Kituo cha Polisi Wilaya ya Butiama chajengwa kwa Tsh. Milioni 802, kukamilika Desemba 2023

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini ameagiza kukamilika kwa wakati Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja B cha Wilaya ya Butiama Mkoani Mara, ifikapo mwezi Disemba 2023 kama ilivyoelekezwa.

Maagizo hayo ameyatoa leo Novemba 18, 2023 wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua uendelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo hicho kilichopo katika eneo la Mtuzu Kata ya Butiama Wilayani Butiama.
View attachment 2818004
Muonekano wa Jengo la Kituo cha Polisi Daraja B kinachojengwa katika eneo la Mtuzu Kata ya Butiama Wilayani Butiama Mkoani Mara Novemba 18, 2023.

View attachment 2818005
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb), akikagua uendelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja B kinachojengwa katika eneo la Mtuzu Kata ya Butiama Wilayani Butiama Mkoani Mara, leo Novemba 18, 2023.

"Nimefurahishwa na kasi ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Butiama, mradi huu unatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wetu mpendwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, bila kuchoka mama huyu amemwaga fedha za kutosha hivyo basi nimtake mkandarasi kukamilisha mradi haraka bila vikwazo kwani Wananchi wana kiu kubwa ya kupata huduma karibu," alisema

Katika taarifa yake Meneja wa Mradi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Butiama wa Kikosi cha Polisi Ujenzi, Mkandarasi SP Masiva Mfinanga alieeleza kuwa, mradi huo una thamani ya Shilingi 802,000,000 (Tsh. Milioni 802) ambapo ujenzi ulianza rasmi Mei 6, 2023 na unategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Disemba 2023.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini yupo Mkoani Mara kwa ziara yake ya kikazi ambapo atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayoendelea katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara hiyo.
Jamani...jamani...Tanzania nchi yangu...hili jengo ni la zaidi ya milioni 800? Ama kweli nchi yangu Tanzania...
 
Karibuni!
 
Attachments

  • FE2447C2-F498-4176-8116-F20AD464141B.jpeg
    FE2447C2-F498-4176-8116-F20AD464141B.jpeg
    120.6 KB · Views: 4
Mkuu hivi kituo cha polisi panakwepo na miundombinu zipi? Je umejiuliza kama fanitures nazo ni sehemu ya mkataba?
Labda kama wananunua bunduki na vifaru
800m ni pesa ndefu mkuu
Watanzania sio wapumbafu
Hilo jengo halizidi milion 40
 
Tusitafute mjadala bado kuna nyumba za askari hazijawekwa pichani.

Na majengo ya serikali ni ya gharama kwanza Mengi

tofali wana LAZA
Madirisha Flat Bar au Nondo zinazotumika sio za kukata na Mkasi kama za nyumba tunazoishi.
Bati ndio usiseme gauge inayotumika
Finishing zake ndio kabisaaa

Ukisikia ujenzi wa majengo ya serikali usije ukafananisha na ujenzi wako wewe hata siku moja.
 
Hata kama umeshiriki kupiga usitete wizi, milioni 802 haziwezi kufika kwa hicho kibanda.
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini ameagiza kukamilika kwa wakati Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja B cha Wilaya ya Butiama Mkoani Mara, ifikapo mwezi Disemba 2023 kama ilivyoelekezwa.

Maagizo hayo ameyatoa leo Novemba 18, 2023 wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua uendelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo hicho kilichopo katika eneo la Mtuzu Kata ya Butiama Wilayani Butiama.
View attachment 2818004
Muonekano wa Jengo la Kituo cha Polisi Daraja B kinachojengwa katika eneo la Mtuzu Kata ya Butiama Wilayani Butiama Mkoani Mara Novemba 18, 2023.

View attachment 2818005
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb), akikagua uendelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja B kinachojengwa katika eneo la Mtuzu Kata ya Butiama Wilayani Butiama Mkoani Mara, leo Novemba 18, 2023.

"Nimefurahishwa na kasi ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Butiama, mradi huu unatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wetu mpendwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, bila kuchoka mama huyu amemwaga fedha za kutosha hivyo basi nimtake mkandarasi kukamilisha mradi haraka bila vikwazo kwani Wananchi wana kiu kubwa ya kupata huduma karibu," alisema

Katika taarifa yake Meneja wa Mradi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Butiama wa Kikosi cha Polisi Ujenzi, Mkandarasi SP Masiva Mfinanga alieeleza kuwa, mradi huo una thamani ya Shilingi 802,000,000 (Tsh. Milioni 802) ambapo ujenzi ulianza rasmi Mei 6, 2023 na unategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Disemba 2023.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini yupo Mkoani Mara kwa ziara yake ya kikazi ambapo atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayoendelea katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara hiyo.
Mnapiga mpaka chumbani kwa Mtakatifu!
 
Kweli jengo la police linajengwa kama nyumba ya kuishi
Hivi wakandarasi hawaendi na wakati?
Hata ku copy majengo ya kisasa kwenye mataifa mengine wameshindwa
Jengo fupi kwa hela hizo wamepiga nusu
 
Halafu waziri ana angalia hilo banda na kufurahia kugumia pesa zote hizo.
Hii Ccm ina laana ya walio kufa
 
Tusitafute mjadala bado kuna nyumba za askari hazijawekwa pichani.

Na majengo ya serikali ni ya gharama kwanza Mengi

tofali wana LAZA
Madirisha Flat Bar au Nondo zinazotumika sio za kukata na Mkasi kama za nyumba tunazoishi.
Bati ndio usiseme gauge inayotumika
Finishing zake ndio kabisaaa

Ukisikia ujenzi wa majengo ya serikali usije ukafananisha na ujenzi wako wewe hata siku moja.

Tuonesheni hizo nyumba basi. Inawezekana upigaji ukawa mkunwa zaidi.
 
Hapo ndiyo mtajua kwa nini serikali imewang'ang'ania walimu kusimamia ujenzi wa madarasa kwa bei ndogo na madarasa yanakamilika!
 
Back
Top Bottom