Kiwanda cha biskuti za bangi chagunduliwa Kawe

Kiwanda cha biskuti za bangi chagunduliwa Kawe

Hata pombe ilikuwa haramu kama bangi ila ikaruhusiwa miaka ya 1930s

Wazungu wametukuta na vilevi vyetu kwanini tufuate sheria zao za vilevi ?

Pombe na Sigara zinaua watu lakini zinaruhusiwa, bangi haijawai kuua na ni dawa ya kansa kwanini inakatazwa ?

Mbona nasikia ukivuta bange unaweza geuka mwehu? au uwongo?
 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekamata kilogramu 423.54 za bangi iliyosindikwa maarufu kama skanka katika operesheni maalum zilizofanyika kwenye mipaka na fukwe za Bahari ya Hindi.

Kilogramu 158.54 zilikamatwa eneo la Kigamboni na Kawe jijini Dar es salaam zikiwa zimehifadhiwa ndani ya mabegi ya nguo tayari kwa kusafirishwa, kilogramu 265 zilikamatwa katika matukio tofauti mikoa ya nyanda za juu kusini zikiwa zimefichwa ndani ya magan kwa kuchanganywa na bidhaa nyingine ikiwemo maboksi yenye matunda aina ya apples zikisafirishwa kuelekea jijini Dar es salaam.

Aidha, Mamlaka imekamata watu wanaojihusisha na utengenezaji wa biskuti kwa kuchanganya na skanka katika eneo la Kawe jijini Dar es salaam. Katika tukio hilo, watuhumiwa walikutwa wakiendelea na uzalishaji wa biskuti hizo kwa kutumia mtambo mdogo wa kusaga skanka na vifaa vya kutengeneza biskuti za bangi.
Nina Mwana ( Rafiki ) hapo najua nae atakuwa Kakamatwa japo nilimuonya sana hakusikia.
 
Ni bangi inayotoka Swaziland
Inalimwa huko,ina soko kubwa sana
Na ina watumiaji wengi sana

Ova
Inalimwa kinamna nyingine au ni mbegu special? Kama ni mbegu huweza kupanda Bongo? Nashangaa kwa nini tutoe Swaziland wakati sisi tuna walimaji wengi tu. Msaada kwa yeyote mwenye kujua please...
 
Mbona nasikia ukivuta bange unaweza geuka mwehu? au uwongo?
Ni kama pombe. Kuna watu inawakataa na kuna watu wanakunywa maisha yao yote. Mimi najua watu wengi wenye heshima na familia + ukwasi mzuri lakini ni wavutaji wa bangi na wanaishi maisha ya kawaida kabisa. Wana hekima na mtaani wanategemewa kwenye kutoa mawazo ya kujenga jamii.
 
Inalimwa kinamna nyingine au ni mbegu special? Kama ni mbegu huweza kupanda Bongo? Nashangaa kwa nini tutoe Swaziland wakati sisi tuna walimaji wengi tu. Msaada kwa yeyote mwenye kujua please...
Kwa bongo ukipanda haitoki kama ya kule swazy, naona hali ya hewa huko inakubali...na wapandaji kule wanaipiga mpaka madawa nk

Ova
 
Hata pombe ilikuwa haramu kama bangi ila ikaruhusiwa miaka ya 1930s

Wazungu wametukuta na vilevi vyetu kwanini tufuate sheria zao za vilevi ?

Pombe na Sigara zinaua watu lakini zinaruhusiwa, bangi haijawai kuua na ni dawa ya kansa kwanini inakatazwa ?
It's all about business bro,

Bangi ikiruhusiwa itapunguza mapato katika viwanda vya sigara ni kama gongo tu ikiruhusiwa viwanda vya pombe Kali vitadumaa
 
Pana watu wanadhani ni Biscuit hizo za madukani hapana kwa jinsi hizo Skanka zinavyogandamizwa zinakua kama biscuits ili kurahisisha kusafirisha na package yake ila ni bangi tuu hiyo na wateja wake wengi ni wageni kwenye Club na hao wadada wa Mjini...Kilo moja ya Skanka inaweza kufika laki nane harafu ndio uzikute hizo biscuits kwenye maduka ya Mangi hakuna kitu kama hicho...
 
Back
Top Bottom