Kivuli cha Hayati Mwalimu Nyerere kinawatisha

Wimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
866
Reaction score
625
Shida ya watanzania kupewa Katiba Mpya ni hofu ya kuuvunja Muungano wa Nyerere ambao kimsingi Muungano huo haupo kila Rais ajaye anaogopa kivuli cha Nyerere.

Na kwa sababu hiyo Tanzania inarudishwa nyuma. Sikutegemea kama aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba naye angeona kuwa si wakati muafaka.
 
🤣🤣🤣
 


Katina mpya ??!!
 
Katiba mpya itakuwa nzuri kama ikidaiwa na wanainchi wenyewe kupitia asasi za kiraia ila sio vyama vya siasa ambavyo wao wanajali maslahi yao na vyeo zaidi kuliko maslahi ya wananchi.

Hivi sasa vyama vya siasa vimegeuza katiba mpya kama ndio agenda yao, na sio agenda ya wananchi tena, wananchi wengi hawana habari na katiba mpya wao wanapambana na makali ya maisha, swali la kujiuliza je katiba mpya ikija itapunguza ugumu wa maisha kwa mtanzania? Na kama ndivyo ni vipengele vipi hivyo vitachagiza hilo? Kwa nini visiwekwe kwenye katiba hii iliyopo tukasonga mbele..

Katiba mpya inaweza kuwa ni muhimu ila bado wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha nini hasa kipo humo kwenye katiba mpya, makundi kama ya wakulima na wafugaji ndio kabisa sijui hata kama maslahi yao yameelezwa kwenye katiba. Isije ikawa ni katiba inayobeba agenda za kisiasa zaidi kuliko agenda za maendeleo ya wananchi. Elimu ya kutosha inahitajika kabla ya kuanza kudai katiba mpya.
 
kuna wasiwasi kwamba endapo Zanzibar itapewa mamlaka kamili kama nchi ndani ya Muungano wa nchi mbili basi huenda huko mbele Zanzibar wakapata Rais ambaye ataifanya Zanzibar kujiunga ama kuingia mikataba ambayo itaathiri Tanzania bara ki ulinzi na usalama.

Kumbukeni sakata na Zanzibar kujiunga na OAC miaka ya nyuma.
 
Hujui hata unachoandika,OAC ndiyo nini!?..hiyo athari ya usalama kwa Uganda iliyojiungaOAC(OIC) ni ipi!?..ni hofu/chuki dhidi ya uislam mliyojijengea kwa vizazi
 
Hujui hata unachoandika,OAC ndiyo nini!?..hiyo athari ya usalama kwa Uganda iliyojiungaOAC(OIC) ni ipi!?..ni hofu/chuki dhidi ya uislam mliyojijengea kwa vizazi
ushaelewa ndiyo maana ume-comment, CCM haiwezi kuiacha Zazibar ikapata mamlaka kamili ya kidola, huo ndiyo wasiwasi wao na ndiyo maana katiba pendekezwa ya Jaji Warioba ikaishia kabatini.
 
Ukivunja muungano Zanzibar haitaweza hata kulipa mishahara yake yenyewe achana kabisa na maendeleo
 
ushaelewa ndiyo maana ume-comment, CCM haiwezi kuiacha Zazibar ikapata mamlaka kamili ya kidola, huo ndiyo wasiwasi wao na ndiyo maana katiba pendekezwa ya Jaji Warioba ikaishia kabatini.
Siyo ccm,Bali Dola..na sababu anazo lukuvi,kamuulize
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…