Kiusalama Marehemu Mchungaji Mtikila alikuwa na cheo gani??

Kiusalama Marehemu Mchungaji Mtikila alikuwa na cheo gani??

Kwamantiki, kama viongozi wa kitaifa watatenda makosa,Sheria itafanya kazi pasipo kujali cheo Wala wadhifa wa mtu yeyote, je mtikila alipata wapi ujasiri wa kusema aliyo yasema, au anacheo ambacho raia tulikuwa hatukijui?
Tutumie akili hata kidogo na tusipende kuzusha mambo ambayo hayapo. Hivi angekuwa na cheo cha siri angetoa tena siri hadharani? Naona wengine ni watoto wadogo na mlikuwa hamjui Mtikila alikuwa mtu wa namna gani!
 
hatujazusha jambo lolote tumejaribu kuuliza kwa wenye ufahamu wa hili, labda kama hujasikia wala kutazama hiyo video hapo juu, ingekuwa vema ukatufahamisha ili tuwe na uwelewa.
 
..kumuita mhusika kituo cha Polisi kuna sheria na taratibu zake.

..pia kumkamata mtuhumiwa kuna sheria na taratibu zake.

..Lissu alipokataa kuripoti Polisi alitoa sababu za kisheria na kiutaratibu za kukataa wito.

..kwa mfano, Igp Sirro alikwenda ktk vyombo vya habari na kumtaka Lissu aripoti kituo Moshi, Kilimanjaro.

..Lissu alikuwa Dsm na alikataa wito huo kwasababu Igp Sirro hakufuata sheria wala taratibu za kumuita kituoni.
ufahamu wa sheria ni jambo moja hasa kwenye haya mataifa yetu ya kiafrika lakini nimuhimu sana kuwa na weledi huo wa kisheria, lisu kwakweli Mungu ampe maisha marefu wengine tunajifunza kutoka kwake
 
Mkuu haya mambo Huwa yanafikirisha Sana, inawezekana ikawa uko sahihi kwamba anaweza akaitwa akaenda lakini wakati mwingine wanaitwa na hawaendi mfano TUNDU LISU juzi tu aliitwa na akasema haendi
Inategemea, kuna wakati mtu anaitiwa ujinga na kikubwa kumpotezea muda, hii hakuna kwenda.
 
hatujazusha jambo lolote tumejaribu kuuliza kwa wenye ufahamu wa hili, labda kama hujasikia wala kutazama hiyo video hapo juu, ingekuwa vema ukatufahamisha ili tuwe na uwelewa.
Hiyo video ni siku nyingi na nilishaiona wakati hili tukio lilipotokea. Kama umesikiliza vizuri utakuwa umesikia Mtikila alivyosema kuwa yeye ni kiongozi wa kitaifa na huyo polisi hana mamlaka ya kumkamata halafu watu wakacheka. Mtikila alikuwa ni mtu wa kujiamini sana sana na alikuwa anajua kucheza na saikolojia za polisi na viongozi wa CCM. Alipokuwa anakaa zile flats za Ilala, kuna siku alikuwa anatoka nyumbani asubuhi kwenda kwenye shughuli zake, kumbe watu wa usalama wa taifa walikuwa wamebana sehemu wanamfutilia, wakiwa na pikipiki (wakati huo kulikuwa hamna hizi pikipiki za mchina). Kumbe wasaidizi wa Mtikila nao walikuwa nyuma ya yule mtu wa usalama wa taifa na kamera yao. Walichukuwa picha jinsi alibana sehemu kusubiri Mtikila aingie kwenye gari na kila hatua anavyomfutilia na pikipiki yake, wakapiga picha na kuja kuchapisha kwenye gazeti. (social media zilikuwa hazijaenea kama sasa). Asubuhi tunaamka tukakutana na hizo picha kwenye gazeti. Huyo huyo Mtikila kuna siku alionyeshwa kitambulisho na mtu wa usalama ili amkamate. Mtikila akamwambie wewe ni mtu wa usalama wa chama cha majambazi na siyo taifa. Huyo ndiyo alikuwa Mtikila.
 
Ukiisikiliza sauti katika video Kuna maneno mchungaji anayasema, Kwa cheo chako huna mamlaka ya kunikamata, akisisitiza Kwani we hujui?

View attachment 3084950
Mwenyekiti wa Chama cha siasa kilichosajiliwa anakamatwa na askari mwenye level ya ofisa mwenye nyota kuanzia inspector na sio constable wa polisi mbavu mbili au tatu!.
Watanzania wengi hawajui haki zao, polisi hawezi kukukamata bila arrest warranty.
P
 
p
P
Hapo P umesema kutokuelewa kunachangia
 
Mwenyekiti wa Chama cha siasa kilichosajiliwa anakamatwa na askari mwenye level ya ofisa mwenye nyota kuanzia inspector na sio constable wa polisi mbavu mbili au tatu!.
Watanzania wengi hawajui haki zao, polisi hawezi kukukamata bila arrest warranty.
P
Asante kwa kuwafundisha vijana wetu
 
Kipo bhana kwenye CPA
Leta hicho kifungu usiseme tu kipo kwenye CPA, mimi nimeweka kifungi kinachomruhusu askari wa cheo chochote kuhoji, na wewe weka hicho kifungu kinacho zuia.
Ili unifundishe
 
Back
Top Bottom