka 8 hivi niliwahi kufunga goli kama la paul gasgoine (gaza).kesho yake tu baada ya kutazama mechi ya uingereza na scotland.kiufupi tungekuwa na mfumo mzuri wa soka kama wenzetu huenda ningekuwa nimestaafu na kina drogba muda huu.na si mimi tu.tanzania kuna vipaji vingi vimepotea.nimewahi kuona wachezaji wazuri sana mtaani .sasa hivi mateja.wanywa gongo.huwa roho inaniumaga sana nikikutana nao .
 
Back
Top Bottom