Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kramo usimuhukumu kwasababu hajacheza badoSimba IMEJAZA wazee na Mizigo
Tukipata nafasi tutawachambua Hawa wachezaji WABOVU..
1. AYOUB Lakred Bomu
2. Sadio Kanute Bomu.
3. Moses Phiri Bonu
4. Aubin Kramo Bomu.
5. Will Onana Bomu
6. Luis MIQUISSONE Bomu
7.( Saido Ntibazonkiza )
Kramo usimuhukumu kwasababu hajacheza bado
Dah sad..binafsi sikufurahishwa kurudishwa kwa konde pia.Hiyo ndio IMEISHA kaka.
Kwa historia ya Mpira wa Bongo HAIWEZEKANI Tena kucheza Tanzania.
Hayo yaliyomkuta kramo yamewakuta pia....
Thadeo Lwanga.
Peter Banda.
Hassan Dilunga
Asante kwasi nk
Dah sad..binafsi sikufurahishwa kurudishwa kwa konde pia.
Hilo CAPO DELGADO halina Akili Mkuu hivyo achana nalo litakupotezea muda wako.Kramo usimuhukumu kwasababu hajacheza bado
Kabla sijachangia chochote, chukua Kwanza maua yako kuhusu Onana. Ukiondoa goli la Simba day anabaki na urembo tu.Beki Chemalone
Yuko vizuri ila Kiufundi GENTAMYCINE nimemtizama na nimegundua amebarikiwa Akili nyingi na Nguvu, ila hana Kasi (pace) na inaweza Kutugharimu tukikutana na Timu zenye Mafowadi Viberenge.
Kipa Ali Salim
Alianza vyema na akawa anakuja vizuri ila Kiufundi kwa Mechi kadhaa na za hivi Karibuni GENTAMYCINE nimegundua amebadilika, amekuwa mpuuzi mno, ana Sifa na amezidisha kujiamini wakati bado hajafikia kiwango hicho kwakuwa anaendelea Kujifunza.
Muzamiru Yasini
Ni Kiungo Mzawa Bora kwa sasa Tanzania na ana Kipaji kikubwa ila Kiufundi huwa anafanya Makosa yasiyo na ulazima huku akipenda sana Usela ambao kuna muda Unamgharimu Kadi. Kama huwa anavuta Pisi 3 kwa Siku basi GENTAMYCINE nashauri awe anavuta Pisi 1 tu ili asidate sana na atufanyie kazi ambayo tunampendea.
Kibu Denis
Nasikitika ni kwanini mpaka sasa siwasikii Watanzania wakimuimba huyu Shujaa mpya wa Tanzania.
Ni Kocha yoyote Mpumbavu tu ndiyo hatoweza Kumpanga na Kumtumia Uwanjani.
Na laiti 95% ya Wachezaji wa Simba SC wangekuwa Wanacheza kwa Pace na Energy yake Kubwa waliyonayo kila Mechi tunashinda na hata Msimu uliopita Simba SC ingekuwa Bingwa wa NBC Premier League.
Hata hivyo Kiufundi baada ya Kumtizama GENTAMYCINE nimegundua ana tatizo Sugu la kutokuwa na Umakini na hata Tenki lake la Pumzi huwa si la Kumaliza dakika 90 za Mchezo.
Leandre Willy Essomba Onana
Nimemuona Mechi kadhaa ila Kiufundi GENTAMYCINE niseme tu kuwa Simba SC tulikurupuka Kumsajili kwani hana yale Makali ya Kuipambania Simba SC.
Anatumia muda mwingi kutafuta Ufalme wa haraka ndani ya Kikosi wakati hana Uwezo huo.
Anapenda Kucheza na Jukwaa Kipuuzi Kipuuzi, Kujiremba mno na Mchoyo wa kuwapa Pasi Wenzake wakiwa katika Nafasi za Kufunga.
Shomary Kapombe
Ni Mtu na Nusu na hajawahi Kuniangusha GENTAMYCINE ila ajitahidi tu kuwa na Maamuzi ya haraka na apunguze Kigugumizi chake cha Miguu ambacho kuna nyakati huwa Kinamgharimu.
Saido Ntibanzokinza
Ana Kipaji Kikubwa na Kilichotuka kabisa ila Kiufundi GENTAMYCINE nimegundua kuwa anapenda mno Kulazimisha kila Tukio alifanye Yeye wakati Kiuhalisia na kwa Umri wake kuna nyakati zingine anashindwa na hata Kuwagharimu Wenzake.
Haya na nyie Wengine (hasa wana Simba SC) hebu kwa nia njema tu toeni Ushauri wenu wa Kiufundi kwa Wachezaji wetu/wenu ili wabadilike upesi na wawe na Msaada Kwetu kwa Mechi zijazo/Michuano ijayo kuanzia na huu wa tarehe 20 Oktoba, 2023 dhidi ya Al Ahly SC katika Ligi Mpya ya African Football League (AFL).
Otherwise nina Imani na Simba SC.
Chukua like yako..ukiangalia hata Yanga walikua wanataka kumsajili Ngoma ili akacheze namba 8 na sio 6.Shida ya Simba ni kukosa kiungo namba 6 halisi. Na pia shida inaweza kuwa kwa Robertinho kwa kushindwa kukitumia kikosi ipasavyo mfano kama hakuna namba sita halisi kwenye kikosi, kocha anaweza kumtumia fullback kama inverted fullback mfano Zimbwe aungane na Mzamiru kama viungo wawili wa chini timu ikiwa inashambaulia na juu yake kuwe na namba 8 wawili mfano Ngoma na Saido.
Hii itasaidia timu ikiwa shambuliwa kwa counter attacks kwasbb kuna kuwa kuna uwiano wa idadi ya namba kutoka ushambuliaji hadi safu ya ulinzi.
Shida nyingine Mzamiru sio namba 8 bora kama alivyo Ngoma. Ngoma ana uwezo mzuri wa kuona mashimo/njia za mpira, kupiga pasi ndefu/fupi, kuusoma mchezo kuliko Mzamiru ambaye sifa yake kubwa ni kukaba tu ni vichache sana Mzamiru atakupa akiwa na mpira mguuni, swali kwann huwa anasogoea kama namba 8 na Ngoma kubaki namba 6? Hapa ndio sbb ya Simba kuruhusu magoli mengi kwa vile Ngoma sio mzuri kwenye kukaba na pia kipindi timu inashambuliwa Mzamiru huwa hayupo eneo la tukio.
La mwisho ni issue ya kisaikolojia kwa Kibu, tangia aifunge Yanga,,,, juhudi yake kurudi nyuma na kukaba imepungua, atafosi kupiga ata sehemu ambayo hapaswi kupiga badala ya kutengeneza nafasi kwa wenzake.