Kiufundi Wachezaji hawa wa Simba SC wakibadilika kwa yafuatayo nitashukuru na Simba SC itaimarika zaidi

Binafsi kwa msimu huu wachezaji waliosajiliwa niliyempitisha moja kwa moja ni Ngoma ila atafutiwemtu wa kusaidiana nae kukaba. Che malone nampa 70% akiongeza kasi na utulivu akiwa na mpira atakua tishio.
 
Simba IMEJAZA wazee na Mizigo
Tukipata nafasi tutawachambua Hawa wachezaji WABOVU..

1. AYOUB Lakred Bomu

2. Sadio Kanute Bomu.

3. Moses Phiri Bonu

4. Aubin Kramo Bomu.

5. Will Onana Bomu

6. Luis MIQUISSONE Bomu

7.( Saido Ntibazonkiza )
Kramo usimuhukumu kwasababu hajacheza bado
 
Kramo usimuhukumu kwasababu hajacheza bado

Hiyo ndio IMEISHA kaka.

Kwa historia ya Mpira wa Bongo HAIWEZEKANI Tena kucheza Tanzania.

Hayo yaliyomkuta kramo yamewakuta pia....
Thadeo Lwanga.
Peter Banda.
Hassan Dilunga
Asante kwasi nk
 
Hiyo ndio IMEISHA kaka.

Kwa historia ya Mpira wa Bongo HAIWEZEKANI Tena kucheza Tanzania.

Hayo yaliyomkuta kramo yamewakuta pia....
Thadeo Lwanga.
Peter Banda.
Hassan Dilunga
Asante kwasi nk
Dah sad..binafsi sikufurahishwa kurudishwa kwa konde pia.
 
Dah sad..binafsi sikufurahishwa kurudishwa kwa konde pia.

Kuna Upigaji unaendeleaje ndani ya Club
Kuna Billions Of Money za African super league 5

Mo akajiingiza na kujifanya analeta usajili WA KISHINDO kwa kuleta mchezaji mkubwa kutoka timu kubwa na kumleta goalkeeper Bora Africa

Ilikuwa Lazima Wasajili Miquisson na Mzungu au Mwarabu mmoja hata kama hakuna kitu. Ili IONEKANE Hela nyingi IMETUMIKA KWENYE usajili

Hela za super cup( African super league zimepigwa na Mo.
 
Shida ya Simba ni kukosa kiungo namba 6 halisi. Na pia shida inaweza kuwa kwa Robertinho kwa kushindwa kukitumia kikosi ipasavyo mfano kama hakuna namba sita halisi kwenye kikosi, kocha anaweza kumtumia fullback kama inverted fullback mfano Zimbwe aungane na Mzamiru kama viungo wawili wa chini timu ikiwa inashambaulia na juu yake kuwe na namba 8 wawili mfano Ngoma na Saido.

Hii itasaidia timu ikiwa shambuliwa kwa counter attacks kwasbb kuna kuwa kuna uwiano wa idadi ya namba kutoka ushambuliaji hadi safu ya ulinzi.

Shida nyingine Mzamiru sio namba 8 bora kama alivyo Ngoma. Ngoma ana uwezo mzuri wa kuona mashimo/njia za mpira, kupiga pasi ndefu/fupi, kuusoma mchezo kuliko Mzamiru ambaye sifa yake kubwa ni kukaba tu ni vichache sana Mzamiru atakupa akiwa na mpira mguuni, swali kwann huwa anasogoea kama namba 8 na Ngoma kubaki namba 6? Hapa ndio sbb ya Simba kuruhusu magoli mengi kwa vile Ngoma sio mzuri kwenye kukaba na pia kipindi timu inashambuliwa Mzamiru huwa hayupo eneo la tukio.

La mwisho ni issue ya kisaikolojia kwa Kibu, tangia aifunge Yanga,,,, juhudi yake kurudi nyuma na kukaba imepungua, atafosi kupiga ata sehemu ambayo hapaswi kupiga badala ya kutengeneza nafasi kwa wenzake.
 
Kabla sijachangia chochote, chukua Kwanza maua yako kuhusu Onana. Ukiondoa goli la Simba day anabaki na urembo tu.
 
Chukua like yako..ukiangalia hata Yanga walikua wanataka kumsajili Ngoma ili akacheze namba 8 na sio 6.
 
Boko kwa aliyo yafanya inatosha, aondoke kabla tuu kabla hajapoteza kale kasifa aliko jijengea kwa muda wote alio cheza msimbazi, sasa hivi muda mwingi anaikaba timu ni kama vile Simba hua inacheza pungufu akiwemo uwanjani, asome alama za nyakati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…