Kiwanda cha Dangote chaleta neema kwa wananchi wa Mtwara

Kiwanda cha Dangote chaleta neema kwa wananchi wa Mtwara

Wizara ya Madini

Govt Institution
Joined
Apr 12, 2025
Posts
50
Reaction score
20
IMG-20250526-WA0602.jpg
Wananchi wa vijiji vya Likonde, Hiyari, Mkwajuni, Mwembetoga, Kyoba, Msijute, Mbuo na Mayanga, mkoani Mtwara, wameeleza kuridhishwa kwao na mchango mkubwa unaotolewa na Kiwanda cha Saruji cha Dangote katika kuboresha huduma za kijamii kwenye maeneo yao, hususan kwenye sekta za elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara.
IMG-20250526-WA0603.jpg

Akizungumza kwa niaba ya walimu na wakazi wa Kijiji cha Kyoba, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kyoba, Muksin Mnakane, amesema kuwa ujenzi wa shule mpya na nyumba za walimu, uliofanywa na kampuni hiyo, umeleta mageuzi makubwa katika utoaji wa elimu kijijini hapo.

“Awali wanafunzi walilazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita mbili kwenda shule za vijiji vya jirani. Hali hiyo ilikuwa inachangia utoro na kushuka kwa ufaulu. Lakini sasa, kwa msaada wa kiwanda cha Dangote, watoto wanasoma karibu na makazi yao, na ufaulu umeimarika,” amesema Mnakane.
IMG-20250526-WA0604.jpg


Ameongeza kuwa kiwanda hicho pia kimeboresha miundombinu ya barabara, jambo lililosaidia kupunguza ajali na kuwezesha wananchi kusafiri kwa urahisi hasa kipindi cha mvua.

“Walimu sasa hawatembei umbali mrefu kufika shuleni. Nyumba walizojengewa zipo karibu kabisa na shule, hivyo wanatimiza majukumu yao kwa wakati na kwa ufanisi zaidi,” ameongeza Mnakane.
IMG-20250526-WA0355.jpg


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Miradi kutoka jamii, Bi. Tatu Salawanda, ameeleza kuwa kiwanda cha Dangote kimefanikiwa kujenga shule katika Kijiji cha Hiyari, nyumba za wahudumu wa afya katika vijiji vya Likonde na Mbuo, pamoja na barabara inayounganisha Kijiji cha Msijute na Zahanati ya Mayanga.

“Wananchi sasa wanaweza kufika hospitali kwa haraka. Aidha, ujenzi wa visima katika kijiji cha Majengo ambapo umesaidia sana wananchi kupata maji safi karibu na makazi yao, tofauti na awali walipolazimika kutembea umbali mrefu,” amesema Salawanda.
IMG-20250526-WA0605.jpg

Naye Meneja wa Mahusiano wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Bw. Abeid Muda, amesema kuwa miradi hiyo ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi karibu na kiwanda hicho.
IMG-20250526-WA0601.jpg


“Mchango wetu unalenga kuleta maendeleo ya kweli kwa jamii. Tumejenga shule, nyumba za watumishi, barabara na miradi ya maji yote haya yakilenga kuwawezesha wananchi wa maeneo haya kufikia huduma bora kwa urahisi,” amesema Muda.

Kwa ujumla, juhudi za Kiwanda cha Dangote zinaendelea kuwa mfano wa kuigwa wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na jamii katika kuleta maendeleo endelevu.
IMG-20250526-WA0606.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250526-WA0602.jpg
    IMG-20250526-WA0602.jpg
    622.8 KB · Views: 36
View attachment 3346500Wananchi wa vijiji vya Likonde, Hiyari, Mkwajuni, Mwembetoga, Kyoba, Msijute, Mbuo na Mayanga, mkoani Mtwara, wameeleza kuridhishwa kwao na mchango mkubwa unaotolewa na Kiwanda cha Saruji cha Dangote katika kuboresha huduma za kijamii kwenye maeneo yao, hususan kwenye sekta za elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara.
View attachment 3346493
Akizungumza kwa niaba ya walimu na wakazi wa Kijiji cha Kyoba, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kyoba, Muksin Mnakane, amesema kuwa ujenzi wa shule mpya na nyumba za walimu, uliofanywa na kampuni hiyo, umeleta mageuzi makubwa katika utoaji wa elimu kijijini hapo.

“Awali wanafunzi walilazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita mbili kwenda shule za vijiji vya jirani. Hali hiyo ilikuwa inachangia utoro na kushuka kwa ufaulu. Lakini sasa, kwa msaada wa kiwanda cha Dangote, watoto wanasoma karibu na makazi yao, na ufaulu umeimarika,” amesema Mnakane.View attachment 3346502

Ameongeza kuwa kiwanda hicho pia kimeboresha miundombinu ya barabara, jambo lililosaidia kupunguza ajali na kuwezesha wananchi kusafiri kwa urahisi hasa kipindi cha mvua.

“Walimu sasa hawatembei umbali mrefu kufika shuleni. Nyumba walizojengewa zipo karibu kabisa na shule, hivyo wanatimiza majukumu yao kwa wakati na kwa ufanisi zaidi,” ameongeza Mnakane.View attachment 3346495

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Miradi kutoka jamii, Bi. Tatu Salawanda, ameeleza kuwa kiwanda cha Dangote kimefanikiwa kujenga shule katika Kijiji cha Hiyari, nyumba za wahudumu wa afya katika vijiji vya Likonde na Mbuo, pamoja na barabara inayounganisha Kijiji cha Msijute na Zahanati ya Mayanga.

“Wananchi sasa wanaweza kufika hospitali kwa haraka. Aidha, ujenzi wa visima katika kijiji cha Majengo ambapo umesaidia sana wananchi kupata maji safi karibu na makazi yao, tofauti na awali walipolazimika kutembea umbali mrefu,” amesema Salawanda.
View attachment 3346497
Naye Meneja wa Mahusiano wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Bw. Abeid Muda, amesema kuwa miradi hiyo ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi karibu na kiwanda hicho.View attachment 3346501

“Mchango wetu unalenga kuleta maendeleo ya kweli kwa jamii. Tumejenga shule, nyumba za watumishi, barabara na miradi ya maji yote haya yakilenga kuwawezesha wananchi wa maeneo haya kufikia huduma bora kwa urahisi,” amesema Muda.

Kwa ujumla, juhudi za Kiwanda cha Dangote zinaendelea kuwa mfano wa kuigwa wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na jamii katika kuleta maendeleo endelevu.View attachment 3346492
Huyu ndiyo Muwekezaji wa ukweli siyo Wachina wanakuja kuuza yebo yebo na dawa za Mbu za kuchoma Kariakoo.
 
Back
Top Bottom