Uchaguzi 2020 Kituko: Tundu Lissu na CHADEMA wanaamini mkoloni angetoa ''haki'' waafrika wasiongemkataa

Duh kwahiyo makaburu wangetoa "haki" wasauzi wangeridhika kutawaliwa na wazungu?
 

Sioni tofauti ya uongozi wa sasa na uongozi wa wakoloni.
1:Wakoloni walitumikisha watu kwa ujira mdogo, ndivyo serikali hii inafanya, haitaka kuwapandishia mishahara wafanyakazi.

2: Wakoloni walipora mali na kupeleka kwao, ndivyo kwa uongozi wa ccm na seriklali yake wanapora mali za watanzania na nakuzipeleka kujenga maeneo waliyotokea

3: Wakoloni ilikuwa ikipingana naokatika mambo yao, basi walikuwa wanakuuwa au kukufunga.

4: Wakoloni walikuwa na ubaguzi wa rangi, hapa kwetu viongozi wanaubaguzi wa kikabila, kikanda na kiitikadi za vyama.

Kuna mengi sana unaweza yaweka hapa.
 
Kwahiyo Gavana wa kiingereza angetoa "haki" angeachwa atawale?
Kwani ukoloni ulikomeshwa kwasababu gani? Haki sio kwasababu ya rangi au maendeleo. Nenda kasome vitabu vya Nyerere.
 
Kwa hiyo Watanzania wote watakaomnyima kura JPM watakuwa wapiga dilii?
 
MADINI MATUPU MKUU!! KUNA NCHI YA AFRIKA ILIYOKATAA MKOLONI AONDOKE NADHANI NI KISIWA MPAKA LEO KIKO CHINI YA HIMAYA YA UFARANSA KIKO MWENYE BAHARI YA HINDI SI HALAFU KUNA WAHAMIAJI WANAZAMIA KUTOKA COMORO KWENDA KUTAFUTA MAISHA BORA PALE
 
Kwahiyo kama Robert Amsterdam akikupa haki bora awe Rais wako?
Mleta mada rudi upya shuleni.
Huwezi kutenda haki na kuwapa uhuru watu halafu hapo hapo ukaendelea kuwa mkoloni.
Mkoloni maana yake ni mfumo wa kuwanyonya watu (kuwanyima haki zao) na kuwatumikisha watu (kuwanyima uhuru wao).
 
Labda nikuulize mkoloni angetoa haki tungemkataa kwa kigezo gani??? Au wewe ukisikia neno haki unaelewaje kilaza wa lumumba???
 
Kama Miundombinu ingekuwa ya maana kuliko Uhuru basi tungewaacha watawale mpaka leo
 
Duh kwahiyo makaburu wangetoa "haki" wasauzi wangeridhika kutawaliwa na wazungu?

..kwa hiyo wewe tatizo lako ni RANGI, na siyo HAKI?

..HAKI maana yake ni pamoja na utawala wa walio wengi.

..kwa kweli CCM mmefilisika, wanaosema chama chenu kimekufa hawajakosea.
 
Duh yaani Gavana wa uingereza angetoa "haki" wewe burudani
..kwa hiyo wewe tatizo lako ni RANGI, na siyo HAKI?

..HAKI maana yake ni pamoja na utawala wa walio wengi.

..kwa kweli CCM mmefilisika, wanaosema chama chenu kimekufa hawajakosea.
 
Yaani mtahangaika sana kutunga tafsiri zenu za lumumba na haitosaidia kitu days are numbered , subirini nguvu ya umma uone kazi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…