Kituo cha Mabasi cha Magufuli kimegeuka soko kwa sababu ya usimamizi mbaya

Kituo cha Mabasi cha Magufuli kimegeuka soko kwa sababu ya usimamizi mbaya

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Hakika inashangaza na Kusikitisha kabisa. SERIKALI inashindwa kuweka na kusimamia Utaratibu Mzuri wa Uendeshaji wa Kituo cha Mabasi cha Magufuli kwa kumwaachia Wafanyabiashara kutandaza na kupanga bidhaa zao kwenye Corridor na sehemu za kupumzika Abiria.

Hivi kusimamia hilo mpaka aje Mzungu? Mbona Viongozi wetu wazembe sana kwenye mambo ya Msingi?

Tunawaomba Wahusika wawaondoe wafanya Biashara wanaopanga na kutandaza bidhaa zao kinyume na Utaratibu.
 
Ukiingia ndani ndiyo balaa zaidi kunauzwa pombe za kila Aina, mateja na vibaka wote wa Ubungo wapo ndani kama kawaida.

Maamuzi ya kisiasa eti waacheni wachinga wafanye biashara ndiyo hiyo imetufikisha hapo. Hiyo terminal ni maskani ya wauza bangi na vibaka.
 
Tatizo la Marehemu Jiwe alitaka kutengeza 'cult' (kama kadini kake mwenyewe chenye wafuasi wanaomuona masiha). Na ili kulitimiza hili akatarget wale wa kipato cha chini sana na kujitwika utetezi hewa.

Kutimiza dhamira yake alikwenda kinyume na mfumo wa kistaarabu ili tu aonekane anajali sana, alifanikiwa kupata wa kumuabudu lakini athari yake inakera wengi zaidi.

Leo hii kupita kariakoo ni tabu maana kumejaa wamachinga kila sehemu, ukija ilala boma barabara imekuwa soko la nyanya na vitunguu.

Na hiyo stendi ya mabilioni ishakuwa kama tandika tayari, yote sababu ya kiumbe mmoja tu aliyetaka kuwa mungu na leo hayupo tena.
 
Tatizo la Marehemu Jiwe alitangaza kutengeza 'cult', yani awe kama mungu mtu. Na ili kulitimiza hili akatarget wale wa kipato cha chini sana na kijitwika utetezi hewa. Kutimiza dhamira yake alikwenda kinyume na mfumo wa kistaarabu ili tu aonekane anajali sana, alifnikiwa kupata wa kumuabudu lakini athari yake inakera wengi zaidi.
Leo hii kupita kariakoo ni tabu maana kumejaa wamachinga kila sehemu, ukija ilala boma barabara imekuwa soko la nyanya na vitunguu. Na hiyo stendi ya mabilioni ishakuwa kama tandika tayari, yote sababu ya kiumbe mmoja tu aliyetaka kuwa mungu na leo hayupo tena.

Umeandika sanaaaaaaa kwanini hawa wamachinga wanakuumiza hivi?

Waache wenzio wapate rizki sababu nao wana mahitaji kama yako japo hawana kazi sawa na yako
 
Hakuna haja ya kuwagusa kama ina maana ya kuwaondoa
Ila ipo haja ya kutengeneza mfumo mzuri wa wao kuwepo kwa manufaa ya wote
Waende wakajifunze hata nchi za jirani
Basi,Waone wanavyoweka mfumo wa wafanyabiashara wadogo wadogo
Waende angalau Lusaka pale kwenye bus terminal yao wakajifunze...
Huwezi kujenga standi ya garama alafu ukaruhusu mambo ya ovyo ovyo, utaratibu zero

Siku zote nasema exposure, exposure, exposure kitu muhimu sana

Ova
 
Umeandika sanaaaaaaa kwanini hawa wamachinga wanakuumiza hivi?

Waache wenzio wapate rizki sababu nao wana mahitaji kama yako japo hawana kazi sawa na yako
Hakuna anaepinga kutafuta kwao rizki hivyo usipotoshe maudhui. Tatizo linakuja wanaitafuataje hiyo rizki. Ikiwa kila mmoja anatumia kigezo cha kutafuta rizki basi hata vibaka hawana makosa.
Kutafuta kwao rizki kusiwe kero kwa wengine, kama kuna sehemu maalum wanatengewa kufanya biashara na hawazitaki wanaishia kukimbilia pembezoni mwa barabara sasa hapo huoni kuwa wanakuwa wabinafsi kwa kuangalia matakwa yao tu kutokuzingatia mahitaji ya wengine.
Na siku nyingine ukiona mtu kaandika sana potezea mama, usisome kuepuka kukereka.
 
Back
Top Bottom