Kituko: TFF yaishusha Kagera Sugar ,Azam tv yaishusha Stand Utd

Kituko: TFF yaishusha Kagera Sugar ,Azam tv yaishusha Stand Utd

Azam wanayo hiyo system na ndiyo tuwaamn...livescore almost zote zinaenda sawa na Azam..TFF wapo tofauti..itakuwa wanafanya mambo yao manually
Mkanganyiko upo kwenye kumbukumbu za matokeo, inamaana TFF na Azam wanashindwa kuwa na software ambazo ukiingiza tu matokeo msimamo unajipanga tu automatic
 
league table ya Azam ndiyo sahihi mkuu...match zote za ligi na points zinaingia automatic kwenye system yao...TFF wametoa boko
Mi mwenyewe sijaelewa Kwa nini wameishusha kagera sugar .


Kama ligi yetu ni Simba na yanga Tu basi mpira wetu na ligi yetu itabaki hivyo hivyo ya kimaskini.


Tena akili za wabongo wanafurahia timu hiyo kiondoka kwamba hawaitaji ushindani kwenye ligi.


Tungekua na kagera kama 10 hiv lig yetu ingekuwa mbali
 
Goal difference zinafanana...ukienda kwenye head to head stand ana advantage as alimfunga kagera 3-1 kaitaba na shinyanga ilikua 1-1...kwa mantiki hiyo kagera anashuka
Kwani kanuni zinasema hivyo ?
 
Hapana kabla ya game ya jana Stand alikuwa na GD-9.
Kagera alikuwa na GD-11
Jana Stand kapigwa 2-0... Kagera akadroo 1-1.
Maana yake sasa GD inakuwa -11 kwa wote wawili.. kinachofata ni H2H.
Kwani kanuni zinataka tuangalie head to head pia ?
 
Yanga haijawahi kufungwa na timu za mikoani Taifa toka 2009
Hata mwaka huu hamjafungwa na timu ya mikoani taifa...sisi simba tumefungwa na timu ya mikoani na tumechukua kombe....hongereni na endeleeni hivyohivyo...huenda kuanzia mwakani ubingwa na kombe atakuwa anapewa yule ambaye hajafungwa na timu za mikoani badala ya yule mwenye point nyingi
 
Kagera wanasemaje?.. kama wamekubali basi wanajua sheria inasemaje.
Kwanza wewe unamjua vizuri mleta Uzi, ni shabiki wa mikia lia lia. Hapo t.f.f kuna mchezo mchafu unaendelea.
 
Kanuni zinasema head to head itaangaliwa ikiwa goals difference mtalingana Sasa hapo huwezi fika huko wakati Kagera anawastani mzuri
hiyo kanuni ni yako, ila kanuni zetu zilizopitishwa na Shirikisho msimu jana haziangaalii Goal Difference kama kigezo cha pili endapo timu zitakua zimefungana point... kama timu zimefungana point inaangaliwa head to head, imeanza tumika msimu huu
 
hiyo kanuni ni yako, ila kanuni zetu zilizopitishwa na Shirikisho msimu jana haziangaalii Goal Difference kama kigezo cha pili endapo timu zitakua zimefungana point... kama timu zimefungana point inaangaliwa head to head, imeanza tumika msimu huu
ungeweka hata kaatachment tungekuamini mkuu
 
Uamini ili iweje? kama hukujua wakati sheria zinapitishwa ujue saiz ya nini?
Hizo hapo
tapatalk_1559125037655.jpeg
View attachment KANUNI.pdf
 
Ina maana kuna kanuni za TFF na kanuni za FIFA duniani
 
MATOKEO YA KAGERA SUGAR KUANZIA ROUND YA 1-2
1. Kagera 2-1 Mwadui
2. Kagera 1-2 Yanga
3. Kagera 0-0 Lyon
4. Biashara 0-0 Kagera
5. Prisons 2-2 Kagera
6. Mbeya City 1-1 kagera
7. Kagera 3-1 Ndanda
8. Kagera 0-0 KMC
9. Kagera 0-0 Ruvu Shooting
10. Lipuli 0-1 Kagera
11. Coastal 1-1 Kagera
12. Mtibwa 1-0 Kagera
13. Kagera 0-1 Azam
14. Kagera 1-1 Singida
15. Kagera 1-0 Alliance
16. Kagera 2-1 Simba
17. Stand 1-1 Kagera
18. Kagera 1-0 JKT Tanzania
19. Kagera 0-0 mbao
20. Mwadui 4-0 Kagera
21. Yanga 3-2 Kagera
22. Lyon 3-2 Kagera
23. Kagera 2-1 Biashara
24. Kagera 0-2 Prisons
25. Kagera 0-1 Mbeya City
26. Ndanda 2-0 Kagera
27. KMC 0-0 Kagera
28. Ruvu 0-0 Kagera
29. Kagera 2-0 Lipuli
30. Kagera 0-1 Coastal
31. Kagera 2-1 Mtibwa
32. Azam 2-0 Kagera
33. Singida 2-1 Kagera
34. Alliance 2-2 Kagera
35. Simba 0-1 Kagera
36. Kagera 1-3 Stand
37. JKT Tanzania 2-0 Kagera
38. Mbao 1-1 Kagera
MAGOLI YA KUFUNGA: 33
MAGOLI YA KUFUNGWA: 43
MATOKEO YA STAND UNITED KUANZIA ROUND YA 1-2
1. Stand 1-0 A Lyon
2. Stand 1-2 Mbao
3. Stand 1-0 Biashara
4. Yanga 4-3 stand
5. Kmc 2-0 stand
6. Ndanda 1-3 stand
7. Stand 0-0 prisons
8. Stand 0-2 MCC
9. Lipuli 1-1 stand
10. Simba 3-0 stand
11. Stand 2-1 Mtibwa
12. Stand 0-1 Mwadui
13. Stand 1-2 coastal
14. Ruvu 2-1 stand
15. Azam 3-1 stand
16. Singida 0-1 stand
17. Stand 1-1 kagera
18. Stand 1-1 alliance
19. Stand 1-0 JKT
20. Lyon 2-0 stand
21. Mbao 2-1 stand
22. Biashara 1-0 stand
23. Stand 1-0 Yanga
24. Stand 0-0 kmc
25. Stand 2-0 Ndanda
26. Prisons 1-0 stand
27. MCC 1-1 stand
28. Stand 3-2 Lipuli
29. Stand 0-2 simba
30. Mtibwa 2-0 stand
31. Mwadui 1-2 stand
32. Coastal 1-0 stand
33. Stand 1-0 Ruvu
34. Stand 1-1 azam
35. Stand 2-2 singida
36. Kagera 1-3 stand
37. Alliance 3-2 stand
38. JKT 2-0 stand
Magoli ya kufunga 38
Magoli ya kufungwa 50
Kanuni zinasema timu zikilingana points kinachaangaliwa Ni goals difference Sasa hapo Kagera sugar ana -10 Huku Stand utd ana -12 maana yake Stand Utd anastahili kushuka moja kwa moja huku Kagera sugar akitakiwa kucheza play off
Kuna mchezo mchafu unaendelea hapo TFF
Weka kanuni tuone!
Kagera wakajifunze kucheza ligi nzima sio mechi mbili tu za Simba. Nyambaff zao na huko wakashuke hadi daraja la mwisho.
 
Kosa walilofanya kagera sugar limeshawahi kufanywa na Toto african ya mwanza, hawa wote ni mabingwa wa kukamia mechi za simba tu, alafu zingine wanatobolewa

Acha wapate walichochagua.
 
Nadhan kuwepo humu tuu ni dhahiri kila mtu anajua kusoma kanuni hizo hapo juu zimewekwa tuzisome jamani tusikurupuke
 
Back
Top Bottom