Kiumbe mkubwa nyuma ya kiti cha Rais na hatma ya maendeleo yetu

Kiumbe mkubwa nyuma ya kiti cha Rais na hatma ya maendeleo yetu

Watu hao / kiumbe huyo ni 'mababeru' kama CCM inavyo jaribu kuaminisha wana wa mtaa wa Lumumba buku saba.
 
Wakati mwingine viongozi hawa wa ulimwengu wa tatu na mataifa mengine hukaribisha kuingiliwa na haya mataifa
 
Mtoa mada wewe unaonekana ndio wale mnaoishi kwa kutegemea misaada, hivyo unapoona utakosa misaada uko radhi hata mkeo atembee na mtu mwenye pesa mbele ya macho yako kisa usikose misaada. Ni hivi tunataka katiba mpya yenye kubeba malengo na matakwa ya wananchi na sio ya hao matajiri wa dunia. Kama wewe na wenzako mnawaogopa hao wazungu hivyo wanawaamulia cha kupitisha kwenye nchi kaeni pembeni tuachieni sisi tusiowaogopa hao wazungu. Tutaweka kila kitu wazi kwa wananchi ni jinsi gani tunawategemea wazungu na kwanini na hatimaye wananchi watajua nini cha kufanya ili kujikwamua na utegemezi kupitia mipango mizuri tutakayojiwekea. Kwa hiyo unamaanisha hao jamaa wa huko nje ndio wanataka sisi tuwe maskini? Hiyo mikwara ya kishamba namna hiyo pelekea waoga wenzio.
Mkuu naona hutaki kuelewa!
 
tindo

Unaongelea wananchi wa Tanzania??? Safari bado ni ndefu sana, na katiba itapita tu.
Labda ingekuwa wananchi wa Nchi ya Zanzibar kama wasingekuwa wamekaliwa na koloni lao,ingewezekana,maana wao wanajitambua.
 
Tatizo kubwa kuwaza chanjo ni lazima watuletee wazungu.

Sasa kwa akili hizi kwa nini huyu kiumbe mzito nyuma ya Rais asitawale?
....haya mambo yanahitaji kutuliza akili kidogo tu na kukokotoa hesabu rahisi tu. Alichoeleza mleta mada kina mantiki (siyo kwamba nakiamini asilimia mia) lakini urafiki wowote na marekani (hasa nchi za dunia ya pili na ya tatu) haujawahi kuleta tija kwa wananchi wake. Misaada yake ni kizungumkuti....Viongozi wa nchi lengwa huwezeshwa kuogelea katika utajiri na sifa za kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa, huku wananchi wakitaabika.....jiulize kwanini chanjo ya malaria haijapatikana (tunagawiwa vyandarua vyenye dawa kwa ajili ya kuwakinga(?) baadhi ya wanafamilia badala ya kupewa dawa yenyewe kwa ajili ya fumigation ili kukinga familia nzima) au kwanini tukimbilie kuanzisha mfuko wa kupambana na ukimwi (ugonjwa unaoepukika) badala ya mfuko wa malaria?? Kwanini kunakuwa na kampeni kubwa ya chanjo (tena bure) kwa magonjwa kama surua na polio wakati vifo vitokanavyo na magonjwa hayo havifikii hata robo ya vile vitokanavyo na malaria??...mengine nitaeleza nikipata muda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada wewe unaonekana ndio wale mnaoishi kwa kutegemea misaada, hivyo unapoona utakosa misaada uko radhi hata mkeo atembee na mtu mwenye pesa mbele ya macho yako kisa usikose misaada. Ni hivi tunataka katiba mpya yenye kubeba malengo na matakwa ya wananchi na sio ya hao matajiri wa dunia. Kama wewe na wenzako mnawaogopa hao wazungu hivyo wanawaamulia cha kupitisha kwenye nchi kaeni pembeni tuachieni sisi tusiowaogopa hao wazungu. Tutaweka kila kitu wazi kwa wananchi ni jinsi gani tunawategemea wazungu na kwanini na hatimaye wananchi watajua nini cha kufanya ili kujikwamua na utegemezi kupitia mipango mizuri tutakayojiwekea. Kwa hiyo unamaanisha hao jamaa wa huko nje ndio wanataka sisi tuwe maskini? Hiyo mikwara ya kishamba namna hiyo pelekea waoga wenzio.
Tindo sijui kama anaikumbuka hii.
 
Rudia ulichoandika uone kama kina reflect mawazo yako ya sasa.

Unadhani mimi ni mwepesi wa hivyo, angalia bandiko la mleta ni la lini, na mimi nilimjibu nini na motive behind ya mleta mada. Jitahidi kusoma paragraph yake ya mwisho ni nini alisema hakina maana. Bila kusahau ulikuwa ni mwaka wa kuelekea uchaguzi mkuu. Kisha uje useme ni wapi msimamo wangu wa kutaka katiba mpya umebadilika, kwa kisingizio chochote kile. Karibu kwa mjadala.
 
Huyu mtoa mada ana mawazo ya kimaskini maana anachokisema hakisadifu ukweli halisi
China imeendelea sana watu hao wakiwa wapi kama ni kweli kila rais anapaswa kubend kwao?

Tukubali sisi watanzania hatujapata viongozi wenye nia ya dhati kututoa hapa, wengi ni wafuasi wa vyama vyao zaidi kuliko taifa letu ndiyo maana wanapasiana vyeo tu huko hata kama uwezo wa wahusika haupo vizuri
Na sasa ni miaka 2 imepita tangu uandike hii post,sasa hivi Tanzania tuna tukio kubwa sana limetokea.

Je,bado una mawazo hayahaya au umebadilika?
 
Hii mada aliyotoa kabla hamjaikosoa jaribuni kuitafakari kwa maana ya historia ya nchi yetu na nchi nyingine hapa Afrika.
Kuna mashiko makubwa ya anachokiongea mtoa mada. Msipokubaliana nae sasa labda mtakuja tena baadae
Baadaye ndio sasa,labda kwa haya tunayopitia sasa kuondokewa na rais wetu yanaweza kuamsha ubongo wa watu
 
Back
Top Bottom