Kwenye ukweli usemwe,,maana ukweli utatuweka huru,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Hakuna watu wabaya kuliko mabeberu kama viongozi hawa wa Afrika,,,,Tusipende kuweka visingizio vya ubeberu katika udhaifu wa viongozi wetu,,,,, Hivi beberu ndiye kaharibu soko la zao la korosho,,hivi beberu ndiye kaharibu soko la mbaazi,,,,,hivi beberu ndiye kashindwa kufanya uwekezaji kwenye kilimo, kwa miaka 50 ,badala yake amesema mjenge Reli kwenda Mwanza ,, badala ya kuelekea Mbeya ,,Zambia na Congo ya,,Lubumbashi Kwenye mizigo mingi kuliko huko Congo ya kisangani?
Hivi huyo beberu ndiye anayefanya mpigine risasi kwa sababu tu ya hoja za Demokrasia na Haki za binadamu,, Ndugu yangu,,..Duniani nchi nyingi zimesonga mbele sana Kimaendeleo mbele ya huyo unayemwita beberu/Ubeberu,,,,,,South Korea, Malaysia, Singapore, Hong-kong, Taiwan, Thailand, China, India, Vietnam, UAE
Tatizo letu ni viongozi wanaojifanya Miungu watu kwa sababu tu ya kuwa Maraisi wa nchi,,,,,Hawataki demokrasia ya kweli, hawataki haki za binadamu zitamalaki, wabinafsi, wachoyo, wana roho mbaya,,,,,,,,na Makatili,,,,Nchi haiongozwi kwa majaribio,,,,
Hivi kuna shida gani kwa kiongozi kuruhusu uhuru wa kidemokrasia katika kuchagua viongozi ndani ya nchi yake,,na kama watu wanampenda na kuamini ayafanyayo si watampa nafasi tena,,,kwanini wanataka kung'ang'ania madarakani wakati tunawaona hakuna cha maana wanachoweza kufanya ili kulivusha taifa kwenye maendeleo makubwa ya kama Singapore?
Hivi kweli unataka kutuambia kwamba huo ubeberu ndiyo uliofanya Gadafi afiche zaidi ya Tillioni 80 Ulaya na Marekani
Hivi kweli ni huo ubeberu Uliofanya Gadafi akaifanya Libya kama nchi aliyorithi kutoka kwa wazazi wake, na kuwafanya wananchi wake kama wanyama/Watumwa? Au wewe kwa uelewa wako nchi ni mali ya nani
Tatizo la Congo ni wakongo wenyewe,,,,
Tunaweza kutoboa,, na kufanikisha taifa kuwa la maendeleo na haki,,,cha muhimu tusiabudu viongozi, kwa sababu viongozi hawawi malaika kwa kupata uongozi,,,ni binadamu wale wale kama sisi na wanamapungufu makubwa kama tuliyonayo, sisi(concept of check and balance comes in because of our human weakness) ,ndio maana watu lazima wawakosoe viongozi wao,,,Demokrasia ya kweli ikiruhusiwa itakuwa neema kwa taifa na kwa maendeleo ya nchi yetu,,,,,Ubeberu si mbaya ukifananisha na viongozi wa Afrika,,
Demokrasia ya kweli, haki za binadamu, uongozi wa sheria zilizo bora, uimara wa mihimili ya serikali katika kucheck na kubalance, Mfumo wa Utawala wa Westiminister (Parliamentary Government),
Vyama imara vya upinzani vyenye uwezo wa kucheck na kubalance ndio tunu pekee za kuipeleka Afrika dunia ya kwanza mahali bora katika miaka michache ijayo (Kwa hili Ghana inaonyesha njia chini ya Raisi Mwanasheria /Wakili Akufo Nana ADDO, Otherwise mtaendelea kumtafuta mchawi wa maendeleo ya Afrika,,,mtamsingizia Beberu, mtasingizia laana, mtasingizia resorce Curse (laana ya mali nyingi) Mtasingizia udikteta, Mtasingizia hali ya hewa, mtasingizia Word Bank na IMF,, mtasingizia Mchina,,,na viongozi wenu watakuwa hawawajibiki kwa kisingizio cha huyo huyo beberu,,, viongozi wenu watakuwa wanaiba mali zenu na kuzipeleka Ulaya,, mkiuliza kwanini hampigi hatua ,,watasingizia huyo huyo beberu,,,,,,kazi kwenu,,,,,,hata Mwalimu Nyerere kiongozi wenu aliposema ili tuendelee,,hakusema tupambane na beberu,,,, na kwamba kama yupo hatuwezi kuendelea. Tanzania siyo kisiwa,,itashirikiana na wenzake ili kupiga hatua za kimaendeleo,,,hata wakati wa utawala wa Kilwa empire,,ilishirikana na mataifa mengine na kupiga hatua kubwa,,,,Akili mukichwa nimemaliza....Mungu akusaidie,,akupe maarifa,,na aendelee kukufunua ubongo ili uijue kweli,,na kweli ikuweke huru.