Ukiondoa nyimbo chache na wanamuziki wachache wa Bongo Flava kiujumla naomba nikiri kuwa nachukia bongo flava; siwezi kusikiliza zaidi sekunda chache za mwanzo, nachukia wanavyoimba utadhani walizaliwa Marekani, nachukia wanavyobana pua na kuvuta maneno ya kiswahili, na ninachukia kwa sababu midundo yao yote karibu inafanana (sijui producer ni mmoja na arranger ndiyo producer huyo huyo!?) na ninachukia maudhui yao.. wako vulgar and nasty wakijaribu kujilinganisha na na magangsta wa US!
Yaani, ukija kwenye nyimbo za mapenzi kwa kweli wamekuwa kama waharibifu wa Classic taarab ambao nao siku hizi wamegeuze Taarab kuwa ndombolo ya aina fulani!
Ninaamini the kipindi cha dhahabu cha kutukuka kwa muziki wa Tanzania kilikuwa ni 70s na 60s wakati Taarab hadi hivi sasa nadhani bado ya Kina Siti Bint Saad bado wako juu.. ni sawa na kule misri na kina Kurthum..
I'm sorry! but I had to say it!
Mzee Mwanakijiji, hii ndio faida ya freedom of choice, preference na freedom of expression, chuki zako kwa bongo flavour ni relative.
Napenda Baadhi ya Bongo.
Nimesema kupenda na kuchukia zote ni relative, ndio maana kwa asiyeelewa classic music, akisema anachukia clasic music, hiyo ndio freedom yake of choice na freedom of expression, ila akiponda classic kwa hoja kuwa hasikii kitu, hizi sio hoja. The same applies to Jazz kwa wana jazz etc. etc.
love ya music ni taste na preference kama ilivyo love preference, kwa anaependa mwanamke mwembamba akisema wanawake wanene ni wabovu, anakuwa hajawatendea haki, maadam chaguo lake ni mamiss, wanene anakuwa hana mpango nao, sambamba na wagonjwa wa wanawake weupe, uzuri kwao ni rangi tuu, wakisema wanawake weusi ni wabaya, wanakuwa hawajawatendea haki.
Nikirudi kwenye msingi wako kuchukia Bongo Fleva siwezi jua taste yako, lakini kuna nyimbo nyingi tuu za Fleva, zimetungwa, zikatungika, zikaimbwa zikaimbika huku zikibeba ujumbe unaozama na uliojitosheza kwa vina na maudhu.
Ningeweza kukupa mifano michache laiti kwanza ningeliijua taste yako.
Ila pia nakubaliana na wewe, nyingi ya nyimbo hizi ni trash, na beat wana download tuu, ndio maana stage performance ni chache sana.Kwenye maktaba yangu, nina bongo fleva zaidi ya 100 ambazo ni nzuri, master pieces!.
Kulinganisha Bongo Fleva na nyimbo za 60's na 70's ni sawa na kulinganisha sera za Ujamaa na Kujitegemea na hizi za sasa za Free Market Economy.
Kitu ambacho kwa upande wangu, naona Bongo Fleva za Zamani zilikuwa nzuri na zimetulia kuliko hizi za sasa. Ukimsikiliza Zahiri Alli enzi za Kimulimuli, 'Tumerudi Kishujaa', ukaja kumsikiliza enzi za Sambulumaa 'Cleopatra' na ukimsikiliza sasa kwenye wimbo wa ' Inasikitisha', utakubaliana na mimi, Zahir Ali is the same but his music is not the same, he is loosing.
The same aplies to Balisidya enzi za Afrosa na alipoibuka na 'Shida'. Ndio maana mpaka leo, ukimsikiliza Marijani Rajabu, utakubali kuwa bado pengo lake halijazibika. Ya kale ni dhahabu! Hivyo kufananisha pure gold na English gold, unakuwa hujaitendea haki English gold.
Hoja zako kwenye uharibifu wa taarabu, nazikubali.