Kiukweli kuna baadhi ya watu mavazi fulani au sare fulani zinawapendeza na wanatokelezea. Shuhudia wanavyopendeza!

Kwahiyo umeleta mtego wa panya, unataka tupunguzwe mitaani!
Niandikie komenti yangu.
 
Hahahaha tafakari mkuu kwanini siku hizi JF unadharaulika tofauti na mwanzo watu walikuwa wanapenda mabandiko yako? sawa pamoja na ukilaza wetu hapa, kwani mkuu umeanza kulalamikiwa leo? mabandiko yako siku hizi hayana mashiko, mbona mwanzo awe CCM, CDM tusio na vyama tulikuwa tunapenda mabandiko yako? sababu ni moja tu ulikuwa una andika fact ambazo kila mtu alikuwa anajua unajenga hoja zenye kuelimisha sn, sawa binadamu ni dynamic nakubali mfano wachukue Ndugai na J Ulimwengu nani jamii ina mheshimu? Ndugai na Pro Assad nani ana heshimika au Bashiru na Lissu nani jamii ina mheshimu? Leo G Malisa ana heshimika kuliko PM. tatizo lilipo ni tamaa tu ndiyo inatutesa tunaacha ukweli njaa zinakuwa mbele. Asante mkuu
 
Kwani tunaongelea hoja ya umuhimu wa miradi kwa taifa? Nilidhani hoja yako ni kuwa miradi ya awamu ya tano yote ni ya JK.

Ila upo sawa Chato airpot kwa sasa sioni umuhimu wake. Naona ni hasara.
Hiyo miradi ya kulitia hasara taifa kwanza hata kuongelewa haitakiwi.

Hiyo miradi haikuwa kipau mbele cha watanzania au taifa bali ni maamuzi binafsi ya kiongozi.
 
Tanzania kuna watu hawaelewi uzito wa dhana nzima ya "Civilian control of the military" and "Justice must not only be done, it must seem to be done".

Likewise, civilians must not only control the military, they must seem to control the military.

Maana yake, viongozi wa kiraia waliochaguliwa kwa kura hawatakiwi kuonekana katika muonekano wa kijeshi.
 
Hilo lingetumika kama haki ya mpiga kura ingeheshimiwa kwenye uchaguzi.
 
Inachukua muda mrefu kujijengea heshima, mfupi mno kuipoteza mazima.

 
Ujinga mtupu we ukiona mtu anashikwa makalio na wazungu ujue hakuna kitu hapo
 
Kuna kesi ya Mbowe nilitegemea ushushe nondo kama mwanasheria na mwandishi wa habari mwandamizi lakini siku hizi huna tofauti na Kibajaji au Ndugai
Kama mwanasheria na wakili hawezi kuingilia mahakama. Hata Lissu hajasema lolote kuhusu hiyo kesi kwababu hiyo hiyo.
 
Ajitafakari kwanini jamii now inamdharau Paschal?
Nadhani sababu moja wapo ni kuiacha mkono Chadema kwenye kuisapoti. Kitendo ambacho ni dhambi kubwa Sana.

Kama ulikuwa mtu utakuwa kuku, kama ulikuwa mwenye akili utakuwa zuzu.
 
Sasa nimeamini wewe ni mtoto wa "nyoka", mwanzoni nilidhani ni fix zako za kupenyeza habari maalumu kwa jamii bila kustua watu. Ha ha haaa! Sasa ngoja nikupeleke kwenye fani yako ingawa mimi si mwandishi wa habari.
====
MAHOJIANO YA NDUGU PASCAL MAYALLA NA TUJITEGEMEE WA KITUO CHA HABARI CHA JAMIIFORUMS.COM JUU YA TATHMINI YA MAENDELEO YA NCHI YETU YALIVYOCHANGIWA NA VYOMBO VYA HABARI TOKA TUPATE UHURU MIAKA 60 ILIYOPITA

TUJITEGEMEE: Habari za leo watumiaji wa kituo hiki bora cha habari. Ninawaribisha, na kwa kweli karibu sana watumiaji wetu wa kituo hiki bora cha habari barani Africa na duniani kwa ujumla mahali lugha ya kiswahili inatumika. Wapendwa watumiaji wa kituo hiki ninafurahi kuwakumbusha kuwa nchi yetu itakuwa inasherekea kumbukumbu ya kujipatia uhuru miaka 60 iliyopita ambao tuliupata tarehe 09/12/1961. Miaka sitini ni mingi na katika wingi huo kuna mambo mengi ya kimaendeleo yamefanyika katika kulistawisha taifa hili. Maendeleo haya yamepatikana kutokana na juhudi mbali mbali kutoka kwa wadau mbali mbali wakiwemo wahandishi wa habari. Wandishi wa habari na watangazaji wa habari wametoa mchango mkubwa tena kwa jasho na damu. Kwa hiyo juhudi zao hizi hatuwezi kuzipuuza tunapofanya tathmini ya maendeleo yetu kama nchi toka tupate uhuru miaka sitini iliyopita.

Kwa msingi huo ndani ya kituo chetu hiki bora cha habari duniani cha JF tumemkaribisha Ndugu yetu, mwananchi mwenzetu, mwanasheria kwa kusomea na kubwa kuliko nguli wetu wa habari kwa kuandika na wakati fulani kuzitangaza na kuzichambua habari hizo hapa nchini na nje ya nchi. Huyu pia anaaminika kuwa nguli wa habari za kiuchunguzi akiamua kufanya hivyo. Kwenye habari, nguli huyu sifa zake ni nyingi nikizieleza hapa zote nitawachosha kwa wingi wa sifa kemkem za mwana habari huyu. Wapendwa watumiaji wa kituo hiki, nguli huyu si mwingine bali ni ndugu Pascal Mayalla, ambaye amefanya kazi katika vituo mbalimbali vya habari hapa nchini vikiwemo vya serikali na vya binafsi. Pia ndugu Mayalla ni mjasiriamali kwenye tasnia ya habari. Lengo hasa la kuwa na Ndugu Mayalla hapa ni kufanya mahojiano naye juu tathmini ya mchango wa vyombo vya habari katika kuliletea taifa letu maendeleo.

Mkuu, nguli wa habari Ndugu Pascal Mayalla, habari za leo na karibu sana kwenye kituo chetu na karibu uwasalimie watumiaji wa kituo hiki kisha tuendelee na lengo hasa la kukualika hapa.

MAYALLA: Asante sana ndugu TUJITEGEMEE. Habari za leo nzuri. Watumiaji wa kituo hiki muhimu cha habari nawasalimu sana. Nimefurahi sana kukaribishwa hapa kwa ajili ya mahojiano muhimu sana juu ya mchango wa tasnia ya habari katika kufanikisha maendeleo tuliyonayo leo kama nchi toka tupate uhuru mwaka 1961. Kwa mara nyingine asante sana.

TUJITEGEMEE: Tuanze mahojiano yetu juu ya habari za upatikanaji wa uhuru wa nchi yetu. Ndugu Mayalla, ni lini hasa ulianza kusikia habari za uhuru wa nchi yetu na nini hasa kilikusukuma kuzifuatilia kwa karibu sana?

MAYALLA: ......
 
Rais Samia sio mtu wa mchezo mchezo kama wengine walivyo mdhania kuwa utawala wake huenda unge kuwa lege lege.

Kulikuwa na mchanganyiko wa mawazo tofauti;

wapo walio kuwa na hofu wakidhani kuwa nchi inaweza kuyumba.....n.k
wapo baadhi ya wana siasa waliona sasa ikulu ile paleeeeeeeee......

Kumbe Amiri Jeshi Mkuu Rais Samia alikuwa anapiga rada tu......ni Imara zaidi ya chuma cha pua.
kama ni medali....basi anastahili kuvishwa medali ya kiviti.
Nampa saluti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…