Kiumbe kinachokula nishati yako (The Pain-Body)

Kiumbe kinachokula nishati yako (The Pain-Body)

Chosen Rich

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2019
Posts
1,565
Reaction score
1,118
Uliwahi kugundua kuwa kuna siku unaamka ukiwa na furaha na amani tele, lakini ghafla baada ya saa chache labda kwa sababu ya neno moja dogo uliloambiwa, au wazo moja tu baya lililopita kichwani unajikuta unadondokea kwenye giza nene la hasira, huzuni, au unyonge ?

Hiyo hali haitokei kwa bahati mbaya. Kuna "Kiumbe" kiko ndani yako kinachofanya kazi hiyo. "The Pain-Body" (Mwili wa Maumivu).

Hiki sio kiumbe cha nyama na damu, bali ni mkusanyiko wa nishati hasi iliyotokana na majeraha yako ya nyuma: kufeli, kukataliwa, migogoro ya utotoni, au mahusiano yaliyovunjika.

Kiumbe hiki kinaishi ndani yako na kina tabia kuu tatu unazotakiwa kuzijua:

1. Kina Tabia ya Kulala na Kuamka (Dormant vs Active)​

Muda mwingi kiumbe hiki kinakuwa kimeshaidishwa (kisiwa cha utulivu). Lakini kikipata kichocheo kidogo tu (Trigger) kama vile mtu kukuudhi, kupishana lugha na mtu au mshirika wako wa kibiashara, au picha fulani mtandaoni kiumbe hiki kinaamka kwa kasi ya ajabu.

2. Chakula Chake Kikubwa ni "Drama" na Mawazo Hasi​

Kikishaamka, kiumbe hiki kina njaa kali sana, na hakili ugali au ndizi; kinakula nishati yako.

  • Ili kile na kikue, kinaanza kukulubuni uanze kuwaza makosa mengine yote uliyowahi kufanya miaka mitano iliyopita.
  • Kinasukuma akili yako kutafuta ugomvi na watu walio karibu nawe, kulalamika, au kujihurumia. Kinafanya hivyo makusudi kwa sababu Drama ndio chakula chake kikuu. Kinataka uteseke ili chenyewe kiishi.

3. Kinajigeuza Kuwa Ndio "Wewe"​

Mtego mkubwa zaidi wa kiumbe hiki ni kukufanya uamini kuwa ile hasira au huzuni ndio "Wewe". Unajikuta ukisema "Mimi nina hasira sana leo" badala ya kuona kuwa kuna nishati ya hasira imevamia mfumo wako.

Unakiuaje Kiumbe Hiki Ili Kilinde Nishati Yako?​

Nini kifanyike ndugu mtaalamu?
Cha kufanya ni hivi ile hali ya giza au hasira inapoanza kupanda, usikimbilie kwenye simu, Kunywa pombe, au kuanza kugombana…Tulia na ujiambie "Ah! Kiumbe cha maumivu kimeamka sasa hivi"
Kishuhudie Mwilini Mwako, Yani badala ya kufuata mnyororo wa mawazo hasi yanayoletwa na akili yako, elekeza umakini wako kwenye uhalisia wa mwili…Hisi kifua kinavyobana, mapigo ya moyo yanavyoenda kasi, au tumbo linavyosokota. Kaa na hiyo hisia bila kuihukumu.
Kinyime Chakula, Unapokiangalia kiumbe hicho kwa utulivu bila kukipa mawazo mapya ya lawama au kulalamika, unakuwa umekata mzunguko wa chakula chake. Kinakosa nishati, kinadhoofika, na mwisho kinayeyuka chenyewe.
 
Hakiwezi kufa kabisa chief, kwasababu kina asili ya kibiolojia na kisaikolojia, Sisi ni binadamu, si roboti, Kwahiyo mfumo wetu wa neva na akili uliumbwa kuhifadhi kumbukumbu za maumivu na hatari ili kutulinda…Kumbukumbu na maumivu yote ya nyuma yaliyotengeneza hicho kiumbe bado yapo kwenye mfumo wako wa ubongo

Na kwakua bado unaishi duniani, utakutana na changamoto mpya, msuguano na watu, msongo wa kazi, au kupoteza vitu unavyovipenda….Vitu hivi ni vichocheo (triggers) ambavyo vinaweza kukiamsha kwa muda mfupi
 
Kiumbe chanya yupo pia ila nataka uelewe kupitia huu mfano
Fikiria viumbe hivi viwili kama mabondia wawili waliopo ndani yako

bondia Hasi umekuwa ukimlisha na kumpa mazoezi tangu utotoni (kila unapowaza makosa ya nyuma, kila unapokasirika, unapofuatilia drama, na unapowaza hofu kuhusu kesho) Yani amekuwa jitu kubwa lenye misuli.

Bondia Chanya umekuwa ukimpa chakula kidogo sana (sekunde chache tu za utulivu au shukrani kwa siku)

Ni nani atakua na nguvu na kelele nyingi ulingoni ?
 
Hakiwezi kufa kabisa chief, kwasababu kina asili ya kibiolojia na kisaikolojia, Sisi ni binadamu, si roboti, Kwahiyo mfumo wetu wa neva na akili uliumbwa kuhifadhi kumbukumbu za maumivu na hatari ili kutulinda…Kumbukumbu na maumivu yote ya nyuma yaliyotengeneza hicho kiumbe bado yapo kwenye mfumo wako wa ubongo

Na kwakua bado unaishi duniani, utakutana na changamoto mpya, msuguano na watu, msongo wa kazi, au kupoteza vitu unavyovipenda….Vitu hivi ni vichocheo (triggers) ambavyo vinaweza kukiamsha kwa muda mfupi
reprogramming your subconscious inaweza kukififisha kama utakuwa na concistency kwa siku 90 hadi miezi 6 alafu baada ya hapo iwe ni life style inawezekana ila inahitaji nia dhabiti hapo angalau utaififisha hio nguvu hasi
 
Kabidhi maisha yako kwa BWANA YESU ili yawe sio ya kwako tena. Roho wa Mungu yaani Roho Mtakatifu Ataingia ndani yako na Atakuwa Anakuongoza katika yote. Negatives zote zinakufa kifo cha asili. Unaanza kuyaishi mapenzi ya Mungu. Unaanza kugundua kuwa maisha ni zaidi ya jinsi tuwazavyo. Unajua kuwa maisha ni milele pamoja na Mungu.

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
reprogramming your subconscious inaweza kukififisha kama utakuwa na concistency kwa siku 90 hadi miezi 6 alafu baada ya hapo iwe ni life style inawezekana ila inahitaji nia dhabiti hapo angalau utaififisha hio nguvu hasi
Kumbe inawezekana kuondoa kabisa!
 
Naombeni msaada wa kua na nguvu chanya naona hii nguvu hasi inanizidia yaani kila ninapokua na furaha Kuna sauti kichwani inaniletea matukio yahofu ili mradi niwe depressed all days
Hiyo hali ya nguvu hasi inapokuvamia usishindane nayo,
Tulia uwe kama mtu anayeshuhudia mwilini Mwako, Yani badala ya kufuata mnyororo wa mawazo hasi yanayoletwa na akili yako, elekeza umakini wako kwenye uhalisia wa mwili…Hisi kifua kinavyobana, mapigo ya moyo yanavyoenda kasi, au tumbo linavyosokota.. Kaa na hiyo hisia bila kuihukumu.
Unapoiangalia hiyo hali kwa utulivu bila kuweka mawazo mapya ya lawama au kulalamika, unakuwa umekata mzunguko huo unaokusumbua..unapunguza nishati ya nguvu hasi, inadhoofika, na mwisho inayeyuka kabisa
 
Asantee sana
 
Back
Top Bottom