Kitu gani unakumbuka zamani ukiwa mdogo mkicheza mpira wa 'manailoni'?

Hiyo ya mwenye mpira hatakiwi kukwaza ndio ilikuwa balaa. Kule kijijini kwetu kulikuwa na jamaa anajua kuitengeneza hiyo mpira utadhani ana kiwanda, Basi alikuwa akikwazwa anauchukua mpira wake halafu anamchagua rafiki yake mmoja wanaanza kucheza wao wawili tu. Hapo sasa inaanza bembeleza, anabembelezwa kwa kuahidiwa zawadi lukuki then ndio anakubali.
 
Baada ya fainali ya world cup 2006.kesho yake nilipiga penati panenka kama ya zidane jana yake.huwa sisahau hili tukio.kuna babu alinizawadia 10000.
Mkuu kumbe wewe ni dogo sana. Yaani chandimu iliyokuwa balaa ilikuwa ya 70s, 80s na kidogo 90s. Hiyo ya 2000+ ilikuwa sio tamu maana TV zilikuwa zipo kibao.
 
Kuna mambo yanafurahisha sana...
  • Mwenye mpira akiitwa mpira umekwisha.
  • Mwenye mpira akichoka half time.
  • Ukimuumiza mwenye mpira ujue wewe ndiyo huchezi tena.


Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…