Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 42
Mimi napenda kuunga mkono hoja za wote wanaotetea kuwa na viwanda vikubwa nchini.
Ukweli ni kwamba siasa zimeharibu sana viwanda vyetu. Hayati Mwalimu Nyerere alipoondoka madarakani, aliacha viwanda vingi vikifanya kazi. Viwanda kama TATC, Viwanda vya ngozi (Moshi Tanneries), Kilimanjaro Machine tools, viwanda vya kusindika pamba n.k. Viwanda kama TATC na Kilimanjaro Machine tools vilisaidia sana ku-support viwanda vingine katika kutengeneza vipuri (spare parts) za aina mbalimbali. Sasa hivi karibu vyote (kama sio vyote) vimekufa na matumizi yake kubadilishwa. Na viwanda hivi vilipokufa tu, ndipo viwanda vingine vyote vikafa pia.
Wakuu, viwanda ndio chachu ya maendeleo duniani kote. Nchi zote zinazoitwa zimeendelea, ni kwa kuwa zina viwanda na hasa viwanda mama (viwanda vikubwa na muhimu kwa uzalishaji). Sio rahisi kuwa na uzalishaji mzuri katika kilimo kama viwanda vya kusindika mazoa havipo. Na vile vile, sio rahisi kuendesha viwanda vya usindikaji kama viwanda vikubwa vya vipuri havipo n.k.
Nikirudi kwenye mjadala kuhusu utengenezaji wa magari nchini, wazo langu ni lile lile kama nilivyolielezea hapo juu. Kwamba ili tuwe na maendeleo endelevu, ni lazima tuwekeze kwenye viwanda kama hivyo. Uwezo wa kufanya hivyo upo. Kinachohitajika ni nia ya kufanya hivyo. Kuna wataalam dunia nzima ambao wanaweza kutusaidia kuanzisha viwanda hivyo (kwa gharama). Wachina wameweza, wahindi pia wameweza. Sisi kama wao, pia tunaweza. Viwanda hivyo si tu vitasaidia kukuza ajira, ila pia vitaongeza pato la taifa kwa kiasi kikubwa sana kuliko tunavyoendelea kutegemea madini na viwanda vya bia na soda.
Mambo kadhaa yanahitajika kufanyika
1. Technology: Technology inayotakiwa kutumika ni lazima iwe ya kisasa (state of the art technology), ili kuweza kuzalisha kwa ubora unaotakiwa, kwa muda mfupi, na kwa wingi. Zaidi ya hayo, ili iweze kudumu kwa muda mrefu kabla haijahitaji mabadiliko.
2. Elimu na Utaalam: Ili tuweze kufanikiwa, ni vyema kusomesha waTZ ili waweze kuendeleza viwanda hivyo kwa utaalam unaotakiwa. Kiufundi na katika ubunifu (R&D)
3. Mitaji: Ni lazima nchi iamue kuwekeza kwa nguvu zote. Viwanda hivi si vya gharama ndogo. Pesa nyingi itahitajika. Serikali itatakiwa kupata kodi tu kutoka kwenye viwanda hivi na si kuchukua mapato yote yanayopatikana na kugawa ruzuku kama ilivyokuwa kwa vile ilivyoviua
4. Branding: ukikosea katika branding, sio rahisi kuweza kushindana na wengine duniani. Branding inawezekana kuwa ndio sababu ya "Uhuru" kushindwa huko Kenya. Unawezaje kutengeneza gari zuri halafu ukaliita Uhuru? Nani anaetaka kununua na kuendesha gari linaloitwa Uhuru? Majina kama haya ni ya kisiasa zaidi ya kibiashara. Hakuna maendeleo ya viwanda yanayoshabihiana na branding za namna hiyo. Majina mazuri husaidia katika marketing
5. Marketing: Pamoja na Branding, marketing nzuri inahitajika kufanikisha kukubalika, uuzaji na usambazaji wa bidhaa hiyo. TATA walipoanza kiwanda chao, walifanya marketing kubwa. Hasa ukizingatia makampuni makubwa kama Toyota, Nissan na mengine yalikuwa yameshashika soko. Lakini wameweza kuendelea na kukua hadi sasa.
Tanzania ina kila sababu ya kufanikiwa katika kila kitu inachotaka kukifanya. Tuna kila kitu tunachohitaji. Maliasili, watu n.k. Nia na utashi ndivyo tunavyokosa.