Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandisi Joseph Nyamhanga, amewataka viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani cha Mbezi Luis, kuanza kutumika ifikapo Desemba 20, 2020.
Ametoa maagizo hayo leo Desemba 7, 2020, alipotembelea mradi huo kuangalia maendeleo yake ambao kwa sasa umefikia asilimia 92-95, akieleza kuwa kazi ndogondogo zilizosalia zimalizike katika kipindi hiki kifupi ili kituo hicho kianze kutumika.
“Kituo kikuu cha mabasi kipya cha Mbezi Luis kiwe tayari kimeanza kufanya kazi, hatua ambayo itapunguza msongamano katika kituo cha Ubungo hususani katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka,”amesema.
Akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya mradi huo, meneja mradi huo, Dkt. Godwin Maro, amesema ujenzi umefikia katika hatua za mwisho na kinaweza kuanza kutumika muda wowote ingawa changamoto ni barabara inayotakiwa kuingiza magari kituoni hapo ambayo kwa mujibu wa meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Ngassa Julius, itakamilika kabla ya Desemba 20 kama ilivyoagizwa ili kituo kianze kutumika rasmi.