Kufariki 1933 haimaanisha Mwalim Cecil hakuwa M/kiti na muasisi 1929
Kuntu! Abdul hakuwahi, Nyerere alisambaza TANU kupitia mikutano ya siasa.
Nafasi ya Mwalim Cecil ipo wapi?
Hata sijui kwanini Abdul kaingia hapa! Just to make him relevant? OK tukubaliane na hilo
Nyerere hakuingizwa, aliingia kwa kumshinda Abdul na aliingia katika uongozi si katika chama
Nyerere alikuwa katibu wa Tawi Tabora, alihudhuria mkutano wa chama 1948
Not true Mo! sijui kwanini unarudia huu uongo! ni uongo kwasababu Nyerere alikuwa katibu wa Tawi la Tabora na 1948 alihudhuria mkutano wa chama.
Hapo akiwa katibu wa Tawi kubwa nchini alikutana na viongozi wa makao makuu akiwemo Abdul.
Kwamba Abdul alimpokea unataka kuuaminisha umma alimuingiza, alimfundisha siasa n.k.
Ukiacha kuwa Abdul alikuwa 'Townsman'' , kwa elimu na kufunguka katika mambo ya kimataifa hasa akiwa masomoni Edimburgh Nyerere alikuwa mbali sana
Abdul hakuwa na chochote cha kumfunza ukiachilia zile connections tu za mjini na uenyeji.
Ni kwa msingi huo Nyerere alipopata uongozi kitu cha kwanza ni kuandika katiba.
Iwe aliandika au kunukuu si hoja , hoja ni kwamba alitambua chama hakiendeshwi kama Familia na wala hakiendi kama Mtumbwi wa Tanga, chama lazima kiwe na utaratibu.
Uwezo wa Nyerere ulimfanya afike sehemu za nchi kuitangaza TANU kwa mafanikio.
Nyerere alitambua Tanganyika ni zaidi ya kidongo chekundu, Kipata na Mwembe Togwa
Katiba na mikutano ni mambo ambayo AbdulWahid Sykes na Kleist Sykes hawakufanikiwa kuyafanya. Mohamed hili si kosa kila kitu kina wakti wake.
Kosa ni kuficha ukweli kwa kumzodoa Nyerere au kumdunisha kama ulivyoleta mada ya katiba.
Well, aandike, aazime, anukuu afanye chochote ukweli utabaki pale pale ni Nyerere aliyefanya hivyo, si Abdu au Kleist. Ni muhimu ingawa ni ngumu 'kumesa' kwa mashabiki
Abdul na Wazee wengine walifanya kilicholingana na uwezo wao na hakika ulikuwa msingi mkubwa wa siasa za nchi, lakini si wao peke yao.
Mchango wa Mwana wa Butiama hauhitaji parapanda, Julius anatetewa na historia
Hili imefika mwisho! nashukuru tumeelewana na
James Comey atakuwa amepata jibu.
Nguruvi...
Nimekueleza kuwa Cecil Matola kafariki 1933 kukufahamisha kuwa hakuishi hadi 1950 pale Abdul na Hamza Mwapachu walipompindua Thomas Plantan aliyekuwa President wa TAA na Clement Mohamed Mtamila Secretary.
Ungejuaje kuwa Cecil Matola ndiye alikuwa rais muasisi kama Kleist Sykes asingeandika mswada wa kitabu cha maisha yake na kueleza vipi aliunda African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?
Waasisi wa AA ni hawa wafuatao: Cecil Matola, Kleist Sykes, Selemani Majisu, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Rawson Watt na Raikes Kusi.
Kleist Sykes anaeleza kwa nini Waislam walikuwa wengi katika AA.
Anasema kanisa lilikuwa linawakataza waumini wao kujihusisha na siasa.
Haya utayapata katika ''seminar paper,'' iliyoandikwa Aisha Daisy Sykes, University of East Africa Dar es Salaam Campus 1968.
Daisy aliandika mada hii kwa msaada wa baba yake Abdulwahid Sykes, kutokana na muswada ulioandikwa na Kleist Sykes.
Angalia A.D. Sykes, ''The Life of Kleist Sykes,'' University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15).
Habari nyingine kuhusu Al Jamiatul Islamiyya zinatokana na mswada ulioandikwa na Tewa Said Tewa, ''A Probe Into the History of Islam in Tanganyika.''
Taarifa nyingine zinatokana na maelezo ya Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika miaka ya mwanzo ya 1940.
Naamini James Comey ataelewa tofauti baina yako na mimi.
Wewe unaandika kwa dhana.
Mohamed Said anaandika kutokana na utafiti.
Hakika Mwalimu aliisambaza TANU katika mikutano ya siasa.
Hebu msome Daisy anasema nini kuhusu hii mikutano:
''Nimesikia mazungumzo mengi wakati baba na wenzake walipokuwa wakijadili majina na shughuli ambazo hawa akina mama walikuwa wahusishwe ili kuleta mvuto wa kisiasa katika mikutano yao ya TANU.''
Hii mikutano ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes na Nyerere akihudhuria pamoja na kamati ya ndani ya TANU ya Mzee Rupia, Dossa Aziz, Bi. Titi Mohamed, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Hawa Maftah kwa kuwataja wachache.
Naamini James Comey ataelewa tofauti baina yako na mimi katika historia hii.
Wewe unaandika kwa dhana.
Mohamed Said licha ya kutafiti na kuandika kitabu ni sehemu ya historia hii.
Baba yangu alimjua Nyerere nyumbani kwa Abdul Syes na haya yote kayashuhudia kwa macho yake.
Ndiyo siku zote akisema vipi hawa wataandika historia ya TANU wasimtaje Abdul Sykes?
Nani anaeficha ukweli huu?
Hakika si Mohamed Said.
Nyerere anaujua mchango wa Abdul Sykes.
Msikilize Daisy:
''Juma moja kabla ya kifo chake nilimuuliza baba swali ambalo jibu alilijua lakini katika hulka yake ya kawaida ya kutopenda kujikweza hakutaka achukue sifa zote kwa ule ukweli na matokeo yake.
Wakati ule nilikuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki Dar - es- Salaam na mwalimu wangu wa Historia Dr. John Iliffe kwa kutambua kuwa natoka familia ya Sykes waasisi wa mwamko wa siasa katika Tanganyika na mchango wa wazee wangu katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika alinitaka niandike mafanikio ya Watanganyika wa kizazi kile pamoja na historia ya babu yangu Abdallah Kleist Sykes.
Dk. John Iliffe alinitia moyo nifanye utafiti na kuandika historia hii na nilikubali kufanya hivyo.
Nilikuwa na swali kuhusu nani khasa walikuwapo katika mkutano na kushiriki wa kuibadili TAA kuwa TANU.
Baba akashauri kuwa tuombe miadi na Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere ili anipe ukweli niliokuwa nautafuta na kusadikisha mambo mengine yanayohusiana na historia hiyo.
Hivyo tukaenda Msasani kuonana na Mwalimu Jumamosi moja asubuhi.
Kama ilivyotegemewa Mwalimu alifurahi sana kutuona maana ilikuwa muda mrefu watu hawa waliokuwa marafiki wakubwa sana kupata kuonana.
Mwalimu alitoa ushirikiano mkubwa sana kwangu kupata ukweli kutoka kwake katika yale niliyotaka kujua kutoka kwake.
Hii ndiyo ilikuwa siku yao ya mwisho kuonana.''
Naamini James Comey ataelewa tofauti baina yako na mimi katika historia hii.
Wewe unaandika kwa dhana.
Wewe hutujui sisi.
''Wastara haumbuki.
Wa mbili havai moja.''
Ningeweza kukueleza mengi lakini nachelea kukuchosha na kuwachosha wasomaji wengine.
Picha hiyo hapo chini ni Daisy na Mohamed Said