Ha ha ha ha ha poleni sn kwa makasiriko. Hivi hamjui km uchumi wa Tz ni wa SOKO HURIA (zingatia maneno SOKO HURIA).
Mnalalamika juu ya biashara, mbona Tz imekubali kuwafundisha watu wake lugha ya KICHINA kuanzia msingi (kwa shule za kimataifa) hadi vyuo vikuu wakati hata lugha yao ya KWAHILI tu hawajui. Hivi kati ya elimu na biashara kipi kina madhara hasi kwa jamii.
Je mnadhani kwa janja janja ya wafanya biashasha wa Tz ya kuchakachua thamani ya bidhaa, kupandisha bei kiholela, kutopenda kulipa kodi stahiki, kuweka migomo kila wakati, hilo soko litakuwepo. Hapa shida ni tabia za Watanzania wenyewe ndo zinapelekea serikali kuwa na maamuzi magumu. Mtanzania anaweza kukuuzia kitu cha elf 20 kwa elfu 50 maana hutanguliza tamaa mbele kuliko kutoa huduma. Mfano, dunia kwa sasa ni Kijiji sababu ya kukua wa teknolojia, bidhaa unaagiza tu kwenye basi inakufikia popote ulipo tena free delivery, sasa kwa Wabongo huu umekuwa ugonjwa, ukiwasiliana na mfanya biashara akutumie bidhaa mikoani kuna kuwa na uwezekano mkubwa wa kulizwa hasa akishapokea pesa. Wakati mwingine atakutumia bidhaa ambayo haikuwa kwenye matangazo yake.
Watanzania wanataka maisha rahisi bila kujali nani anafanya biashara. Mataifa km Uganda baada ya kuruhusu Wachina kufungua maduka yao KAMPALA wananchi sasa hivi ni kicheko ingawa kwa wafanya biashara wenyeji ni kilio. Huwezi kiniuzia bidhaa bei kubwa kwa sababu tu ya UZALENDO, wakati wapo wenye uwepo wa kuniuzia bidhaa hiyohiyo kwa bei nafuu. Haya ni maisha siyo mchezo wa kuigiza, kila mtu atambe pande zake.
Hizi fikira za kukataa ngozi nyeupe ndo zimeyanfa nchi nyingi za Africa ikiwemo Tz kuugulia umaskini wa kutupwa. Nchi zote zilizofukuza wakoloni kwa kigezo cha KUJITAWALA na UZALENDO wa kuthamini cha kwetu pekee leo ndo wanaishi chini ya dola moja kwa siku Tz ikiwa kinara ikifuatiwa na Zimbabwe nk. Lakini nchi zilizoona umuhimu wao na kuwaacha kuendelea kuishi na kuwekeza japo kwa mashariti leo pato la Taifa na mtu mmoja mmoja liko juu. Mfano South Africa.
Km kariskoo pekee wameshindwa kuindesha kwa weredi, wataweza Ubungo. Yani pale Kariskoo wafanya biashara wamejaza MAWINGA kila sehemu ya maduka yao, na hao ndo wanawaumiza Watanzania kwa kuwapandishia bei huku wenye maduka wakikenua meno. Kariskoo haina tofauti na stand za mabasi kulikojaa wapiga debe, na hawa wamekuwa wakiwaumiza abiria kwa kuwapandishia bei. Sasa kwenye nchi ya watu wastaarabu huu ujinga hapo.
Tukubali tukatae kumuamini Mtanzania ktk biashara ni sawa na kununua mbuzi kwenye gunia. Leo wanatafuta huruma kwa serikali, lakini kesho wakikabidhiwa soko tu WANANCHI hawa hawa watarudi kulalamika.
Saidi: BANDOKITITA