Kitwanga atoa ufafanuzi wa suala la Lugumi na uhusiano wake kuhusu kutumbuliwa kwake

CHARLES Kitwanga, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema kuwa, hajutii ‘kutumbuliwa’ na Rais John Magufuli, anaandika Moses Mseti.

Ametoa kauli hiyo wikiendi iliyopita jimboni kwake Misungwi jijini Mwanza ikiwa ni takribani mwezi mmoja baada ya kung’olewa kwenye nafasi hiyo.

Kitwanga alifukuzwa kazi kwa madai ya kuingia bungeni na kujibu masali ya wizara yake akiwa amelewa.

Amesema kuwa, anamshukuru Mungu kwa kuondolewa katika nafasi hiyo na kwamba, huenda kama angeendelea kuwepo, angepata matatizo makubwa zaidi.

Na kwamba, hatua ya Rais Magufuli kumwondoa katika nafasi hiyo kitamsaidia kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kwa ukaribu zaidi tofauti na alivyokuwa kwenye nafasi ya uwaziri.

“Namshukuru sana Mungu kuondolewa katika nafasi hii (Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi) labda ameniepusha na mambo mengi ambayo yangeweza kunikumba na hii itanisaidia kuwatumikia wanamisungwi kwa ukaribu,” amesema Kitwanga.

Kitwanga baada ya kung’olewa katika nafasi hiyo, siku kadhaa baadaye alitimkia nchini Israel ambako inadaiwa kwenda kupumzika ambapo alirejea nchini hivi karibuni.

Baada ya kurejea nchini, Kitwanga moja kwa moja alikabidhiana Ofisi na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa Mwigulu Nchemba aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo. Nchemba alikuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Kabla ya kutimuliwa Kitwanga alikuwa akiandamwa na kashfa ya Kampuni ya Lugumi iliyopewa zabuni ya kufunga mashine za kutambua alama za vidole katika vituo vyote vya Jeshi la Polisi nchini.

Jeshi hilo liliingia mkataba na Kampuni ya Lugumi Enterprises ili kufunga mashine 108 nchi nzima lakini kampuni hiyo ilifunga mashine 14 tu.
Nimemuona wakati anaongea kama tayari alisha piga kile kilicho mponza
 
Baada ya kupokea mgao wako toka bilioni 37 mlizozipata kifisadi na kuongezewa bonus baada ya kupoteza ajira na kesi ndiyo Magufuli kishaipotezea rasmi ni lazima usijute sasa ni kula kuku tu za mabilioni yako haramu.
Kaingia na pikipiki 100 za kuwakopesha wana jimbo lake,chezea nguvu ya lugumi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nadhani ameshatambua rangi halisi ya serikali yake.

Jiuzulu na ubunge tu mzee upumzike kwa amani maana pesa uliyoipiga kwa wadanganyika ni ndefu mno.
Kuwepo bungeni bado kunahitajika kwake kwani kuna vinafasi vinamuwezesha kuwaona wakubwa
 
CHARLES Kitwanga, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema kuwa, hajutii ‘kutumbuliwa’ na Rais John Magufuli, anaandika Moses Mseti.

Ametoa kauli hiyo wikiendi iliyopita jimboni kwake Misungwi jijini Mwanza ikiwa ni takribani mwezi mmoja baada ya kung’olewa kwenye nafasi hiyo.

Kitwanga alifukuzwa kazi kwa madai ya kuingia bungeni na kujibu masali ya wizara yake akiwa amelewa.

Amesema kuwa, anamshukuru Mungu kwa kuondolewa katika nafasi hiyo na kwamba, huenda kama angeendelea kuwepo, angepata matatizo makubwa zaidi.

Na kwamba, hatua ya Rais Magufuli kumwondoa katika nafasi hiyo kitamsaidia kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kwa ukaribu zaidi tofauti na alivyokuwa kwenye nafasi ya uwaziri.

“Namshukuru sana Mungu kuondolewa katika nafasi hii (Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi) labda ameniepusha na mambo mengi ambayo yangeweza kunikumba na hii itanisaidia kuwatumikia wanamisungwi kwa ukaribu,” amesema Kitwanga.

Kitwanga baada ya kung’olewa katika nafasi hiyo, siku kadhaa baadaye alitimkia nchini Israel ambako inadaiwa kwenda kupumzika ambapo alirejea nchini hivi karibuni.

Baada ya kurejea nchini, Kitwanga moja kwa moja alikabidhiana Ofisi na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa Mwigulu Nchemba aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo. Nchemba alikuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Kabla ya kutimuliwa Kitwanga alikuwa akiandamwa na kashfa ya Kampuni ya Lugumi iliyopewa zabuni ya kufunga mashine za kutambua alama za vidole katika vituo vyote vya Jeshi la Polisi nchini.

Jeshi hilo liliingia mkataba na Kampuni ya Lugumi Enterprises ili kufunga mashine 108 nchi nzima lakini kampuni hiyo ilifunga mashine 14 tu.
Mimi nilifikiri hajuti kuingia kazini akiwa amelewa, kumbe kuondolewa kazini. Yupo sawa hata mimi siwezi juta kuachishwa madaraka ya kuteuliwa kwa mapenzi ya mteuaji.
 
Hana wasiwasi tena wa kuonyesha pesa yake hadharani. Maana nguvu ya Lugumi iliingia mpaka kwenye kuchangia kampeni za uchaguzi. Sasa wanavuna matunda ya Lugumi "kuwekeza"

Kaingia na pikipiki 100 za kuwakopesha wana jimbo lake,chezea nguvu ya lugumi
 
Hana wasiwasi tena wa kuonyesha pesa yake hadharani. Maana nguvu ya Lugumi iliingia mpaka kwenye kuchangia kampeni za uchaguzi. Sasa wanavuna matunda ya Lugumi "kuwekeza"
Kweli kabisa mkuu hakuna mamlaka ya kuhoji hapo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hana wasiwasi tena wa kuonyesha pesa yake hadharani. Maana nguvu ya Lugumi iliingia mpaka kwenye kuchangia kampeni za uchaguzi. Sasa wanavuna matunda ya Lugumi "kuwekeza"
Heshima yako mkuu lile swala la Lugumi limeshaisha mpango wao umeshafanikiwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Heshima yako mkuu lile swala la Lugumi limeshaisha mpango wao umeshafanikiwa
Tena kwa kutufunika na kaniki usoni huku wakituimbia nyimbo mzuri za kihindi, lugumi hiyooooo
 
Duh nchi yetu inaliwa wenye meno bado kuna watu wana imani kubwa CCM .
Tena kwa kutufunika na kaniki usoni huku wakituimbia nyimbo mzuri za kihindi, lugumi hiyooooo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Chama cha mafisadi ndivyo kilivyo!! Eti anatuzuga kajitoa kafara kupambana na mafisadi!
Kajitoa kafara wapi ule ulikuwa mkakati maalumu wameshamaliza kazi yao dili zimeshapigwa tayari manyumbu wamebaki kuimba CCM MBELE KWA MBELE
 
Back
Top Bottom