Kituo cha kuuliza maswali ya kifala, na wewe uliza lako

Kituo cha kuuliza maswali ya kifala, na wewe uliza lako

Magari Aina Zote

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
3,150
Reaction score
528
KITUO CHA KUULIZA MASWALI YA KIFALA 1- NA WEWE ULIZA LAKO


i. Shilingi 1000/-ni bei gani?- Kisa wa Mbeya

JIBU:Ndugu yangu swali lako zuri sana, uchumi kwa kuwa umepanda na wewe chukua ngazi uufwatie hukohuko maana ukiwa juu alfu ni kama shilingi 900/- lakini ukiwa chini bei ya alfu ni shilingi 600/-
ii. Niko chuoni nasomea unesi, je unadhani nikimaliza shule nitaweza kufanya kazi gani?- Nene wa Kondoa

JIBU: Ukimaliza utakuwa polisi
iii. Je Iringa kubwa kuliko Tanzania?- Magnus wa mafinga

JIBU: Ni wazi wewe ni Mnyalu, ndio Iringa kubwa kuliko Marekani. Angalia kwenye ramani ya Australia utakuta Iringa kaskazini inapakana na Mexico
iv. Je ni kweli binadamu wana miguu miwili?- El Murieti wa Arusha

JIBU: Huo ni uwongo unaoenezwa na wapinzani, tafadhali usidanganyike. Miguu ya kawaida ina binadamu wawili
v. Nimejiangalia kwenye kioo sikujiona, niko wapi?- Chausiku wa Kisarawe

JIBU: Kioo hicho kitakuwa kibovu, si unajua wachina kila kitu wanaleta feki. Kifupi saa hizi uko ahera
vi. Diamond Platnumz ameacha Ubunge wa Chunya?- Fusu wa Kinondoni

JIBU: Diamond ni Mbunge wa kudumu wa bunge la Senegal, aliacha Ubunge wa Chunya kutokana na tatizo la kupatwa kwa jua
vii. Ukichanganya instagram na whatsapp unapata nini?- Stela wa Ostabei

JIBU: Unapata Google, jamani maswali mengi ni ya kitoto mno muwe mnajijibu wenyewe
viii. Nilikuwa macho lakini nikaota nahamia Dodoma, maana yake nini?- Mwanasiasa wa Kagera

JIBU: Maana yake utafungwa kwa wizi wa michango ya serikali za mtaa
x. Naweza kupiga mswaki na brash ya viatu?- Vanga- Geita

JIBU: Bahati mbaya hukutaja kabila lako, lakini kwa uhakika kabila lenu mtafukuzwa hapa nchini muda si mrefu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
hahahahaaaa [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] walahi aliyetunga hii ana kipaji cha uchekeshaji afanye mpango akitumie vzur
 
mkuu Ndeko umetisha sana asee,,jina lako lenyew ni kituko,,km una fb page iweke niku follow mkuu
 
Wew jamaa ni hatari kwa mbavu za watu [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Eti serikali ni nn
Serikali Ni aina ya kemikali Kali mno,.. ambayo ukiichanganya na ukweli unapata uchochezi uliofanya viti kung'olewa taifa hatimaye Man u kufungwa manfongo ila sio na shemeji,

dady what is cockroach?
kokurochi ni aina ya chakula kwan mwanangu hukijui
?
hapana
ni kukurosti maana yake sawa ehh",..¿!
aiya..

Mh! tafuta fani nyingine mkuu!
 
Hivi kwa nini scorpion aliachiwa mahakamani?
ustadhijuma wa jamiiforum
 
Ke : helo , hujalala saa sita USIKU yote hii , unafanya nini kwani mpk sa hizi

Me: nipo nje hapa naotaota jua
 
Back
Top Bottom