Kitu hiki kimoja unachokosa ndiyo kitakachokuzuia usipate mafanikio makubwa

Kwanini usitumie huo "ubatizo wa moto" ili ufanikiwe badala yake umekuwa mjasiriamali wa kutuuzia vitabu?

Jombaa ukweli ni kwamba kwenye mafanikio/fursa huwa hatualikani.

Ila nakutakia kila la kheri maana kuna utakaowakamata.
Asante mkuu,
Karibu sana.
 
JF ina wasomi ambao tuna PhD lakini pia tuna elimu kubwa ya maisha, ya biashara, ya kupambana, na ya mafanikio. Kwa hio nenda ukatafute platform nyingine ya kuwadanganya watu. JF umegonga mwamba.
Una phd halafu hujui nini maana ya mafanikio.
 
Unakaribia miaka 10 ya uandishi makala. Unaandika lakini you probably do not walk the talk. Manake unaongea tu lakini unachokiongea haukifanyii kazi ww binafsi katika maisha yako. Kwa kifupi Ww ni msanii kweli kweli 😂😂😂😂
 
Wewe unao ubatizo wa mafanikio? Umefanikiwa katika lipi?
 
Mkuu wewe mtunzi wa Hiko kitabu umefanikiwa?
Tuanzie hapo kwanza
Kama umefanikiwa tuelezee mafanikio yako,
Kama hujafanikiwa endelea kujisomea ulichokiandika katika kitabu chako ukifanikiwa angusha Uzi hapa Jf tutakuelewa
 
Uko sahihi mkuu, huyu jamaa anataka kufanikiwa kwa kupanda mgongoni kwetu. Eti anatuonea huruma sisi ambao hatujafanikiwa. Toka lini mtu aliyefanikiwa akakuuzia mbinu ya kufanikiwa! Ahahhaah hadanganyiki mtu hapa.
 
Ktk sehemu nimeona unarukia vitu Ni hapa, Trump sio mtu wa kumsifia kwa chochote kile.Very unethical man kwny biashara,integrity yake Ni Zero kabisa na Wala hakuna brand/watu wenye reputation wanaojihusisha nae kwny biashara.Na kikubwa mpk Sasa Trump anavimba tu Wala sio bilionea Ni madeni matupu yanamzunguka.Kama unabisha khs hili tunaweza tukaenda sambamba hapa nikakuonyesha huyo jamaa Ni muongo na hata mnavyoambiwa khs assets na biz zake nyingi Ni uongo mtupu.
 
Ukiona fursa ujue wewe ndio fursa yenyewe

Umechelewa sana mjomba enzi ya vitabu vya kuhamasisha utajiri zimeshapita sasa hivi ni vitendo tu
Binafsi sijawahi kuona kitabu cha mtu aliyefanikiwa akieleza jinsi ya kufanikiwa, zaidi naona vitabu vya hawa makanjanja tu. Ukimuuliza yeye kafanikiwa nini anaona kama vile unamuataki au unamkashifu.
 
Wengi hapa mna mtazamo hasi ambao ndiyo kikwazo cha kwanza kwenye kupata mafanikio kwenye maisha.
Niwakaribishe sana mjipatie kitabu hiki, kitawafungua kwa namna ya tofauti na kuwapa mtazamo sahihi ambao utayafanya maisha kuwa bora zaidi.
Wasiliana na 0752 977 170 kupata nakala yako ya kitabu.
Karibuni sana wote.
 
You can’t sell this bro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…