kenge 10
JF-Expert Member
- Jul 2, 2014
- 1,450
- 2,383
Alaf wenye mipira huwa hawawapendi wapiga madochi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alaf wenye mipira huwa hawawapendi wapiga madochi
Hiyo ya mwenye mpira hatakiwi kukwaza ndio ilikuwa balaa. Kule kijijini kwetu kulikuwa na jamaa anajua kuitengeneza hiyo mpira utadhani ana kiwanda, Basi alikuwa akikwazwa anauchukua mpira wake halafu anamchagua rafiki yake mmoja wanaanza kucheza wao wawili tu. Hapo sasa inaanza bembeleza, anabembelezwa kwa kuahidiwa zawadi lukuki then ndio anakubali.Niliwahi kutoa kucha ya dole gumba baada ya kukosea timing ya kupiga ule mpira. Niliificha home wasijue hadi kidole kikatoa ufunza, dawa ilikuwa ni mchanga tu hadi kucha mpya ikarudi.
Mwenye mpira ndiye hatakiwi kukwazwa, maana anaweza kuuchukua, alafu asiondoke akabaki hapohapo na nyie hamna cha kumfanya
Mkuu kumbe wewe ni dogo sana. Yaani chandimu iliyokuwa balaa ilikuwa ya 70s, 80s na kidogo 90s. Hiyo ya 2000+ ilikuwa sio tamu maana TV zilikuwa zipo kibao.Baada ya fainali ya world cup 2006.kesho yake nilipiga penati panenka kama ya zidane jana yake.huwa sisahau hili tukio.kuna babu alinizawadia 10000.