The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Gilead John Teri, amewahimiza wanafunzi wa vyuo vikuu kuwa na uelewa wa msingi kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji ili waweze kujiajiri mapema hata kabla ya kuingia rasmi kwenye soko la ajira.
Amesisitiza hayo Februari 28, 2025 katika semina ya uwekezaji kwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya TIC na Save Youth's Dreams Foundation (SYDF),
Bw. Teri amesema wangependa mwanafunzi anayetoka chuo kikuu awe na uelewa wa msingi wa biashara, ikiwa ni pamoja na kujua jinsi ya kufungua kampuni.
"Mwanafunzi wa IT, kwa mfano, anaweza kuanza kutoa huduma zake akiwa bado shuleni kabla ya kuhitimu."
Pia amewaeleza kuwa kuna fursa nyingi kwa vijana kuwekeza hata kwa mtaji mdogo, ikiwemo ununuzi wa hisa na uwekezaji katika sekta mbalimbali. Amesisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kuzitumia fursa hizi badala ya kuwaachia wawekezaji wa kigeni.
"Kuna takwimu ambayo ningependa kuona ikiongezeka. wawekezaji wa ndani wa Tanzania bado ni wachache. Wageni wanakuja na kuwekeza kwenye fursa ambazo sisi wenyewe Watanzania tungeweza kuzichangamkia," amesema Bw. Teri.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, amesema kuwa semina hiyo ni sehemu ya mikakati ya UDOM katika kuwaandaa wanafunzi kwa changamoto za kiuchumi na kuwaelimisha juu ya mbinu za uwekezaji.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki semina hiyo walieleza kuwa wamepata mwanga mpya kuhusu umuhimu wa kuweka akiba na kuwekeza mapema kwa ajili ya mustakabali wao wa kifedha.
Hata hivyo, Semina kama hizi zinaendelea kuwa nyenzo muhimu kwa vijana katika kuwaandaa kuwa sehemu ya maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania.