Uchaguzi 2020 Kituko: Tundu Lissu na CHADEMA wanaamini mkoloni angetoa ''haki'' waafrika wasiongemkataa

Uchaguzi 2020 Kituko: Tundu Lissu na CHADEMA wanaamini mkoloni angetoa ''haki'' waafrika wasiongemkataa

Duh kwahiyo makaburu wangetoa "haki" wasauzi wangeridhika kutawaliwa na wazungu?
..Afrika Kusini ilikuwa nchi huru[wengine wanaita wa bandia] wakati Mzee Mandela na wenzake wako gerezani.

..kilichokuwa kinapiganiwa pale ni HAKI kwamba mfumo wa utawala uliokuwepo ulikuwa hautoi haki sawa kwa raia wote wa Afrika Kusini.

..Zanzibar ilipata uhuru toka kwa Muingereza tarehe 10 Disemba 1963 lakini kulikuwa na figisu-figisu wakati wa uchaguzi na masuala ya ubaguzi na hivyo kusababisha mapinduzi ya tarehe 12 January 1964.

..Tatizo la wana-CCM ni kutokusoma. Hili ni tatizo la Mwenyekiti wao, mpaka huku ngazi za chini na hawa watetezi wa chama kwenye mitandao.
 
Ndugu zangu,

Nikiwa katikati ya shughuli zangu nimesikia kituko toka kwa Lissu na wafuasi wa CHADEMA eti..''pamoja na maendeleo aliyoleta mjerumani alikataliwa na waafrika sababu hakutenda haki'' kwa lugha rahisi ni kuwa mjerumani angetenda hiyo ''haki'' Lissu na wenzake wangefurahia tu angebaki kutawala.

Sijashangaa kwani hata CHADEMA wenyewe wanaamini ni bora leo Robert Amsterdam awe rais wa Tanzania sababu atawapa ''haki'' kuliko Rais Magufuli kwani hatawapa ''haki'' hata kama ataboresha miundombinu. Hii ni akili yenye kukumbatia ukoloni mambo leo na kuhusudu utumwa. Eti waafrika tusijitawale kisa mzungu anatenda ''haki'', duh!

Nimalize tu kwa kusema Tanzania ni ya watanzania haitatawaliwa na mtumwa wa wakoloni wala aliyewatuma.

Embu fikiria kama watu aina ya Lissu wangekuwepo kipindi cha kudai uhuru halafu mzungu akawapa ''haki'' tungekuwa huru??

Sioni tofauti ya uongozi wa sasa na uongozi wa wakoloni.
1:Wakoloni walitumikisha watu kwa ujira mdogo, ndivyo serikali hii inafanya, haitaka kuwapandishia mishahara wafanyakazi.

2: Wakoloni walipora mali na kupeleka kwao, ndivyo kwa uongozi wa ccm na seriklali yake wanapora mali za watanzania na nakuzipeleka kujenga maeneo waliyotokea

3: Wakoloni ilikuwa ikipingana naokatika mambo yao, basi walikuwa wanakuuwa au kukufunga.

4: Wakoloni walikuwa na ubaguzi wa rangi, hapa kwetu viongozi wanaubaguzi wa kikabila, kikanda na kiitikadi za vyama.

Kuna mengi sana unaweza yaweka hapa.
 
Kwahiyo Gavana wa kiingereza angetoa "haki" angeachwa atawale?
Kwani ukoloni ulikomeshwa kwasababu gani? Haki sio kwasababu ya rangi au maendeleo. Nenda kasome vitabu vya Nyerere.
 
Jomba umepoteza muda wako bureee sijui utaulipiaje..kwanza unazungumzia demokrasia, hivi umeshafanya analysis kwenye vyama hivi vyooote na kuona demokrasia inavyokandamizwa wapi...tuwe wakweli tu..tusijifanye tunafumba macho..uliza kwanini vipngozi wengi wamehama vyama vyao wameenda kuunga mkono juhudi za Magufuli..whyyy..kwenye vyama vyao Kuna matatizo gani...jiulize..
Umeshauliza ruzuku zinatafunwaje kwenye vyama hivi , hiki ni kipimo kizuri Sana Cha uadilifu na demokrasia..tupe data jomba..chambua tuone..
Umesikia leo jinsi waombaji ubunge wanawake wanavyolalamika wameenguliwa bila sababu za msingi...umepimaje hili kwa vyama vyenu..je kuna demokrasia..mambo yapo chungumzima na najua mnajua Sana sema mna chuki tu na mtu kwa jinsi alivyowatumbua na kuwakosesha fursa zile za madili
Kwa hiyo Watanzania wote watakaomnyima kura JPM watakuwa wapiga dilii?
 
Kwenye ukweli usemwe,,maana ukweli utatuweka huru,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Hakuna watu wabaya kuliko mabeberu kama viongozi hawa wa Afrika,,,,Tusipende kuweka visingizio vya ubeberu katika udhaifu wa viongozi wetu,,,,, Hivi beberu ndiye kaharibu soko la zao la korosho,,hivi beberu ndiye kaharibu soko la mbaazi,,,,,hivi beberu ndiye kashindwa kufanya uwekezaji kwenye kilimo, kwa miaka 50 ,badala yake amesema mjenge Reli kwenda Mwanza ,, badala ya kuelekea Mbeya ,,Zambia na Congo ya,,Lubumbashi Kwenye mizigo mingi kuliko huko Congo ya kisangani?

Hivi huyo beberu ndiye anayefanya mpigine risasi kwa sababu tu ya hoja za Demokrasia na Haki za binadamu,, Ndugu yangu,,..Duniani nchi nyingi zimesonga mbele sana Kimaendeleo mbele ya huyo unayemwita beberu/Ubeberu,,,,,,South Korea, Malaysia, Singapore, Hong-kong, Taiwan, Thailand, China, India, Vietnam, UAE

Tatizo letu ni viongozi wanaojifanya Miungu watu kwa sababu tu ya kuwa Maraisi wa nchi,,,,,Hawataki demokrasia ya kweli, hawataki haki za binadamu zitamalaki, wabinafsi, wachoyo, wana roho mbaya,,,,,,,,na Makatili,,,,Nchi haiongozwi kwa majaribio,,,,
Hivi kuna shida gani kwa kiongozi kuruhusu uhuru wa kidemokrasia katika kuchagua viongozi ndani ya nchi yake,,na kama watu wanampenda na kuamini ayafanyayo si watampa nafasi tena,,,kwanini wanataka kung'ang'ania madarakani wakati tunawaona hakuna cha maana wanachoweza kufanya ili kulivusha taifa kwenye maendeleo makubwa ya kama Singapore?

Hivi kweli unataka kutuambia kwamba huo ubeberu ndiyo uliofanya Gadafi afiche zaidi ya Tillioni 80 Ulaya na Marekani
Hivi kweli ni huo ubeberu Uliofanya Gadafi akaifanya Libya kama nchi aliyorithi kutoka kwa wazazi wake, na kuwafanya wananchi wake kama wanyama/Watumwa? Au wewe kwa uelewa wako nchi ni mali ya nani
Tatizo la Congo ni wakongo wenyewe,,,,

Tunaweza kutoboa,, na kufanikisha taifa kuwa la maendeleo na haki,,,cha muhimu tusiabudu viongozi, kwa sababu viongozi hawawi malaika kwa kupata uongozi,,,ni binadamu wale wale kama sisi na wanamapungufu makubwa kama tuliyonayo, sisi(concept of check and balance comes in because of our human weakness) ,ndio maana watu lazima wawakosoe viongozi wao,,,Demokrasia ya kweli ikiruhusiwa itakuwa neema kwa taifa na kwa maendeleo ya nchi yetu,,,,,Ubeberu si mbaya ukifananisha na viongozi wa Afrika,,
Demokrasia ya kweli, haki za binadamu, uongozi wa sheria zilizo bora, uimara wa mihimili ya serikali katika kucheck na kubalance, Mfumo wa Utawala wa Westiminister (Parliamentary Government),

Vyama imara vya upinzani vyenye uwezo wa kucheck na kubalance ndio tunu pekee za kuipeleka Afrika dunia ya kwanza mahali bora katika miaka michache ijayo (Kwa hili Ghana inaonyesha njia chini ya Raisi Mwanasheria /Wakili Akufo Nana ADDO, Otherwise mtaendelea kumtafuta mchawi wa maendeleo ya Afrika,,,mtamsingizia Beberu, mtasingizia laana, mtasingizia resorce Curse (laana ya mali nyingi) Mtasingizia udikteta, Mtasingizia hali ya hewa, mtasingizia Word Bank na IMF,, mtasingizia Mchina,,,na viongozi wenu watakuwa hawawajibiki kwa kisingizio cha huyo huyo beberu,,, viongozi wenu watakuwa wanaiba mali zenu na kuzipeleka Ulaya,, mkiuliza kwanini hampigi hatua ,,watasingizia huyo huyo beberu,,,,,,kazi kwenu,,,,,,hata Mwalimu Nyerere kiongozi wenu aliposema ili tuendelee,,hakusema tupambane na beberu,,,, na kwamba kama yupo hatuwezi kuendelea. Tanzania siyo kisiwa,,itashirikiana na wenzake ili kupiga hatua za kimaendeleo,,,hata wakati wa utawala wa Kilwa empire,,ilishirikana na mataifa mengine na kupiga hatua kubwa,,,,Akili mukichwa nimemaliza....Mungu akusaidie,,akupe maarifa,,na aendelee kukufunua ubongo ili uijue kweli,,na kweli ikuweke huru.
MADINI MATUPU MKUU!! KUNA NCHI YA AFRIKA ILIYOKATAA MKOLONI AONDOKE NADHANI NI KISIWA MPAKA LEO KIKO CHINI YA HIMAYA YA UFARANSA KIKO MWENYE BAHARI YA HINDI SI HALAFU KUNA WAHAMIAJI WANAZAMIA KUTOKA COMORO KWENDA KUTAFUTA MAISHA BORA PALE
 
Kwahiyo kama Robert Amsterdam akikupa haki bora awe Rais wako?
Mleta mada rudi upya shuleni.
Huwezi kutenda haki na kuwapa uhuru watu halafu hapo hapo ukaendelea kuwa mkoloni.
Mkoloni maana yake ni mfumo wa kuwanyonya watu (kuwanyima haki zao) na kuwatumikisha watu (kuwanyima uhuru wao).
 
Ndugu zangu,

Nikiwa katikati ya shughuli zangu nimesikia kituko toka kwa Lissu na wafuasi wa CHADEMA eti..''pamoja na maendeleo aliyoleta mjerumani alikataliwa na waafrika sababu hakutenda haki'' kwa lugha rahisi ni kuwa mjerumani angetenda hiyo ''haki'' Lissu na wenzake wangefurahia tu angebaki kutawala.

Sijashangaa kwani hata CHADEMA wenyewe wanaamini ni bora leo Robert Amsterdam awe rais wa Tanzania sababu atawapa ''haki'' kuliko Rais Magufuli kwani hatawapa ''haki'' hata kama ataboresha miundombinu. Hii ni akili yenye kukumbatia ukoloni mambo leo na kuhusudu utumwa. Eti waafrika tusijitawale kisa mzungu anatenda ''haki'', duh!

Nimalize tu kwa kusema Tanzania ni ya watanzania haitatawaliwa na mtumwa wa wakoloni wala aliyewatuma.

Embu fikiria kama watu aina ya Lissu wangekuwepo kipindi cha kudai uhuru halafu mzungu akawapa ''haki'' tungekuwa huru??
Labda nikuulize mkoloni angetoa haki tungemkataa kwa kigezo gani??? Au wewe ukisikia neno haki unaelewaje kilaza wa lumumba???
 
Kama Miundombinu ingekuwa ya maana kuliko Uhuru basi tungewaacha watawale mpaka leo
 
Duh kwahiyo makaburu wangetoa "haki" wasauzi wangeridhika kutawaliwa na wazungu?

..kwa hiyo wewe tatizo lako ni RANGI, na siyo HAKI?

..HAKI maana yake ni pamoja na utawala wa walio wengi.

..kwa kweli CCM mmefilisika, wanaosema chama chenu kimekufa hawajakosea.
 
Duh yaani Gavana wa uingereza angetoa "haki" wewe burudani
..kwa hiyo wewe tatizo lako ni RANGI, na siyo HAKI?

..HAKI maana yake ni pamoja na utawala wa walio wengi.

..kwa kweli CCM mmefilisika, wanaosema chama chenu kimekufa hawajakosea.
 
Ndugu zangu,

Nikiwa katikati ya shughuli zangu nimesikia kituko toka kwa Lissu na wafuasi wa CHADEMA eti..''pamoja na maendeleo aliyoleta mjerumani alikataliwa na waafrika sababu hakutenda haki'' kwa lugha rahisi ni kuwa mjerumani angetenda hiyo ''haki'' Lissu na wenzake wangefurahia tu angebaki kutawala.

Sijashangaa kwani hata CHADEMA wenyewe wanaamini ni bora leo Robert Amsterdam awe rais wa Tanzania sababu atawapa ''haki'' kuliko Rais Magufuli kwani hatawapa ''haki'' hata kama ataboresha miundombinu. Hii ni akili yenye kukumbatia ukoloni mambo leo na kuhusudu utumwa. Eti waafrika tusijitawale kisa mzungu anatenda ''haki'', duh!

Nimalize tu kwa kusema Tanzania ni ya watanzania haitatawaliwa na mtumwa wa wakoloni wala aliyewatuma.

Embu fikiria kama watu aina ya Lissu wangekuwepo kipindi cha kudai uhuru halafu mzungu akawapa ''haki'' tungekuwa huru??
Yaani mtahangaika sana kutunga tafsiri zenu za lumumba na haitosaidia kitu days are numbered , subirini nguvu ya umma uone kazi .
 
Back
Top Bottom