Mwanakijiji ukisoma hiyo mada hapo chini, ukatulia, ukatafakari basi utachukua hatua ya kuupenda mziki wa bongo fleva "kiujumla":
http://www.redet.udsm.ac.tz/documents_storage/2009-2-1-9-30-27_ndani%20ya%20bongo-utandawazi%20na%20migogoro%20ya%20utamaduni.pdf
Katika mada hiyo hapo juu kwenye tovuti utapata dondoo hii:
Vijana na Migongano ya Mitizamo Kuhusu Demokrasia
Utamaduni wa sasa wa vijana ni ule wa kutoficha kitu. Wanaimba na kuongea wazi juu ya matatizo yanayowakabili, wanafanya utani na kudhihakiana na wakati huo huo wakisisitiza upendo na kupendana. Kadhalika wanashirikiana, wasichana kwa wavulana, katika R&B na Hip Hop, na yote kwao ni Bongo Flava. Kwa mfano, Juma Nature ameshirikiana kurekodi na Profesa Jay, Lady Jay Dee (naye pia kashirikiana
na Mark T, Ray C, n.k.), Zay B, Inspekta Haroun na Mabaga Fresh; au Wagosi wa kaya wmeshirikiana First Mack, Lady Q, Johhny Walker, Ustaadhi Muarobaini na Mr. Paul. Wao tangu mwaka 1995 walishatamka kwamba "Vijana ni taifa la Leo!", wakimaanisha kwamba wao ndio wengi zaidi na inabidi haki zao zizingatiwe.
Ulikuwa ni utambuzi kwamba wazee walikuwa wameyahaini matamanio na mategemeo yao.18 Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2000, kwa mfano, kuna wimbo uliopigwa na Olduvai Gorge ukihimiza suala la uchaguzi. Wimbo huu haukudumu katika vyombo vya habari, kwani ulibainisha wazi unafiki na uongo wa baadhi ya
wagombea, na ukawataka watu wawakatae. Katika kibwagizo chake, vijana wali Rap: "Wabunge hawa Bwana! Kura tumewapa! Bungeni wamekwenda! Lakini, Laa! Balaa, Wanasinzia…."