Kiungo Yaya Toure aomba msamaha Manchester City

Kiungo Yaya Toure aomba msamaha Manchester City

PAGAN

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
12,181
Reaction score
20,148
uyt.png


Kiungo wa kati wa Manchester City amesalimu amri na kumuomba msamaha wasimamizi wa klabu hiyo baada ya kutochezeshwa kwa muda na meneja wa klabu hiyo Pep Guardiola.

Kupitia taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema: "Naomba radhi - kwa niaba yangu na watu wanaoniwakilisha - wasimamizi wa timu na wote wanaofanya kazi katika klabu hii kwa sababu ya sintofahamu zilizotokea awali.

"Matamshi hayo hayawakilishi msimamo wangu kuhusu klabu au watu wanaofanya kazi katika klabu hii."

Wiki iliyopita, Guardiola aliambia wanahabari kwamba anamuhitaji Toure lakini bado anasubiri kuombwa msamaha na ajenti wa mchezaji huyo Dimitry Seluk.

Toure, 33, ameshiriki katika mechi moja kati ya mechi nane walizozicheza Manchester City msimu huu.

Baada ya kuachwa nje ya Guardiola kikosi cha wachezaji watakaocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Seluk alisema kuwa kiungo huyo wa kati ''alifedheheshwa'' na kwamba Gurdiola anafaa kumuomba msamaha iwapo City haitashinda kinyang'anyiro hicho.

Ni hapo ambapo Guardiol alijibu na kusema Toure hangecheza tena hadi ajenti huyo aombe msamaha.

''Sitakubali kama kocha kila ajenti, kwenda kwa vyombo vya habari kuwasilisha malalamiko yao iwapo mchezaji wake hajashirikishwa kwenye kikosi," Guardiola alisema.

_92251254_dc805c0d-d934-429b-8234-5264f77d318b.jpg

Chanzo: BBC
 
Hata kama ataomba msamaha, roho ya Chuki aliyonayo Pep kwa Yaya haiwezi kufutika.
 
Cant everyone let Yaya play his football in peace? Be that Drama Queen Guardiola or his stupid agent or fans or pundits! This is supposed to be a beautiful game, at the end of all this saga the one who is going to suffer is Yaya.
 
Kwanza kaomba radhi kwa manegment ya club sio kocha ndo mana hakumtaja jina lake, chezea janja wee
 
Mimi ni mmojawapo wa mwashabiki wa mpira wenye higher respect kwa Yaya Toure, nimejikuta nina mdisrespect Gurdiola kwa chuki zake dhidi ya huyu jamaa. Napaswa kumsifu Yaya kwa kuomba msamaha ingawa hakustahili kwani kuomba msamaha hakumdhoofishi wala kumshusha hadhi bali kunamuonyesha kuwa yeye ni extraordinary player. Watu wanaotaka kuabudiwa na kutukuzwa ni wale tu wanaopenda kujenga matabaka dhidi ya watu wengine kwa kujiona wao ni bora zaidi.
 
N upumbavu mkubwa kwa toure kuomba msamaha amekubali ubaguzi kwa maslahi yake sasa na gardiola alivyo mnafki na namba hatopata bora angekaza mwez wa 1 asepe timu nyingine kubwa pale uingereza akamjibu uwanjan kama etoo alivyomjibu
 
Gurdiola mshenzi sana yaan simpendi kwa ujinga wake wa ubaguzi aisee
 
Ilikuwa lazima afanye hivyo otherwise ahame
 
Combo ya Toure na Silva ina sumu kuliko hizi ambazo Guadiola anahangaika nazo. Mfano mechi ya leo na Middlesbrough long range shooter from the middle of the park could have made a difference!
 
Mimi ni mmojawapo wa mwashabiki wa mpira wenye higher respect kwa Yaya Toure, nimejikuta nina mdisrespect Gurdiola kwa chuki zake dhidi ya huyu jamaa. Napaswa kumsifu Yaya kwa kuomba msamaha ingawa hakustahili kwani kuomba msamaha hakumdhoofishi wala kumshusha hadhi bali kunamuonyesha kuwa yeye ni extraordinary player. Watu wanaotaka kuabudiwa na kutukuzwa ni wale tu wanaopenda kujenga matabaka dhidi ya watu wengine kwa kujiona wao ni bora zaidi.
Jamaa ni fundi sana, ila Pepe hamtaki hata kidogo.
 
Back
Top Bottom