Kiujumla, nachukia Bongo Flava!

Kiujumla, nachukia Bongo Flava!

Mimi sichukii bongo fleva
i am a big fan.....lakini
ninachukia mno wasanii wa bongo fleva....
Wana mentality za kishamba mno...
Wapo fake paka inaboa......

But nakubalina na mwanakijiji kwenye taarab na baadhi ya pointi,
nafikiri ukiwa na mawazo ya african renainsance kama mwanakiji lazima
bongofleva ikupe taabu......i understand the point.....
 
you are not alone...ni nyimbo chache sana za bongo fleva ndio nzuri...kuna huyu anajiita dudu baya, sijui hua anatoa ujumbe gani kwenye nyimbo zake...huwa simwelewi

Aneleza madudu yake! Huenda watu wakjifunza na kuyaacha hayo madudu
 
Yaani, ukija kwenye nyimbo za mapenzi kwa kweli wamekuwa kama waharibifu wa Classic taarab ambao nao siku hizi wamegeuze Taarab kuwa ndombolo ya aina fulani!

Ninaamini the kipindi cha dhahabu cha kutukuka kwa muziki wa Tanzania kilikuwa ni 70s na 60s wakati Taarab hadi hivi sasa nadhani bado ya Kina Siti Bint Saad bado wako juu.. ni sawa na kule misri na kina Kurthum..

I'm sorry! but I had to say it!

Si mpenzi wa taarab ki vile kwa kujilazimisha nilihudhuria onesho lao moja sehemu fulani; nikakutana na hiyo wanayoiita kiduku! Arghhhhhhhhh!
Taarabu imeporwa na ilekeako ni shimoni!

Nikajiuliza yule Mtunzi wa Njiwa; yu wapi?
 
Mwanakijiji ukisoma hiyo mada hapo chini, ukatulia, ukatafakari basi utachukua hatua ya kuupenda mziki wa bongo fleva "kiujumla":

http://www.redet.udsm.ac.tz/documents_storage/2009-2-1-9-30-27_ndani%20ya%20bongo-utandawazi%20na%20migogoro%20ya%20utamaduni.pdf

Katika mada hiyo hapo juu kwenye tovuti utapata dondoo hii:

Vijana na Migongano ya Mitizamo Kuhusu Demokrasia
Utamaduni wa sasa wa vijana ni ule wa kutoficha kitu. Wanaimba na kuongea wazi juu ya matatizo yanayowakabili, wanafanya utani na kudhihakiana na wakati huo huo wakisisitiza upendo na kupendana. Kadhalika wanashirikiana, wasichana kwa wavulana, katika R&B na Hip Hop, na yote kwao ni Bongo Flava. Kwa mfano, Juma Nature ameshirikiana kurekodi na Profesa Jay, Lady Jay Dee (naye pia kashirikiana
na Mark T, Ray C, n.k.), Zay B, Inspekta Haroun na Mabaga Fresh; au Wagosi wa kaya wmeshirikiana First Mack, Lady Q, Johhny Walker, Ustaadhi Muarobaini na Mr. Paul. Wao tangu mwaka 1995 walishatamka kwamba "Vijana ni taifa la Leo!", wakimaanisha kwamba wao ndio wengi zaidi na inabidi haki zao zizingatiwe.
Ulikuwa ni utambuzi kwamba wazee walikuwa wameyahaini matamanio na mategemeo yao.18 Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2000, kwa mfano, kuna wimbo uliopigwa na Olduvai Gorge ukihimiza suala la uchaguzi. Wimbo huu haukudumu katika vyombo vya habari, kwani ulibainisha wazi unafiki na uongo wa baadhi ya
wagombea, na ukawataka watu wawakatae. Katika kibwagizo chake, vijana wali Rap: "Wabunge hawa Bwana! Kura tumewapa! Bungeni wamekwenda! Lakini, Laa! Balaa, Wanasinzia…."

 
Kwa kuwa "kiujumla" Watanzania hatupendi kusoma mada ndefu na kwa kuwa Mwanakijiji ni mtu mwenye asili ya Tanzania pia, ngoja niongezee dondoo fupi kutoka kwenye mada ndefu iliyorejewa hapo juu:

zilizoletwa na utandawazi. Kinyume na dhana kwamba utandawazi umewafanya waige, wao wameweza kujiundia silaha ya kuupinga na kuyapinga maovu yote yanayowakabili kila siku na wakitaka watambulike kimataifa. Wanapingana na ulimwengu ambao unawadhalilisha na kuwabetulia pembeni kama nyangalika. Wale wasiokitaka kile ambacho vijana wanakiimba kwa madai kwamba hakieleweki, wanasingizia kwamba vijana hawa wanaiga mambo ya kigeni na kuharibu utamaduni wa Mwafrika. Lakini ukweli ni kwamba​
Hip Hop na R&B chimbuko lake ni mwingiliano wa tamaduni nyingi, zikiwemo za Kiafrika, na ni sehemu ya utamaduni wa ukinzani duniani. Kinachoitofautisha Hip Hop ya Kitanzania na ile ya Marekani kwa sasa hivi ni fani na maudhui yake, japo misingi inafanana. Hawa vijana
wanakataa kuisherehekea hii mipaka ya nchi iliyowekwa na akina Bismark mwaka 1884, na kuungana kiutamaduni na watu wengine wenye asili ya Afrika, popote pale wanapoonewa (Pan Africanism-umoja wa Waafrika, au
ukandawazi wa Waafrika). Wanaimba juu ya mambo ya kitaifa na kimataifa, na wameukana kabisa ukasuku. Wanadai haki ya uwezo wa kufikiria. Nyimbo zao zinawatambulisha kama wao ni nani, na wametokea wapi na kadhalika matatizo yanayowakabili na yanayowasibu.

 
Nimetumia dakika kumi na tano kusoma tena ile post bwana bendera....ninachoweza kusema ni kwamba bongo flava iko juu, anayeichukia na aichukie. Ukiondoa wimbo wa SMS ambao siwezi kusikiliza mstari wake wa wanza nikamaliza, vijana wanajitahidi na wanapendwa na wengi wa wabongo wanaoishi bongo.

naishi bongo na nazichukia bongo fuleva!!!
 
Si mpenzi wa taarab ki vile kwa kujilazimisha nilihudhuria onesho lao moja sehemu fulani; nikakutana na hiyo wanayoiita kiduku! Arghhhhhhhhh!
Taarabu imeporwa na ilekeako ni shimoni!

Nikajiuliza yule Mtunzi wa Njiwa; yu wapi?

mnyalu hiyo kitu ni uchafu, nashindwa kuelewa lengo la muziki wa aina ile hasa ni nini???

na huu nao atahri za utandawzi eeh??
 
Nakukubalia Mwanakijiji, kweli Music wetu umebomoka, kimantiki tumerudi nyuma, tunashindwa kupiga hatua ambayo kina Balisdya walivuka,
kweli tunashindwa kwenda mbio, tumekwama kwenye kila nyanja ya sanaa ma michezo. Aibu leo hakuna kitu chakujivunia hapa nyumbani.
 
Back
Top Bottom