KERO Kituo kidogo cha magari Simike - jijini Mbeya kinahatarisha usalama wa abiria

KERO Kituo kidogo cha magari Simike - jijini Mbeya kinahatarisha usalama wa abiria

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
📖Mhadhara (71)✍️
Mbeya ni mkoa ambao unakabiriwa na matukio ya ajali za mara kwa mara. Maeneo ambayo ajali hutokea sana ni;
1. Mlima nyoka,
2. Mteremko wa Simike (Nzovwe), na
3. Mlima wa Mbalizi.

Licha ya ajali nyingi kutokea katika maeneo hayo hasa Mteremko wa Simike (Nzovwe), lakini mabus madogo (Coaster) yanayobeba abiria wa kutoka Mbeya mjini kwenda Tunduma na Ileje yanasimama kwa muda mrefu sana kwenye kituo kidogo (parking) cha Simike huku yakisubiri abiria. Kituo kidogo cha Simike kimekuwa ni stendi kuu ya mabus madogo (coaster) hali inayohatarisha usalama wa abiria.

Ifahamike kuwa eneo lile (Simike) ni eneo la kushusha na kuchukua abiria kisha kuondoka, na wala si eneo la kusubiria abiria kwa muda mrefu, lakini Coaster zinasimama Simike zaidi ya dakika 15. Wapiga debe wa eneo lile (Simike) wamechapisha mpaka T-shirts zao zisomekazo "Maafisa usafirishaji" kudhihirisha kuwa pale ni stendi ya mabus kama stendi nyingine. Wakati mwingine unakuta coaster imesimama vibaya yaani eneo la nyuma lote lipo barabarani mpaka malori yanapiga honi ya kumtaka dereva wa coaster asimamishe vizuri, ni hatari sana.

Mbali na kero hiyo ya kuhatarisha usalama wa abiria, kero nyingine ni wapiga debe wa eneo lile (Simike) ni wababe sana kwa abiria. Naomba mamlaka husika zote zitazame kero hizi kwa jicho la kumi ili kuepusha ajali za mara kwa mara zinazotokea katika Mkoa wa Mbeya.
images.jpeg

RIGHT MARKER,
DAR ES SALAAM.
👁️Utalii wa JIJINI MBEYA.
 
Tatizo sio coster kusimama tatizo ni barabara ipanuliwe na malori mabovu yatolewe barabarani, mara nyingi ajali Simike inatokana na malori kufail break na kuparamia watu, bajaji na magari mengine hivyo ni vyema hao wachina wanayopanua hiyo barabara wakawekeza nguvu kwenye hicho kipande kwanza.
 
Dah!! Simike, Meta, Mabatini, Mbembela, Nzovwe, Kalobe, Iyunga,.....!! Kitambo sana.
 
Suluhisho la kudumu eneo hilo ni barabara ya mchepuko, vinginevyo tutaendelea kushuhudia watanzania wenzetu wakipoteza maisha kwa mamia katika eneo hilo ambalo haipiti miezi mitatu bila kuua kwa makumi.
 
Back
Top Bottom