Kivuli cha Kwame Nkrumah katika TANU

Mkuu, hili chapisho ulikuwa umewahi kulisoma hapo kabla ??? Mimi ninayo nakala ngumu (Hard Copy) ambayo ilichapishwa mwaka 1973. Soma hicho kitabu, taarifa kuhusu Chief Edward zipo. Tena waandishi wanaenda mbali zaidi kuweka hadi Exchange of Notes ambazo Sultani wa Zanzibar baada ya mkutano wa Berlin analalamika kwa Uingereza na Ujerumani akidai kwamba Aruscha (Arusha) na maeneo mengine ya Uchagani yalikuwa ni mali ya Zanzibar (Under Zanzibar Suzerain), hivyo angehusishwa kwenye ule mkutano.

Mkuu, umeniambia kwa ujasiri kabisa kwamba umesoma maandiko yote kuhusu Tanganyika. Lakini kwanini taarifa muhimu kama hizi kuhusu Tanganyika zikupite ???
 
Gaddafi alianza vizuri na alipata heshima kubwa Libya, laiti angekubali kukubaliana na mabadiliko ya dunia na kuacha demkrasia ichukue mkondo wake angebaki kuwa baba wa Taifa la Libya na heshima zote.
 
Mkuu Mohamed,
Earl Seaton na Sosthenes Mality walikuwa ndiyo wanaongoza kitengo cha tafiti wizara ya mambo ya nje ya Tanganyika kipindi cha awamu ya kwanza. Walijitahidi kuandaa nyaraka nyingi kuhusu Tanganyika hata kabla ya ukoloni. Lakini pia baada ya uhuru kuna machapisho yalikuwa yanaandaliwa na wizara ya mambo ya nje yaliitwa TANZANIA TREATY SERIES, ambayo yanatoa taarifa nyingi sana kuhusu Tanganyika, Zanzibar na Tanzania.

Nadhani ufanye kuyatafuta kwa watu wa mambo ya nje , kama bado yatakuwepo salama..
 
Malcom...
Kweli nimesoma mengi lakini taarifa hii sikupata kusoma kokote lazima nikwambie ukweli.
Ndiyo maana nikaingia kutafuta hizi taarifa.

Hizi ni taarifa muhimu sana.

Hata John Iliffe ambae ndiye bingwa wa historia ya Tanzania hakuna popote amegusia hata kwa mbali.

Nakushukuru sana.

Ikiwa si taklif kwako nitashukuru kupata screen shots za vipande muhimu hasa hivyo muhimu vya kudai uhuru ingawa sijui ingewezekanaje maana zipi zile Article 26 na 27 za Mandate Territory ambazo Seaton alikuwa bingwa na anazijua fika.

Nitakachofaya nitawasiliana na jamaa zangu Zanzibar Archives nione kama kuna lolote kuhusu Sultan katika kadhia hii.

Nitakachopata nitakiweka hapa In Shaa Alah.
 
Shukrani, nitajitahidi....
 
Gold...
Kwangu kuniita ''Wewe'' si adabu akina mama wanawafunza watoto wao adabu.
Sitaki kuamini kuwa wewe hukufunzwa adabu kwenu.

Usiwatukanishe wazee wako.
Kuniiita ''Mzee,'' hakika mimi ni mzee nina miaka 70.

Hujakosea.
Uzee ndiyo cheo changu.

Huu ni mjadala tu wala hapa si mahali pa kuvunjiana heshima.
Ungeweza ukasema na ingependeza,''Mzee unajuridia...''

Ungeeleweka na ingependeza.
Hakuna sababu ya wewe kuja hapa umeghadhibika na kutukana.

Unadhani mimi najishusha hadhi kwa kuandika historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika?

Inawezekana vipi mimi kuwaeleza Watanzania mchango wa wazee wangu katika kupigania uhuru wa Tanganyika liwe jambo la kunivunjia heshima?

Kitabu changu kina ''credibility'' kubwa sana labda kama wewe hufahamu.
Tunakwenda toleo la tano toleo moja baada ya lingine matoleo yakifukuzana.

Unajua kama Sykes wako katika Dictionary of African Biograpahy na mimi ndiyo niliyopewa kazi ya kuwaandika?

Haikushangazi kuwa Sykes hawako katika kitabu cha historia ya TANU cha Chuo Cha CCM Cha Kivukoni lakini wako katika Dictionary of African Biography?

Huu ulikuwa mradi wa Harvard na Oxford University Press, New York.

 
Mzee,
Nimepata shauku, andiko la Nguruvi linatakiwa kudhibitishwa.
Kwa ufahamo wako, ni kweli kuwa Ally Sykes hakuwai toa hutuba yoyote ya kudai uhuru nje ya Mwembe Togwa au nje ya Dar esam Salaam?
James Comey, unajua hoja nzima hapa ni kutaka kuonyesha jambo kuhusu Nyerere

Mada ya katiba imekuja mahususi kwasababu tumewahi kujadiliana na Mo na kumwambia aliyeandika katiba ya TANU ni Julius Kambarage Nyerere wa Butiama.

Ukisoma bandiko lake, Mo anasisitiza kuwa katiba imenukuliwa neno kwa neno kutoka Ghana.
Tukubaliane naye kwa hilo, swali linabaki nani alinukuu katiba hiyo? hapa hatakueleza

Kumbuka kuanzia 1929 Mwalimu Cecil Matola na Kleist wakiasisi chama , na hapa Cecil ndiye chair hadi mapinduzi yaliyofuatia ya akina Abdul na hadi Abdul anagaragazwa na Mwalimu Nyerere pale Anatouglo hakuna kitu kilichoitwa katiba, iwe ya page 1 au kunukuu kutoka South Africa

Hapa haina maana Nyerere alianzisha harakati, la hasha, wakati anazaliwa shughuli za siasa zilishaanza. Wakati anakuja Dar alikuwa na taarifa za uwepo wa chama ukizingatia alikuwa kiongozi Makerere , alikuwa kiongozi Tawi la Tabora, alikuwa Msomi wa kweli

Kazi ya Mo ni moja kutafuta kila hiyana kumdunisha, kumzodoa Mwalimu n.k.

Mada hapo juu imekuja mahususi kuonyesha kwamba Nyerere hakuandika katiba
Well, tuonyeshe ya Abdul Sykes ya kunukuu! kutoka popote , iwe nusu ukurasa au mstari mmoja

Nyerere atakuwa Nyerere na ndiye Rais wa Tanganyika.

Tunawashukuru sana sana wazee wetu wakiwemo akina Abdul Sykes kwa kazi zao zilizotufanya tuwe Taifa kama leo. Hata kama Abdul hakuwahi kuwa katibu kata, kazi zake na wenzake ni za kutukuka na ziheshimiwe
 
MS,
Nashukuru, ninazidi kuelewa utofauti wa Julius Nyerere na viongozi wengine wa TANU. Kiufupi iwe TAA iwe TANU Nyerere ndiye aliipeleka mikoani. Na hii ndiyo hoja ninayoiona ya Nguruvi ambayo anaipia chapuo kuwa kwanini maelezo yako mengi huwa yanatukuza "wazee wako" mara nyingi kuliko wazee wote waliopigania nchi?
 
Mimi ni mpenzi wa kufuatilia historia na huwa napenda eye witness hasa ktk historia ya kudai uhuru wa Tanganyika.
Huwa naonaga mambo mengi yanajadiliwa humu wakati watu kama Maria Nyerere na wengine ambao walikuwa karibu na Nyerere wangeweza kuyatolea ufafanuzi.

Bado naamini kuwa Nyerere alikuwa nanuwezo mkubwa wa kuandika katiba ya TANU pasi na kukopi ya CPP. Ama idhibitishwe vinginevyo.

Kwangu naona hoja nyepesi kutoka kwa mzee MS kuamini kuwa hiyo katika ilikopiwa neno kwa neno kwa kuogopa kubatilishwa na British Colonial Government. Kwamba TANU ilikosa utashi kitu ambacho kinaacha maswali mengi kuliko majibu.
 
Usharejesha ufidhuli tayari. Hakuna tatizo

Mjibu James Comey hoja yake. Ni wapi na lini AbdulWahid Kleist Sykes Mbuwane aliwahi kuhutubia mkutano wa kuimarisha chama au kudai uhuru nje ya eneo la Mwembe Togwa!
Nguruvi...
(Cecil Matola alifariki 1933 nna nafasi yake ikashikwa na Mzee bin Sudi).

Hilo swali nimelijibu.
Na si leo.

Abdul Sykes umuhimu wake hauko katika kuhutubia mikutano.

Umuhimu wake upo kuwa baba yake Kleist Sykes ndiye aliyekutana na Dr. Kwegyr Aggrey 1924 na Dr. Aggrey akampa wazo la kuunda African Association (AA) 1924.

Kleist akaunda AA 1929.

Ili kutenganisha maslahi ya Waislam katika AA akaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Muslim Association) 1933 akiwa Secretary na Mzee bin Sudi akiwa Rais.

Lakini juu ya juhudi hizi ilibakia kuwa tabu kuweka pembeni ushawishi wa Waislam katika siasa za Dar es Salaam ya miaka ile.

Wawili hawa walikuwa President na Secretary katika AA.

Abdul Sykes alipochukua uongozi wa TAA na Dr. Kyaruzi 1950 iliundwa TAA Political Subcommittee na katika wajumbe wa kamati hii alikuwamo Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir.

Hii kamati ndiyo ilijenga msingi wa kuunda TANU 1954 baada ya Julius Nyerere kuingizwa katika uongozi wa TAA baada ya uchaguzi kati yake na Abdul Sykes April 1953.

Lakini kubwa katika mkadama huu ni kuwa haya niliyoandika hapa yote yalikuwa katika mswada wa kitabu alioandika Kleist Sykes kabla hajafa 1949.

Mswada huu ni sura katika kitabu alichohariri John Iliffe, "Modern Tanzanians," "Kleist Sykes The Townsman."

Sasa historia ya TANU inaanza na mswada huu wa Kleist.

Kuanzian1949 baada ya kifo cha Kleist Sykes utaisoma historia ya TAA hadi kuundwa kwa TANU kutoka kwa Abdul na Ally Sykes kwa ushahidi wa nyaraka, picha na shajara.

Hapa ndipo utakapokutana na Julius Nyerere alivyopokelewa na Abdul Sykes 1952.

Waliokuja kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika haya hawakuyataka.

Hawakuitaka historia kutoka 1954 rudi nyuma hadi 1924.

Ikawa mwiko kuwataja wazalendo wa miaka hiyo.

Si hili tu.

Hata hapo walipotaka kuanzia wao mengi muhimu katika historia ya TANU hawakuyataka pia.

Watu wakaamini kuwa historia ya TANU ni hiyo waliyoikuta.

Hapo ndipo mimi nilipoamua kuandika "...The Untold Story..."

Duru za African History katika vyuo vingi walishangazwa na waliyosoma katika kitabu changu.

Historia hii ya Abdul Sykes, nduguze na baba yao na wenzake wa nyakati zile na wazalendo wengine Dar-es-Salaam na majimboni ndiyo muhimu kwangu sio kama Kleist Sykes au mwanae Abdul alikwea jukwaa kufanya mkutano wa hadhara.

Atakae mjadala na mimi tujadili haya kwa nini historia hii ilifutwa na kwa nini leo kila mtu anataka kuijuwa?

 
James...
Nyerere hakuipeleka TAA wala TANU majimboni.

Nimeeleza katika kitabu cha Abdul Sykes vipi TAA ilienezwa majimboni toka ilipoundwa 1929 hadi kufikia 1950 ulipokuja mwamko mpya.

Unaijua historia ya Ali Migeyo?
Salum Mpunga?
Msham Awadhi?
Hamisi Heri?
Mama bint Mwalimu?
Bi. Chiku bint Said Kisusa?
Bi. Mwamtoro bint Chuma?


Salum Mpunga

Soma kitabu.
Usichangie kwa dhana.

Hawa wazee wangu mchango wao hauna mfanowe.

Soma historia ya Schneider Abdillah Plantan kwanza katika jeshi la Wajerumani Vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914-1918) kisha soma historia yake katika TAA na TANU 1950 - 1961 uhuru ulipopatikana.

Soma kitabu.
Ndiyo maana kitabu hiki haijapata kutokea kinakwenda toleo la tano kuanzia 1998.
 
James...
Hakuna tatizo.

Una haki na uhuru wa kuamini utakacho.

Watu wameamini makubwa kupita hayo uliyosema.

Mimi hapa naeleza niyajuayo sikulazimishi kuniamini.

Mimi muhimu kwangu ni wewe usome tu historia hii ambayo hukupatapo kuisoma popote.

Natosheka na hili.

Angalia taarifa za Special Branch hapo chini:

 
Nguruvi...
(Cecil Matola alifariki 1933 nna nafasi yake ikashikwa na Mzee bin Sudi).
Kufariki 1933 haimaanisha Mwalim Cecil hakuwa M/kiti na muasisi 1929
Abdul Sykes umuhimu wake hauko katika kuhutubia mikutano.
Kuntu! Abdul hakuwahi, Nyerere alisambaza TANU kupitia mikutano ya siasa.
Nafasi ya Mwalim Cecil ipo wapi?
Abdul Sykes alipochukua uongozi wa TAA na Dr. Kyaruzi 1950 iliundwa TAA Political Subcommittee na katika wajumbe wa kamati hii alikuwamo Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir.
Hata sijui kwanini Abdul kaingia hapa! Just to make him relevant? OK tukubaliane na hilo
Hii kamati ndiyo ilijenga msingi wa kuunda TANU 1954 baada ya Julius Nyerere kuingizwa katika uongozi wa TAA baada ya uchaguzi kati yake na Abdul Sykes April 1953.
Nyerere hakuingizwa, aliingia kwa kumshinda Abdul na aliingia katika uongozi si katika chama
Nyerere alikuwa katibu wa Tawi Tabora, alihudhuria mkutano wa chama 1948
Hapa ndipo utakapokutana na Julius Nyerere alivyopokelewa na Abdul Sykes 1952.
Not true Mo! sijui kwanini unarudia huu uongo! ni uongo kwasababu Nyerere alikuwa katibu wa Tawi la Tabora na 1948 alihudhuria mkutano wa chama.

Hapo akiwa katibu wa Tawi kubwa nchini alikutana na viongozi wa makao makuu akiwemo Abdul.

Kwamba Abdul alimpokea unataka kuuaminisha umma alimuingiza, alimfundisha siasa n.k.

Ukiacha kuwa Abdul alikuwa 'Townsman'' , kwa elimu na kufunguka katika mambo ya kimataifa hasa akiwa masomoni Edimburgh Nyerere alikuwa mbali sana

Abdul hakuwa na chochote cha kumfunza ukiachilia zile connections tu za mjini na uenyeji.

Ni kwa msingi huo Nyerere alipopata uongozi kitu cha kwanza ni kuandika katiba.
Iwe aliandika au kunukuu si hoja , hoja ni kwamba alitambua chama hakiendeshwi kama Familia na wala hakiendi kama Mtumbwi wa Tanga, chama lazima kiwe na utaratibu.

Uwezo wa Nyerere ulimfanya afike sehemu za nchi kuitangaza TANU kwa mafanikio.
Nyerere alitambua Tanganyika ni zaidi ya kidongo chekundu, Kipata na Mwembe Togwa

Katiba na mikutano ni mambo ambayo AbdulWahid Sykes na Kleist Sykes hawakufanikiwa kuyafanya. Mohamed hili si kosa kila kitu kina wakti wake.

Kosa ni kuficha ukweli kwa kumzodoa Nyerere au kumdunisha kama ulivyoleta mada ya katiba.

Well, aandike, aazime, anukuu afanye chochote ukweli utabaki pale pale ni Nyerere aliyefanya hivyo, si Abdu au Kleist. Ni muhimu ingawa ni ngumu 'kumesa' kwa mashabiki

Abdul na Wazee wengine walifanya kilicholingana na uwezo wao na hakika ulikuwa msingi mkubwa wa siasa za nchi, lakini si wao peke yao.
Mchango wa Mwana wa Butiama hauhitaji parapanda, Julius anatetewa na historia
Historia hii ya Abdul Sykes, nduguze na baba yao na wenzake wa nyakati zile na wazalendo wengine Dar-es-Salaam na majimboni ndiyo muhimu kwangu sio kama Kleist Sykes au mwanae Abdul alikwea jukwaa kufanya mkutano wa hadhara.
Hili imefika mwisho! nashukuru tumeelewana na James Comey atakuwa amepata jibu.
 
Nguruvi...
Nimekueleza kuwa Cecil Matola kafariki 1933 kukufahamisha kuwa hakuishi hadi 1950 pale Abdul na Hamza Mwapachu walipompindua Thomas Plantan aliyekuwa President wa TAA na Clement Mohamed Mtamila Secretary.

Ungejuaje kuwa Cecil Matola ndiye alikuwa rais muasisi kama Kleist Sykes asingeandika mswada wa kitabu cha maisha yake na kueleza vipi aliunda African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?

Waasisi wa AA ni hawa wafuatao: Cecil Matola, Kleist Sykes, Selemani Majisu, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Rawson Watt na Raikes Kusi.

Kleist Sykes anaeleza kwa nini Waislam walikuwa wengi katika AA.
Anasema kanisa lilikuwa linawakataza waumini wao kujihusisha na siasa.

Haya utayapata katika ''seminar paper,'' iliyoandikwa Aisha Daisy Sykes, University of East Africa Dar es Salaam Campus 1968.

Daisy aliandika mada hii kwa msaada wa baba yake Abdulwahid Sykes, kutokana na muswada ulioandikwa na Kleist Sykes.

Angalia A.D. Sykes, ''The Life of Kleist Sykes,'' University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15).

Habari nyingine kuhusu Al Jamiatul Islamiyya zinatokana na mswada ulioandikwa na Tewa Said Tewa, ''A Probe Into the History of Islam in Tanganyika.''

Taarifa nyingine zinatokana na maelezo ya Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika miaka ya mwanzo ya 1940.

Naamini James Comey ataelewa tofauti baina yako na mimi.
Wewe unaandika kwa dhana.

Mohamed Said anaandika kutokana na utafiti.

Hakika Mwalimu aliisambaza TANU katika mikutano ya siasa.
Hebu msome Daisy anasema nini kuhusu hii mikutano:

''Nimesikia mazungumzo mengi wakati baba na wenzake walipokuwa wakijadili majina na shughuli ambazo hawa akina mama walikuwa wahusishwe ili kuleta mvuto wa kisiasa katika mikutano yao ya TANU.''

Hii mikutano ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes na Nyerere akihudhuria pamoja na kamati ya ndani ya TANU ya Mzee Rupia, Dossa Aziz, Bi. Titi Mohamed, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Hawa Maftah kwa kuwataja wachache.

Naamini James Comey ataelewa tofauti baina yako na mimi katika historia hii.
Wewe unaandika kwa dhana.

Mohamed Said licha ya kutafiti na kuandika kitabu ni sehemu ya historia hii.

Baba yangu alimjua Nyerere nyumbani kwa Abdul Syes na haya yote kayashuhudia kwa macho yake.

Ndiyo siku zote akisema vipi hawa wataandika historia ya TANU wasimtaje Abdul Sykes?
Nani anaeficha ukweli huu?

Hakika si Mohamed Said.
Nyerere anaujua mchango wa Abdul Sykes.

Msikilize Daisy:

''Juma moja kabla ya kifo chake nilimuuliza baba swali ambalo jibu alilijua lakini katika hulka yake ya kawaida ya kutopenda kujikweza hakutaka achukue sifa zote kwa ule ukweli na matokeo yake.

Wakati ule nilikuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki Dar - es- Salaam na mwalimu wangu wa Historia Dr. John Iliffe kwa kutambua kuwa natoka familia ya Sykes waasisi wa mwamko wa siasa katika Tanganyika na mchango wa wazee wangu katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika alinitaka niandike mafanikio ya Watanganyika wa kizazi kile pamoja na historia ya babu yangu Abdallah Kleist Sykes.

Dk. John Iliffe alinitia moyo nifanye utafiti na kuandika historia hii na nilikubali kufanya hivyo.

Nilikuwa na swali kuhusu nani khasa walikuwapo katika mkutano na kushiriki wa kuibadili TAA kuwa TANU.

Baba akashauri kuwa tuombe miadi na Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere ili anipe ukweli niliokuwa nautafuta na kusadikisha mambo mengine yanayohusiana na historia hiyo.

Hivyo tukaenda Msasani kuonana na Mwalimu Jumamosi moja asubuhi.

Kama ilivyotegemewa Mwalimu alifurahi sana kutuona maana ilikuwa muda mrefu watu hawa waliokuwa marafiki wakubwa sana kupata kuonana.

Mwalimu alitoa ushirikiano mkubwa sana kwangu kupata ukweli kutoka kwake katika yale niliyotaka kujua kutoka kwake.

Hii ndiyo ilikuwa siku yao ya mwisho kuonana.''

Naamini James Comey ataelewa tofauti baina yako na mimi katika historia hii.
Wewe unaandika kwa dhana.

Wewe hutujui sisi.

''Wastara haumbuki.
Wa mbili havai moja.''

Ningeweza kukueleza mengi lakini nachelea kukuchosha na kuwachosha wasomaji wengine.

Picha hiyo hapo chini ni Daisy na Mohamed Said

 
Bwana James...
Hayo hapo chini ni kutoka kitabu cha Abdul Sykes:

''Tabora ilianza kushiriki katika siasa mwaka 1945 wakati African Association ilipoingizwa mjini Tabora kutoka Dodoma kutokana na juhudi za Edward Mwangosi.

Tabora kwenyewe msukumo wa kuanzisha chama cha Waafrika zilitoka Combine Dancing Club, kilabu kilichoanzishwa na vijana wa pale mjini kwa ajili ya kujifurahisha.

Wanachama mashuhuri wa kilabu hiyo walikuwa ndugu wawili Wamanyema - Maulid na Abdallah Kivuruga, Chamngíanda Usingizi, Ramadhani Nasibu, Rashid Mussa, Issa Kibira, Hamis Wabeba, Mwinyi Khatib Hemed, Swedi Juma, Issa Hamis Pama na Rajab Kanyama.

Wanachama wengi wa kilabu hii walikuwa Wamanyema, kizazi cha pili baba zao wakiwa wametokea ile iliyokuwa wakati huo Belgian Congo, wakafanya maskani Kigoma, Ujiji na Tabora mwishoni mwa karne ya kumi na tisa.

Wamanyema likiwa kabila la Waislam watupu ilikuwa rahisi kuungana kama kikundi cha kabila moja na kuanzisha chama cha siasa.

Kwa hiyo Combine Dancing Club kidogo kidogo ilijigeuza kutoka chama cha starehe na kuwa chama cha siasa.

Kumbukumbu za kikoloni zinaonyesha kwamba kamati ndogo ndani ya kilabu iliundwa katika mwaka 1945, Mwinyi Khatibu Hemed, Mzigua kutoka Bweni, Pangani, akiwa katibu.

Hemed aliandika barua makao makuu ya African Association mjini Dar es Salaam kuujulisha uongozi ju ya dhamira ya kufungua tawi mjini Tabora.

Tarehe 3 Machi, 1945 African Association mjini Tabora ilifungua ofisi yake ikiwa na na viongozi wafuatao: Hamisi Simbe (Rais), Ramadhani Nasibu (Makamu wa Rais), M. K. Hemed (katibu), Chamng'anda Usingizi (Mwenyekiti), Fimbo Mtwana (Mweka Hazina) na Rashidi Mussa (Mkaguzi wa Hesabu).

African Association, kama ilivyokuwa asili ya kilabu iliyotokana nayo, ilishikwa na Wamanyema.
Hivyo ndivyo Wamanyema walivyokuja kuongoza siasa Tanganyika.

Julius Nyerere, wakati huo akifundisha St. Maryís School, alishuhudia sherehe za uzinduzi wa African Association.

Nyerere hakutambua hata kidogo wakati huo kuwa alikuwa akishuhudia sehemu ya historia yake mwenyewe ikijifungua mbele ya macho yake.

Mwaka 1946 wasomi wa Makerere walianza kujishughulisha na African Association pale Hamza Mwapachu na Julius Nyerere walipochaguliwa Katibu na Katibu Msaidizi na nafasi nyingine za uongozi zikishikwa na Wamanyema.

Baada ya uhamisho wa Mwapachu kutoka Tabora, Nyerere akashika nafasi yake na kuwa katibu wa chama.

Mwaka huo huo Nyerere alisafiri kwenda Dar es Salaam kama mjumbe wa Tabora kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa African Association.

Katika mkutano huu ndiyo kwa mara ya kwanza Dossa Aziz alimtia Nyerere machoni.

Lakini urafiki baina ya Dossa na Nyerere haukushamiri hadi mwaka 1952, Nyerere alipokuja Dar es Salaam na kuungana na wazalendo wengine.''

Bwana James...
Hali ya siasa kote majimboni ilikuwa hivi.

Hakutoka mtu TANU New Street kupeleka chama cha TANU majimboni.
TAA ilikuwapo na wanachama wake na matawi haya ndiyo yakaja kuwa matawi ya TANU.

Dodoma alikuwapo Hassan Suleiman na Juma Ponda.
Lindi alikuwapo Suleiman Masudi Mnonji.

Tanga alikuwapo Mwalimu Kihere.
Moshi alikuwa Joseph Kimalando.

Mwanza alikuwapo Paul Bomani.
Kwa kuwataja wachache.

Dar es Salaam New Street alikuwapo Abdul Sykes na Hamza Mwapachu.
Na baba yake Abdul ndiye muasisi wa chama hiki.

Imekuwaje historia hii ikageuzwa?


Abdallah Kivuruga

 
Mzee,
Aya ya tatu inaweza upeleka huu mjadala kwingine. Hai swii kuandika maneno kama hayo kwa muandishi makini kama wewe. Hapa mtu anaweza sema unamfananisha Nyerere na wazee wako na ukamuona Nyerere hafiki ktk viwango vya hao wazee wako.
Hapo mjadala utakuwa mwingine.

Kusema Nyerere hakuipeleka TANU majimboni pia kunaweza kujadiliwa.

Huo mwamko unaouzungumzia kuanzia 1952 kwa nini haukutokea kabla ya Nyerere kuwa mwenyekiti TANU?

Sikatai kuwa kuna wazee wa makabila mbalimbali (hata wazee wangu) wameshiriki katika Uhuru wa Tanganyika lakini ukisema "Mfanowe hakuna" hapa panaleta shida.
 
Nashukuru, majibu nimepata mengi kuliko nilivyofikiri mwanzo.

Napenda kujifunza, na hapa nimepata kitu. Nimepata kuishi Dar es Salaam kwa miaka kadhaa na hizi kauli za kuwa wazee wa DSM ndo wamemfundisha Nyerere kuvaa suruali na kumfundisha siasa ni story za muda mrefu saana zikiwa na lengo la kumlinganisha au kumdunisha Nyerere.

Lakini kupitia mjadala huu nimejua kuwa kuvaa kampura ilikuwa ni majukumu ya kikazi ya kikoloni.

Pia, kuhusu siasa, Nyerere alianza muda mrefu na hata kuaminika kuongoza tawi Tabora na si baada ya kuja Pugu sekondari.
 
James...
Nitakuondolea hiyo shida yako.
Hebu soma hii hapo chini:

''Kitabu kilikuwa kimetoka na siku hiyo nilikwenda nyumbani kwa Mama Daisy kumpa nakala yake ya kitabu.

Tulikuwa tumekaa kwenye varanda yake nyumba yake Barabara ya Ali Hassan Mwinyi iliyokuwa mkabala na Hellenic Club.

Alikipokea kitabu akawa anatazama picha ya mumewe kwenye jalada na akawa kimya kwa muda mrefu.

Bila shaka alikuwa anawaza maisha aliyoishi na baba yetu wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950.

Mama Daisy alikuwa shoga wa marehemu mama yangu Bi. Baya bint Mohamed na nyumba zao hazikuwa mbali kwani sisi tulikuwa Mtaa wa Kipata na si mbali na Mtaa wa Stanley.

Nyumba zao zilitenganishwa na Mtaa wa Kitchwele (sasa Uhuru Street).

Naamini kuwa ile mimi mtoto wa shoga yake kuwa ndiye niliyekuja kuandika kitabu cha Abdul Sykes, mtu ambae historia ilikuwa imemfuta bila shaka fikra hii ilikuwa ikizunguka katika kichwa chake.

''Mwanangu Mohamed, baba yako alijitolea sana katika kupigania uhuru wa Tanganyika,'' Mama Daisy alianza kusema.

''Alikuwa na sanduku akiweka fedha zake na kila TANU wakija hapa kutaka kile au hiki yeye alikuwa anaingia ndani analifungua lile sanduku anatoa fedha kuwapa alikuwa hawarudishi mikono mitupu.

Mimi nikawa namwambia, ''Bwana Abdul taratibu lakini hakunisikia, hakuacha kutoa fedha kwa ajili ya chama chake.

Bwana Abdul alikuwa mtu karimu sana.''

Bwana James,
Haikushagazi kuwa Abdul Sykes hayuko katika historia ya kupigania uhuru?
Hebu nipe jibu.


Abdul Sykes na mkewe Mama Daisy Government House katika Garden Party 1950s
 
James...
Ikiwa una ushahidi kuwa Nyerere aliipeleka TANU majimboni uweke hapa kwani sote tunajifunza.

Unazungumzia yaliyotokea mwaka wa 1952 sawa nashangaa kwa nini hujiulizi iweje TANU iundwe nyumbani kwa Abdul Sykes.

Kwa nini TANU haikuundwa mji mwingine wowote majimboni?

Kwa nini kadi ya Ally na Abdul Sykes ni no. 2 na 3 na kadi 1000 za mwanzo kanunua Ally Sykes kutoka mfukoni kwake.

Au hukuwa unayajua haya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…