Kituo cha kuuliza maswali ya kifala, na wewe uliza lako

Kituo cha kuuliza maswali ya kifala, na wewe uliza lako

Swali; Je hivi ni kweli mmeona hii coment yangu?
Jibu; Anzisha uzi wako kisha hesabu like utakazopata, jitahidi pia uweke kitufe chako chenye selfie camera ukifunge kwenye kila post/comment na kiwe automatic kupiga selfie kwa yule atakayetazama kila post yako!!
 
KITUO CHA KUULIZA MASWALI YA KIFALA 1- NA WEWE ULIZA LAKO


i. Shilingi 1000/-ni bei gani?- Kisa wa Mbeya

JIBU:Ndugu yangu swali lako zuri sana, uchumi kwa kuwa umepanda na wewe chukua ngazi uufwatie hukohuko maana ukiwa juu alfu ni kama shilingi 900/- lakini ukiwa chini bei ya alfu ni shilingi 600/-
ii. Niko chuoni nasomea unesi, je unadhani nikimaliza shule nitaweza kufanya kazi gani?- Nene wa Kondoa

JIBU: Ukimaliza utakuwa polisi
iii. Je Iringa kubwa kuliko Tanzania?- Magnus wa mafinga

JIBU: Ni wazi wewe ni Mnyalu, ndio Iringa kubwa kuliko Marekani. Angalia kwenye ramani ya Australia utakuta Iringa kaskazini inapakana na Mexico
iv. Je ni kweli binadamu wana miguu miwili?- El Murieti wa Arusha

JIBU: Huo ni uwongo unaoenezwa na wapinzani, tafadhali usidanganyike. Miguu ya kawaida ina binadamu wawili
v. Nimejiangalia kwenye kioo sikujiona, niko wapi?- Chausiku wa Kisarawe

JIBU: Kioo hicho kitakuwa kibovu, si unajua wachina kila kitu wanaleta feki. Kifupi saa hizi uko ahera
vi. Diamond Platnumz ameacha Ubunge wa Chunya?- Fusu wa Kinondoni

JIBU: Diamond ni Mbunge wa kudumu wa bunge la Senegal, aliacha Ubunge wa Chunya kutokana na tatizo la kupatwa kwa jua
vii. Ukichanganya instagram na whatsapp unapata nini?- Stela wa Ostabei

JIBU: Unapata Google, jamani maswali mengi ni ya kitoto mno muwe mnajijibu wenyewe
viii. Nilikuwa macho lakini nikaota nahamia Dodoma, maana yake nini?- Mwanasiasa wa Kagera

JIBU: Maana yake utafungwa kwa wizi wa michango ya serikali za mtaa
x. Naweza kupiga mswaki na brash ya viatu?- Vanga- Geita

JIBU: Bahati mbaya hukutaja kabila lako, lakini kwa uhakika kabila lenu mtafukuzwa hapa nchini muda si mrefu.
Daa unafaa kuajiliwa na Nyambali Nyangwine kuandaa vitabu vya maswali na majibu
 
Naitwa CHUMA ULETE kutoka Mafinga Iringa

Nasikia Mfalme wa Tanzania ndg Pombe Lissu anahamia nyumbani kwake Kenya,swali ni je bado atakuwa na madaraka ya kifalme kwa nchi yake ya chato?
 
Naitwa CHUMA ULETE kutoka Mafinga Iringa

Nasikia Mfalme wa Tanzania ndg Pombe Lissu anahamia nyumbani kwake Kenya,swali ni je bado atakuwa na madaraka ya kifalme kwa nchi yake ya chato?
Bila shaka ; Kumbuka hata yeye alivyomwalika rasi wa morko, alimuomba amjengee bahar ya mkra domya, na hata hivyo huko ndiko atahamia ili akajfunze kuogelea mpra, lakini na wewe hivi hili swal gani kwani hili ni swali la kijinga?
Ungeegelezea kwenye orodha ya kuzidisha namba!!
 
Back
Top Bottom