Kitwanga atoa ufafanuzi wa suala la Lugumi na uhusiano wake kuhusu kutumbuliwa kwake

Kitwanga atoa ufafanuzi wa suala la Lugumi na uhusiano wake kuhusu kutumbuliwa kwake

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,903
CHARLES Kitwanga, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema kuwa, hajutii ‘kutumbuliwa’ na Rais John Magufuli, anaandika Moses Mseti.
Ametoa kauli hiyo wikiendi iliyopita jimboni kwake Misungwi jijini Mwanza ikiwa ni takribani mwezi mmoja baada ya kung’olewa kwenye nafasi hiyo.

Kitwanga alifukuzwa kazi kwa madai ya kuingia bungeni na kujibu masali ya wizara yake akiwa amelewa.
Amesema kuwa, anamshukuru Mungu kwa kuondolewa katika nafasi hiyo na kwamba, huenda kama angeendelea kuwepo, angepata matatizo makubwa zaidi.

Na kwamba, hatua ya Rais Magufuli kumwondoa katika nafasi hiyo kitamsaidia kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kwa ukaribu zaidi tofauti na alivyokuwa kwenye nafasi ya uwaziri.

“Namshukuru sana Mungu kuondolewa katika nafasi hii (Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi) labda ameniepusha na mambo mengi ambayo yangeweza kunikumba na hii itanisaidia kuwatumikia wanamisungwi kwa ukaribu,” amesema Kitwanga.

Kitwanga baada ya kung’olewa katika nafasi hiyo, siku kadhaa baadaye alitimkia nchini Israel ambako inadaiwa kwenda kupumzika ambapo alirejea nchini hivi karibuni. Baada ya kurejea nchini, Kitwanga moja kwa moja alikabidhiana Ofisi na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa Mwigulu Nchemba aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo. Nchemba alikuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Kabla ya kutimuliwa Kitwanga alikuwa akiandamwa na kashfa ya Kampuni ya Lugumi iliyopewa zabuni ya kufunga mashine za kutambua alama za vidole katika vituo vyote vya Jeshi la Polisi nchini.

Jeshi hilo liliingia mkataba na Kampuni ya Lugumi Enterprises ili kufunga mashine 108 nchi nzima lakini kampuni hiyo ilifunga mashine 14 tu.

 
Nasikia kuna tetesi kuwa ana mpango wa kuhama chama na kutimukia chama kikuu cha upinzani
 
Ule ulikuwa ni mkakati maalumu hawawezi kujuta umeona swala Lugumi limeishia hewani wamepewa miezi mitatu wahakikishe vifaa vimefungwa na vinafanya kazi basi
 
Habari za kusikia changanya na za kwako ule ulikuwa na mkakati maalumu hawawezi kuhama huko CCM
Nasikia kuna tetesi kuwa ana mpango wa kuhama chama na kutimukia chama kikuu cha upinzani
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hiyo kweliiiiiiiii na ndo maana alienda kula chachandu israel
 
Ccm wasituletee porojo kwenye mahakama ya mafisadi.. Tunataka wa kina Kitwanga tuwaone kizimbani
 
Habari za kusikia changanya na za kwako ule ulikuwa na mkakati maalumu hawawezi kuhama huko CCM

Aaaah jamani, mbona hata wale walio balehe wakiwa katika chama nao wamehama, anyway sishangai hata iliposemwa kuwa fulani anataka kuhamia watu walibisha hivi na post zao zipo mpaka leo!
 
Inaeleweka kuwa sio lazima kusema yaliyokuumiza moyoni kwa kuanika maumivu uliyopata. Vizuri kuwa +ve na kumshukuru Mungu kwanza huku ukiamini kuwa umejifunza.

Haya piga kazi wakuchague tena ukitaka kugombea 2020.
 
Ccm wasituletee porojo kwenye mahakama ya mafisadi.. Tunataka wa kina Kitwanga tuwaone kizimbani

Usiseme akina Kitwanga tu, sema unataka kuwaona mafisadi wote mahakamani. Hapo utakuwa umejitendea haki na kulitendea haki taifa
 
Tutasikia mengi sana mwaka huu......23 vs 24
 
Ninapenda kufahamu, je, Kitwanga ni mojawapo ya wabunge wa CCM waliondikiwa barua ya utoro bungeni...?
 
Porojo za mahakama ya ufisadi zinazidi kudhihirika.
Uzushi na ukurupukaji usio na kifani kwa serikali hii ya 5
 
Ule ulikuwa ni mkakati maalumu hawawezi kujuta umeona swala Lugumi limeishia hewani wamepewa miezi mitatu wahakikishe vifaa vimefungwa na vinafanya kazi basi
Mtango mwitu huwezi kuzaa maembe
 
Back
Top Bottom