Kiumbe mkubwa nyuma ya kiti cha Rais na hatma ya maendeleo yetu

Deception

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2014
Posts
1,183
Reaction score
3,167
Mnamo mwaka 1910 nchini Marekani kulikuwa na watu wenye uwezo mkubwa kiuchumi ambao walikutana pamoja katika kisiwa cha Jekyll katika pwani ya Georgia.Watu hawa J.P Morgan,William Rockefeller na jamaa zao wa karibu walikuwa na uwezo wa kiuchumi sawa na asilimia 25 ya uchumi wa dunia yote.

Katika mkutano wao pia waliwahusisha watu wa serikali ya Marekani ambapo lengo lao kubwa la kukutana ni kuunda mfuko wa fedha ambao ungeisadia serikali katika wakati wa shida au wakati ambapo serikali itakuwa imeishiwa na fedha kabisa.

Mfuko huu huitwa Federal Reserve System(FED).Mfuko huu kiuhalisia haumilikiwi na serikali ya Marekali bali humilikiwa na watu hawa waliotajwa hapo juu na jamaa zao wa karibu.

Watu hawa waliunda mfuko huu kwa madhumuni ya kumiliki mambo yote ya kifedha nchini Marekani na hata dunia nzima,kwa mtu anayejua vizuri sayansi ya fedha na jinsi mfuko huu unavyofanya kazi ni rahisi kwake kuelewa jinsi watu hawa wanavyonufaika na mfuko huu.Watu hawa hujiingizia fedha nyingi sana kupitia mfuko huu.

Fedha hizo huwawezesha kutimiza majukumu mengine muhimu ambayo wameyalenga bila kupata kikwazo.Fedha hizo zinatumika kumiliki/kutawala mamlaka,taasisi au mashirika kwa kuwanunua wale ambao wanaongoza mamlaka,taasisi au mashirika husika.Hununua wanasiasa,vyama vya siasa,televisheni,Redio,magazeti,vyuo vikuu,vyama vya wafanyakazi,mashirika ya biashara na taasisi nyingine zinazofanana na hizo.

Watu hawa ndio watawala halisi katika serikali ya Marekani na ndio wanaoamua mambo yote ya kiserikali,rais wa Marekani anatumwa tu kutekeleza.

Watu hawa ndio ndio walioshinikiza kuundwa kwa umoja wa mataifa(UNO) mwaka 1945 baada ya kushindwa kundeleza jumuiya ya mataifa(League of Nations) iliyondwa na hao wenyewe mwaka 1920 lengo lao kubwa ni kupanua wigo wa kutawala kuvuka mipaka ya Marekani.

Agenda zote za kuundwa jumuiya ya mataifa na umoja wa mataifa zilianzishwa na marais wa Marekani ambao ni Woodrow Wilson 1920 na Franklin D.Roosevelt 1945.

Mashirika mbalimbali ya UNO yaliundwa kutegemea na maeneo ambayo walilenga kutawala kama vile Benki ya dunia(World Bank),mfuko wa fedha wa dunia(IMF),shirika la afya duniani(WHO),shirika la chakula na kilimo(FAO),shirika la wafanyakazi duniani(ILO) na mengineyo.Mashirika yote ya kifedha yana makao yake makuu nchini Marekani,yaani IMF na World Bank.

Katika safari yao ya kujikusanyia mamlaka wanafanya mambo mengi sana likiwemo lile la kumiliki wanasiasa ambalo nilishalitaja hapo juu ili kujimilikisha mali asili na malengo mengine nje ya mali asili katika nchi husika ambazo wanasiasa hao wanatoka au wanaishi.

Watu hawa wanapohitaji jambo fulani katika taifa husika,hufanya kila njia ili wafanikiwe bila kujali madhara yatakayotokea.Wanapohitaji mali asili fulani au jambo fulani kutoka nchi fulani ambalo ni muhimu kwao hutumia njia kuu tatu kutegemea na ugumu wa nchi au kiongozi wake ,njia hizo ni ‘economic hitman'(huuwa/hurubuni uchumi wa nchi),'the jackals'(mtaalamu/wataalamu wa mauaji ili kumuua anayekwamisha malengo) na ‘military'(hutumia nguvu za kijeshi ),mwandishi wa kitabu kimoja kiitwacho Confessions of an Economic Hitman aitwaye John Perkins anafafanua vizuri sana suala hili.

John Perkins mwenyewe alikuwa ‘economic hit man' hivyo mambo anayoeleza kwenye kitabu chake ni yale ambayo amekutana nayo yeye mwenyewe akiwa kazini.

Katika historia kuanzia mwaka 1950 nchi nyingi ziliwahi kukumbwa na msukosuko kwa viongozi wa nchi hizo kutokukubaliana na matakwa ya watu hawa.Baadhi ya viongozi wa nchi hizo waling'olewa madarakani na wengine waliuawa.

Baadhi ya nchi hizo ni Iran, Guatemala, Equardo, Panama, Venezuela, Afghanistan, Iraq, Libya na sasa watu hawa wapo Syria.Kiongozi atakaye kubaliana na matakwa ya hawa watu ndiye pekee atakayedumu madarakani.
Hakuna ubishi kwamba Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi sana yakiwemo madini mbalimbali pamoja na gesi iliyogundulika hivi karibuni.

Rasilimali hizi ni muhimu sana si tu kwa watu hawa bali pia nchi nyingine tajiri duniani zinakodolea macho.Mazingira yote yanajionesha kwamba watu hawa wamesha jichimbia nchini mwetu wakimiliki rasilimali hizi pamoja na kutimiza malengo mengine nje ya hapo.

Jambo hili linathibitisha kwamba wamefanikiwa kununua kiti cha rais wetu pamoja na kwamba anayekaa kwenye kiti hicho ni mtanzania mwenzetu.Kwa mtu yeyote mwenye upeo mkubwa atabaini kwamba kutokana na ukweli huu kuna mambo fulani ya kimaendeleo nchini kwetu hayatawezekana kamwe kwa kuwa hatuongozwi na rais wetu bali kiumbe aliye nyuma ya kiti chake ndiye anayetoa amri zote kuhusu mambo muhimu.Rais wetu wa sasa na yeyote atakayekuja baada yake hawana ubavu wa kupingana na kiumbe huyu.

Kama kiumbe huyu alidiriki kuua rais wa nchini mwake JF Kennedy, basi kwake ni rahisi zaidi kuua yeyote Yule atakayepingana na mipango yake.

Kutokana na ukweli huu nadadavua kwamba,kama rais wa nchi yoyote ile atakuwa na urafiki na serikali ya Marekani basi lazima awe adui kwa wananchi wake,na rais yeyote atakayekuwa na urafiki na wananchi wake basi lazima awe adui kwa serikali ya marekani na hivyo hatadumu madarakani.

Katika hali kama hii katiba mpya haina maana au mantiki tena hata kama itashushwa kutoka mbinguni,kupiga kura ili kuchagua viongozi hakuna maana tena,mipango yote ya maendeleo kwenye elimu haina maana tena,mipango yote ya maendeleo kwenye kilimo haina maana tena,mipango yote ya maendeleo kwenye afya haina maana tena,hakuna tena dira ya maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa misingi yote ya maendeleo imeshikwa au inamilikiwa na kiumbe huyu mkubwa.
 
Kweli ndio huo lakini hatupaswi kukata tamaa kabisa. Nakumbuka ktk somo la uchumi nilipitia MultiNationalCooporation hii ilinifanya kukata tamaa kama mtoa Mada. Kama mnakumbuka sakata la Karamagi kusaini mkataba nje ya nchi. Hizi ndio kazi zao.Kwa maana wao ndio wamiliki halisi wa rasilimali duniani.
 
umekata tamaa na umejaa woga, nikusaidie kidogo tu kwamba sheria za kisayansi zinabainisha kwamba hakuna jambo lolote lisilowezekana katika ulimwengu huu, kitu cha msingi ni kulipangilia kwa umakini na kisayansi, kwa maana hiyo hutakiwi kuogopa kwani hao unaowasema ni binadamu kama wewe wanaakili kama wewe, wao wanatake advantege ya weakness za watu wengine lakini si tishio katika ulimwengu wa fikra pevu, kama taifa tunaweza kuwaovercome kama tu tutaacha siasa uchwara na kuwekeza katika think tanks ili wawe chachu ya mabadiliko katika nyanja mbalimbali
 
Mtoa mada wewe unaonekana ndio wale mnaoishi kwa kutegemea misaada, hivyo unapoona utakosa misaada uko radhi hata mkeo atembee na mtu mwenye pesa mbele ya macho yako kisa usikose misaada. Ni hivi tunataka katiba mpya yenye kubeba malengo na matakwa ya wananchi na sio ya hao matajiri wa dunia. Kama wewe na wenzako mnawaogopa hao wazungu hivyo wanawaamulia cha kupitisha kwenye nchi kaeni pembeni tuachieni sisi tusiowaogopa hao wazungu. Tutaweka kila kitu wazi kwa wananchi ni jinsi gani tunawategemea wazungu na kwanini na hatimaye wananchi watajua nini cha kufanya ili kujikwamua na utegemezi kupitia mipango mizuri tutakayojiwekea. Kwa hiyo unamaanisha hao jamaa wa huko nje ndio wanataka sisi tuwe maskini? Hiyo mikwara ya kishamba namna hiyo pelekea waoga wenzio.
 
Mbona Mugabe kadumu madarakani japo ni adui wa USA?
Vipi Botswana mbona wameweza kujiletea maendeleo kwa kutumia raslimali zao?
 
Nilichokibaini kwa ninyi mliotangulia kuchangia ni aidha hamjasoma post hii mpaka mwisho,au hamjaelewa context ya hii post au hamna uelewa wa kutosha kuhusu mfumo mzima wa hawa watu wazito.
Kuhitimisha kwamba mimi nimekata tamaa ni wazi kabisa hamjaelewa maana ya post hii ni nini.Ili tuweze kupata maendeleo kwanza inabidi tuelewe matatizo yetu ya msingi ni ya namna gani,sio kukurupuka na kusema katiba mpya ndio itatatua matatizo yetu,au ujasiri ndio utatatua matatizo yetu.Wangapi wana katiba nzuri na viongozi majasiri wanaopenda wananchi wao lakini wamepotea?Iraq,Libya,Panama,Equador,Afghanistan,Syria na nyingine nyingi.Cha msingi kwanza ni kujua msingi wa tatizo,halafu uje kuanisha njia za kutatua tatizo.Tatizo letu la msingi sisi sio katiba wala ujasiri wa viongozi.SOMENI TENA LABDA MNAWEZA KUJA TOFAUTI.
 
Hii mada aliyotoa kabla hamjaikosoa jaribuni kuitafakari kwa maana ya historia ya nchi yetu na nchi nyingine hapa Afrika.
Kuna mashiko makubwa ya anachokiongea mtoa mada. Msipokubaliana nae sasa labda mtakuja tena baadae
 
tindo

Unaongelea wananchi wa Tanzania??? Safari bado ni ndefu sana, na katiba itapita tu.
 
Last edited by a moderator:
....haya mambo yanahitaji kutuliza akili kidogo tu na kukokotoa hesabu rahisi tu. Alichoeleza mleta mada kina mantiki (siyo kwamba nakiamini asilimia mia) lakini urafiki wowote na marekani (hasa nchi za dunia ya pili na ya tatu) haujawahi kuleta tija kwa wananchi wake. Misaada yake ni kizungumkuti....Viongozi wa nchi lengwa huwezeshwa kuogelea katika utajiri na sifa za kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa, huku wananchi wakitaabika.....jiulize kwanini chanjo ya malaria haijapatikana (tunagawiwa vyandarua vyenye dawa kwa ajili ya kuwakinga(?) baadhi ya wanafamilia badala ya kupewa dawa yenyewe kwa ajili ya fumigation ili kukinga familia nzima) au kwanini tukimbilie kuanzisha mfuko wa kupambana na ukimwi (ugonjwa unaoepukika) badala ya mfuko wa malaria?? Kwanini kunakuwa na kampeni kubwa ya chanjo (tena bure) kwa magonjwa kama surua na polio wakati vifo vitokanavyo na magonjwa hayo havifikii hata robo ya vile vitokanavyo na malaria??...mengine nitaeleza nikipata muda
 

good perception.
 
Je Huyu kiumbe hayupo nyuma ya kiti cha rais wa Zimbabwe (mgabe) ? Tatizo ni watawala wetu
 
Hoja mujarabu , muhimu nililolighamua ni kuwa kuna umuhimu mkubwa kujifunza kutatua matatizo kwa kujua chanzo cha matatizo yetu na si kutafuta matokea ya matatizo yetu kuna hatua muhimu sana za kufanya ikiwa ni pamoja na kuijaza imani ya ushindi kwenye mioyo kwa wale wote waliokata tama.
 
Tatizo sio mmarekani, wengi mnaamini matatizo mengi ya dunia yanasababishwa na mmarekani, USA inatumika kama fimbo ya kuchapia wengine,ila mwenye dunia ni Vatican na makundi yake ndo wanacontrol dunia Makundi hayo ni Jesuits, Illuminatti, Mashirika yao ya fedha, Central bank zao ndo zina manipulate politics, finance, TV nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…