Kituo cha Polisi Wilaya ya Tunduru kinajaa wananchi sana asubuhi

Kituo cha Polisi Wilaya ya Tunduru kinajaa wananchi sana asubuhi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Sijaelewa ni mentality ya raia tu kupenda kupelekana polisi kwa kesi hata ndogondogo au ni mazingira polisi wametengeneza ili kupiga hela kwa sababu haiwezekani asubuhi tu kituo kinajaa wateja zaidi ya 100 na ni kila siku mpaka inafikia hatua wanaitwa kwa foleni.

Mambo haya hayapo katika vituo vingine iwe ni masasi au Dodoma au Mtwara au Songea au Singida au Arusha au Dar ni hapo tu Tunduru naomba pachunguzwe kuna nini?
 
Sasa hao polisi wa Tunduru bado hawajaona ni hatari sana kukaribisha idadi kubwa hiyo ya watu kwenye eneo lao. Polisi wengine sijui walilazimishwa kutumikia hivi vyombo vya ulinzi ama walipenda wenyewe.

Mimi siyo askari ila nisingeruhusu kituoni kwangu kila siku kuwe na idadi kubwa ya watu. Kwanza usalama wa hicho kituo ni mdogo na huo mkusanyiko wa kila siku UKOME.
 
Polisi wa Tunduru wanataka rushwa kupita maelezo. Wanakopa vitu madukani na hawalipi ukimdai atakupa kesi.
 
Lazima wamembinu binu wangine waige uenda wanatatua migogoro midogomidogo kwa uwazi zaidi iyo nayo ni kazi zao
 
Hata huku kuna hospital zinajaza sana watu nje sijui wote ni wagonjwa au yametengenezwa mazingira ya rushwa
 
Kuna watu wanapenda mikesi
Kitu kidogo kakimbilia polisi
Au mahakamani

Ova
 
Sijaelewa ni mentality ya raia tu kupenda kupelekana polisi kwa kesi hata ndogondogo au ni mazingira polisi wametengeneza ili kupiga hela kwa sababu haiwezekani asubuhi tu kituo kinajaa wateja zaidi ya 100 na ni kila siku mpaka inafikia hatua wanaitwa kwa foleni.

Mambo haya hayapo katika vituo vingine iwe ni masasi au Dodoma au Mtwara au Songea au Singida au Arusha au Dar ni hapo tu Tunduru naomba pachunguzwe kuna nini?
Sure mkuu now npo uku hii Hali naiona sana tena wengi wamejaa kando ya barabara apa nje soko la madini wamejaa barabarani kama wanamuaga rais..
 
Back
Top Bottom