Kiwanda cha kuassemble magari Tanzania...kitarudi kweli?

Kiwanda cha kuassemble magari Tanzania...kitarudi kweli?

Mimi napenda kuunga mkono hoja za wote wanaotetea kuwa na viwanda vikubwa nchini.

Ukweli ni kwamba siasa zimeharibu sana viwanda vyetu. Hayati Mwalimu Nyerere alipoondoka madarakani, aliacha viwanda vingi vikifanya kazi. Viwanda kama TATC, Viwanda vya ngozi (Moshi Tanneries), Kilimanjaro Machine tools, viwanda vya kusindika pamba n.k. Viwanda kama TATC na Kilimanjaro Machine tools vilisaidia sana ku-support viwanda vingine katika kutengeneza vipuri (spare parts) za aina mbalimbali. Sasa hivi karibu vyote (kama sio vyote) vimekufa na matumizi yake kubadilishwa. Na viwanda hivi vilipokufa tu, ndipo viwanda vingine vyote vikafa pia.

Wakuu, viwanda ndio chachu ya maendeleo duniani kote. Nchi zote zinazoitwa zimeendelea, ni kwa kuwa zina viwanda na hasa viwanda mama (viwanda vikubwa na muhimu kwa uzalishaji). Sio rahisi kuwa na uzalishaji mzuri katika kilimo kama viwanda vya kusindika mazoa havipo. Na vile vile, sio rahisi kuendesha viwanda vya usindikaji kama viwanda vikubwa vya vipuri havipo n.k.

Nikirudi kwenye mjadala kuhusu utengenezaji wa magari nchini, wazo langu ni lile lile kama nilivyolielezea hapo juu. Kwamba ili tuwe na maendeleo endelevu, ni lazima tuwekeze kwenye viwanda kama hivyo. Uwezo wa kufanya hivyo upo. Kinachohitajika ni nia ya kufanya hivyo. Kuna wataalam dunia nzima ambao wanaweza kutusaidia kuanzisha viwanda hivyo (kwa gharama). Wachina wameweza, wahindi pia wameweza. Sisi kama wao, pia tunaweza. Viwanda hivyo si tu vitasaidia kukuza ajira, ila pia vitaongeza pato la taifa kwa kiasi kikubwa sana kuliko tunavyoendelea kutegemea madini na viwanda vya bia na soda.

Mambo kadhaa yanahitajika kufanyika
1. Technology: Technology inayotakiwa kutumika ni lazima iwe ya kisasa (state of the art technology), ili kuweza kuzalisha kwa ubora unaotakiwa, kwa muda mfupi, na kwa wingi. Zaidi ya hayo, ili iweze kudumu kwa muda mrefu kabla haijahitaji mabadiliko.
2. Elimu na Utaalam: Ili tuweze kufanikiwa, ni vyema kusomesha waTZ ili waweze kuendeleza viwanda hivyo kwa utaalam unaotakiwa. Kiufundi na katika ubunifu (R&D)
3. Mitaji: Ni lazima nchi iamue kuwekeza kwa nguvu zote. Viwanda hivi si vya gharama ndogo. Pesa nyingi itahitajika. Serikali itatakiwa kupata kodi tu kutoka kwenye viwanda hivi na si kuchukua mapato yote yanayopatikana na kugawa ruzuku kama ilivyokuwa kwa vile ilivyoviua
4. Branding: ukikosea katika branding, sio rahisi kuweza kushindana na wengine duniani. Branding inawezekana kuwa ndio sababu ya "Uhuru" kushindwa huko Kenya. Unawezaje kutengeneza gari zuri halafu ukaliita Uhuru? Nani anaetaka kununua na kuendesha gari linaloitwa Uhuru? Majina kama haya ni ya kisiasa zaidi ya kibiashara. Hakuna maendeleo ya viwanda yanayoshabihiana na branding za namna hiyo. Majina mazuri husaidia katika marketing
5. Marketing: Pamoja na Branding, marketing nzuri inahitajika kufanikisha kukubalika, uuzaji na usambazaji wa bidhaa hiyo. TATA walipoanza kiwanda chao, walifanya marketing kubwa. Hasa ukizingatia makampuni makubwa kama Toyota, Nissan na mengine yalikuwa yameshashika soko. Lakini wameweza kuendelea na kukua hadi sasa.

Tanzania ina kila sababu ya kufanikiwa katika kila kitu inachotaka kukifanya. Tuna kila kitu tunachohitaji. Maliasili, watu n.k. Nia na utashi ndivyo tunavyokosa.
 
Jamani mambo ya magari safari tuliwahi mno kuanza. Kwanini tusingeanza na manati kwanza 😕
 
Tanzania tuliruka mkojo tukakanyaga kinyesi. Tulifundishwa kuwa mchukia pema, pabaya panamwita. Niliwahi nasikiliza mojawapo ya hotuba za Nyerere pale kwa nukta77 akikiri kuwa ni kweli kuna makosa aliyofanya, ni ni haki yasahihishwe, lakini alishangaa sana kuona kuwa tunaondoa hata yale mazuri aliyofanya.

Kuua viwanda vyetu na mashirika ya umma ndio ujinga mkubwa ambao watanzania tulifanya, na tutakuja gundua when it is too late.

Nilitegemea leo hii viwanda kama Scania, na Nyumbu vingekuwa vinafua baadhi ya spare parts za magari hapa hapa nyumbani. At least kwenye roli la Scania tungekuwa tumeongeza added value kubwa sana.

Kwa kuwa viongozi waliotokana na rushwa sidhani kama tutakujakuwa na viwanda vyetu tena.
 
du! e bwana eeeh!!!!!!
nikiwemo mimi, ni wa tzwangapi tupo tayari Kununua, kutumia, na kuona fahari kuwa na NYUMBU na kutupilia mbali TOYOTA, NISSAN, ET AL....?
je tupo tayari kutumia cha kwetu? na sisi watoa mada ni kama wanasiasa?
 
aroo, vitu hivyo kama vikiwepo hapa kwetu vitanunulika tu. hapa kwetu kuna watu wengu tu ambao wanahitaji magari ya kufanyia kazi sio starehe. najua kama unahitaji gari au kitu cha starehe utapenda kununua japan au China etc, lakini kwa watu ambao tunahitaji vitu vya kurahisisha kazi, kama vile matrecta,magari ya mizigo, na machines za aina mbalimbali tutanunua tu. mbona kuna mafundi kibao tu mtaani hapa wanatengeneza machine za kuranda mbao kwa motor,wanatengeneza machines mbalimbali lakini tu ni mfano wa zile machine during industrial revolution ya karne ya kumi na tano ulaya. hata hawajaenda shule ila vitu vinatengenezwa. kama selikali ikiweka sera thabiti kuhusu hilo, tunaweza, na tunaweza hata kushindana na mataifa hayo mengine.

kuagiza gari toka japan ichukue muda, garama za usarifi nk, haiwezi kushindana na kagari hata kama si ka kifahari unakoenda kununua kiwandani pale kibaha au mkuranga kwenye kiwanda chetu.
 
No offense. Mzee unakoroma tu kwa sababu za kisiasa.

Katika engineering kitu ambacho anatumia mlaji kinakuwa kimepitia process nyingi sana. Process ya mwisho ni production.

Magari ya nyumbu yalikuwa kwenye hatua za mwanzo za research and development na hayakufikia kwenye production.
 
Tanzania tuliruka mkojo tukakanyaga kinyesi. Tulifundishwa kuwa mchukia pema, pabaya panamwita. Niliwahi nasikiliza mojawapo ya hotuba za Nyerere pale kwa nukta77 akikiri kuwa ni kweli kuna makosa aliyofanya, ni ni haki yasahihishwe, lakini alishangaa sana kuona kuwa tunaondoa hata yale mazuri aliyofanya.

Kuua viwanda vyetu na mashirika ya umma ndio ujinga mkubwa ambao watanzania tulifanya, na tutakuja gundua when it is too late.

Nilitegemea leo hii viwanda kama Scania, na Nyumbu vingekuwa vinafua baadhi ya spare parts za magari hapa hapa nyumbani. At least kwenye roli la Scania tungekuwa tumeongeza added value kubwa sana.

Kwa kuwa viongozi waliotokana na rushwa sidhani kama tutakujakuwa na viwanda vyetu tena.

Kichuguu:

Huwezi kufanya vitu bila kuwa na strategic interests. Nyerere aliacha vitu vingi. Lakini viwanda vingi vilipangwa kisiasa zaidi lakini sio kuwa na strategic interests.

Kwa mfano, makaa ya mawe na chuma yanapatika Mbeya. Machine tools kilikuwa Kilimanjaro na research za magari Kibaha. Wapi na wapi hapo??
 
Ndugu yangu Zakumi, kumbuka kulikuwa na viwanda vingi zaidi ya hivyo ulivyovitaja. Kulikuwa na viwanda vya Kahawa, Tanneries, Pamba, Bia, Korosho, Vioo, Sabuni, Soda, Kusindika nyama, n.k. Viwanda hivi havikuwepo sehemu moja. Kiwanda cha nyumbu pamoja na kuwa na uwezo wa kutengeneza magari, pia kilikuwa na uwezo wa kutengeneza spares na zana nyingine. Inawezekana kuwa location zake hazikuwa sahihi, lakini location gani ni sahihi?
 
Mawazo ya jamaa ni mazuri, na analosema limo ndani ya uwezo wetu kabisa, kwa sababu teknolojia ipo, utafiti ulishafanywa, wasomi wapo, pesa zipo ( mmejenga twin tower na vitambulisho vya bei mbaya), raw materials zipo, ila tatizo lipo kwenye priorities, kutojiamini na kukosekana kwa uzarendo..... YES, WE CAN jamani
 
Ndugu yangu Zakumi, kumbuka kulikuwa na viwanda vingi zaidi ya hivyo ulivyovitaja. Kulikuwa na viwanda vya Kahawa, Tanneries, Pamba, Bia, Korosho, Vioo, Sabuni, Soda, Kusindika nyama, n.k. Viwanda hivi havikuwepo sehemu moja. Kiwanda cha nyumbu pamoja na kuwa na uwezo wa kutengeneza magari, pia kilikuwa na uwezo wa kutengeneza spares na zana nyingine. Inawezekana kuwa location zake hazikuwa sahihi, lakini location gani ni sahihi?

Recta:

Mada ni kiwanda cha ku-assemble magari. Hivyo hapa tunaweza kuzungumza Scania na Nyumbu. Hivyo viwanda vingine utakuwa unatoka nje ya mada.

Magari ya Nyumbu hayakuingia katika full production. Na kama yaliingia, sijuhi units ngapi zilikuwa zinatengenezwa kwa mwaka ??? Hivyo huwezi kusifia kitu ambacho kilikuwa kwenye research tu. Hata Kenya waliwahi kutoa magari yao, MOI I and MOI II, lakini yote yalikuwa ni project za university tu.

Kuhusu Scania kuna factors nyingi kuanzia kuongezeka kwa magari mitumba, na vilevile biashara kuwa mikononi mwa watu binafsi, choices. Huwezi kuwalazimisha watu kununua vitu.

Kuhusu location I beg to differ. Kwanini Silicone Valley hiko california, Makampuni ya magari Detroit n.k

Location ni kitu muhimu sana.
 
Zakumi, kama tunazungumzia uzalishaji wa magari tu, basi sina mchango mkubwa kwa hilo. Ila kama tunazungumzia viwanda vikubwa, nadhani kuna mengi ya kuongelea. Ila hata wazo la kuzalisha magari sio baya sana kama nguvu zinazohitijika kufanya hivyo zitatumika kwa uangalifu mkubwa.

Mimi sina ubishi na umuhimu wa location katika maendeleo ya biashara yoyote. Location ikichaguliwa vibaya, hata kama biashara ni kubwa na nzuri kiasi gani, uwezekano wa kuwa endelevu unakuwa mdogo. All businesses are catalyzed by location to a large extent.
 
Vitu vingi vinaendeshwa kwa imagination, you have it or you don't. Chukua mfano wa UFI, toka wameanza bidhaa zilikuwa ni zilezile. Kulikuwa hakuna enhancement yoyote.

Urafiki kabla ya kurudi waChina mitambo ilikuwa ni hilehile na uzalishaji hulehule.

Viwanda vyote vilivyoanzishwa vilikuwa vinatengeneza bidhaa zilezile, kwa kutumia njia zilezile na kutegemea wanunuzi watabakia na mtazamo hulehule.

Kulikuwa hakuna innovation yoyote hile. Hivyo kufa kwa viwanda doesn’t depress me at all.
 
Wana JF,
Hii mada nzuri sana. Mie nakubaliana na wale wanaosema kuwa viwanda vingi wakati wa Nyerere vilikuwa vya kisiasa. Hasa inapokuja kwenye swala la location ambalo kwa njia moja au nyingine linaongeza ghalama za uzalishaji.

Kiwanda cha magari ni wazo zuri. Ila hili naona TULIACHE KWANZA. Ili tufanikiwe katika hilo, lazima twende kwenye MZIZI wa fitina. Mzizi wa fitina hapa ni STEEL. Chuma hiki kiitwacho STEEL ndicho kinaweza kuwa MKOMBOZI wa Tanzania. Itabidi sisi wenyewe tuinvest sana kwenye hili katika utafiti hasa kwenye steel produation na ALLOYS. Kwa sasa hizi ALLOYS ndiyo zinatesa sana. Chuma kama chuma ni kizito sana. Inapokuja kwenye utengenezaji wa ndege kwa mfano, wanatumia zaidi ALLOYS ambazo zinakuwa ngumu kama chuma na nyepesi kama karatasi (bado wanaendelea na utafiti).

Somo la STEEL na ALLOYS (Metal Engineering prodution na Chemical Engineering) limekuwa likiwapa ulaji sana Wazungu. Kuna somo nilishafanya linaitwa "Theory of elasticity and Plasticity". Sijui kama nimeandika vizuri, ni somo moja gumu sana na ukilijua basi utafanya vitu vingi sana kwa kutumia hili somo. Nilishangaa kuona kuwa kiwanda kama BMW walikuwa wakitumia hili somo kabla ya vita vya 2 ya dunia katika kudesign injini za magari. Hili somo utaweza kulitumia kwenye ujenzi (structures), magari, meli, hospital (mwalimu wangu alienda USA kudesign taya la mtu artificial) nk nk. Sasa basi kwa mawazo yangu mie ni kuwa kama vijana wangelisomeshwa hayo masomo mawili na waanze kwa kutumia kidogo ujanja wao wa kuzaliwa, wizi walioiba wakiwa nje, na huku kikiwepo kitengo cha MASHUSHUSHU wa technologia nje ya nchi, nafikiri tungelifaulu.
Hiki chuo inatakiwa kiwe chini ya JESHI. Huwezi kuenda popote pale duniani leo hii na ukafundishwa somo la steel. Walioendelea wana vyuo vyao ndani ya kambi za jeshi na huko ndiko wanakofanyia ugunduzi na utafiti wa haya mambo. Wanajua kuwa MPINGO ukijua basi wao wamekufa njaa. Kama tukijua kucheza na STEEL na hizo alloy nyingine basi itakuwa hata zaidi ya kuwa na mafuta/dhahabu Tanzania. Mjapan hana kitu chochote kwake ila anajua kucheza na hivi vitu.
Ukiangalia mawazo ya Watz utaona jinsi walivyo na hamu ya kuona nchi yao inakuwa JAPAN ya Africa. Ila tatizo ni WANASIASA. Kuchukua wanasiasa na kuwapa nchi, ni system ya ovyo kabisa iliyowekwa na wazungu ili kuhakikisha sisi hatufiki mbali. Ingelikuwa wanasiasa wanatakiwa wawe WAHANDISI, nina amini leo hii angelishatokea Rais mzuri sana Tz. Ila kama kigezo ni mtu anayejiuza, sera zake, ng'ombe wake, takrima yake na maneno matamu kama asali...... tupo hapo tulipo. Ingelikuwa ni kigezo cha UHANDISI, ingelikuwa inawekwa mezani, wewe umekuwa mbunifu wa kitu gani na wewe kitu gani. Kama mhandisi hajawahi kufanya kitu chochote, na AFIE MBALI.
Narudia tena, ili tuendelee na tuwe na viwanda, basi tuanzie na kiwanda cha chuma kwanza (STEEL). Tukiweza hili, mengine yatateleza tu. Tukishindwa hili, hamna haja ya kurukia kwenye mengine ambayo ni PRODUCT ya steel.
 
No offense. Mzee unakoroma tu kwa sababu za kisiasa.

Katika engineering kitu ambacho anatumia mlaji kinakuwa kimepitia process nyingi sana. Process ya mwisho ni production.

Magari ya nyumbu yalikuwa kwenye hatua za mwanzo za research and development na hayakufikia kwenye production.

mkuu, kama una muda hebu fanya kutembelea hiyo tovuti yao:Welcome to TATC halafu ufanye tathmini ya dhamira ya Mradi mzima wa 'nyumbu.'
 
Gari jipya la nyumbu lazinduliwa
nyumbu.JPG

Gari jipya aina ya NYUMBU lililotengenezwa na kampuni ya mzinga ya JWTZ likiwa kwenye maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma-kwenye viwanja vya manzi mmoja
 
Jamaniee, Mungu atupe nini sisi watz? Kule Liganga kuna chuma ambayo tutaweza kuchimba kwa miaka hata mia, kule mchuchuma na mbinga kuna makaa ya mawe tunayoweza kuchimba kwa muda wa miaka hamsini. tunayo bahari kuingizia mashine na vito vinginge tusivyonavyo. makaa ya mawe kutengeneza umeme mwingi. gesi kutengeneza umeme na matumizi ya ndani. mafuta nayo kuna uwezekano mkubwa kuwepo.

zamani tulikuwa na kiwanda cha kuassemble magari kule kibaha(NYUMBU), si mnakumbuka magari ya nyumbu jamani? kiwanda kile kilikufa kifo cha mende(mende akifa kimgongo asipolalia kifua anaweza akaozea hapohapo). what makes us tzs kutokuhimiza kiwanda kipya cha magari hapa jamani? wakati chuma tunayo ya kumwaga. uranium kama ni kutengeneza umeme etc tunayo ya kumwaga hapa(in mbinga and around lake nyasa). wakenya wana assemble magari tayari, na sisi tunang'a macho tu. wakenya wangekuwa na resources hizi, wangekuwa mbali sana.

kama kuna kiongozi aliyeshika rungu humu(mimi sijashika rungu ndo maana sauti au impact yangu haiwezi kuwa kubwa kama ile ya watu tuliowapa dhamana), huko china,uturuki,japan etc mnakopeleka wanafunzi, basi pelekeni wanafunzi kwenye mambo ya technologia, ili wakirudi tuanzishe vitu vyetu.

Kuna kijana mmoja kule kanda ya ziwa alisoma Japan, akafanya field kule kwenye kampuni ya kutengeneza boat, kwasasa amerudi hapa bongo, anatengeneza boti nzuri na za kisasa kule ziwa victoria sana. yaani very good ship builder aisee. nina uchungu sana na nchi yangu kwakweli.

JE UPO TAYARI?

Kutembea kwa miguu mpaka viwanda vyetu vya kutengeneza magari vitakavyoweza kukidhi soko la ndani?

Mwanzo wa matatizo mengi tuliyonayo ni baada ya Mzee RUKSA (MWINYI) kuruhusu vitu kuingia, hapo ALIUA uwezo wetu wa kufikiri na kukabiliana wenyewe na changamoto zinazotukabili. Changamoto nyingi tunazokabiliana bado hatujawa na uwezo wa kufikiri jinsi ya kuondokana nazo, mara nyingi huwa tunatafuta teknolojia toka nje ziweze kutatua changamoto zetu.

Ili kuweze kufufua viwanda vyetu vya ku-assemble magari itabidi kwanza kufunga mipaka ya kuagiza magari kutoka nje, ili kusiwe na ushindani ambao utapelekea viwanda hivi visikue na hivi ndivyo wenzetu walivyoendeleza viwanda vyao.
 
Jamaniee, Mungu atupe nini sisi watz? Kule Liganga kuna chuma ambayo tutaweza kuchimba kwa miaka hata mia, kule mchuchuma na mbinga kuna makaa ya mawe tunayoweza kuchimba kwa muda wa miaka hamsini. tunayo bahari kuingizia mashine na vito vinginge tusivyonavyo. makaa ya mawe kutengeneza umeme mwingi. gesi kutengeneza umeme na matumizi ya ndani. mafuta nayo kuna uwezekano mkubwa kuwepo.

zamani tulikuwa na kiwanda cha kuassemble magari kule kibaha(NYUMBU), si mnakumbuka magari ya nyumbu jamani? kiwanda kile kilikufa kifo cha mende(mende akifa kimgongo asipolalia kifua anaweza akaozea hapohapo). what makes us tzs kutokuhimiza kiwanda kipya cha magari hapa jamani? wakati chuma tunayo ya kumwaga. uranium kama ni kutengeneza umeme etc tunayo ya kumwaga hapa(in mbinga and around lake nyasa). wakenya wana assemble magari tayari, na sisi tunang'a macho tu. wakenya wangekuwa na resources hizi, wangekuwa mbali sana.

kama kuna kiongozi aliyeshika rungu humu(mimi sijashika rungu ndo maana sauti au impact yangu haiwezi kuwa kubwa kama ile ya watu tuliowapa dhamana), huko china,uturuki,japan etc mnakopeleka wanafunzi, basi pelekeni wanafunzi kwenye mambo ya technologia, ili wakirudi tuanzishe vitu vyetu.

Kuna kijana mmoja kule kanda ya ziwa alisoma Japan, akafanya field kule kwenye kampuni ya kutengeneza boat, kwasasa amerudi hapa bongo, anatengeneza boti nzuri na za kisasa kule ziwa victoria sana. yaani very good ship builder aisee. nina uchungu sana na nchi yangu kwakweli.

Hujuma zilizofanywa na serikali zilizofuata baada ya Baba wa Taifa kuachia uongozi zitalitesa taifa letu kwa miaka mingi ijayo. Ni majuzi tu nilikuwa nikisoma makala moja ya Jenerali iliyonukuliwa katika moja ya websites na inayopatikana pia katika gazeti la Raia Mwema kwamba kujivua magamba tu hakutoshi bali nchi hii ili irudi kwenye mwelekeo inabidi ikabidhiwe kwa "Nyerere" mwingine; yaani mtu atakayekuwa shupavu, makini na mweledi kama wa huyo hayati.
Hebu tafakari, ndani ya kipindi kisichozidi miaka 30 tokea JKN kuschia ngazi mafisadi waliojipenyeza serikalini kupitia chama tawala walishawishi uuzwaji kwa bei ya kutupa wa mashirika na viwanda vingi, vikiwemo viwanda mama Mzee yule alivyokuwa ameandaa kwa ajili ya maendeleo ya siku za mbele kama kwanda pekee kilichokuwa cha kusafisha mafuta cha TIPER, Kiwanda cha kutengeneza mashine nzitonzito kilichokuwa Moshi (Kilimanjaro Machine tools), kile cha Mang'ula Mechanical Tools Morogoro, kilichokuwa kiwanda cha kuunganisha magari aina ya Scania kule Kibaha na vingine vingi kwa kisingizio rahisi cha ati serikali haifanyi biashara! Upandaji holela wa bei ya bidhaa za Petroli leo ungeweza kabisa dhibitiwa kama mafuta yangekuwa yana safishwa hapa hapa! na tatizo hili haliishii hapo tu, kwa mfano sasa kuna kila dalili za kuwepo kwa mafuta hapa nchini; lakini kwa hujuma hii hata tukianza kuyachimba kesho bei haitabadilika kwani bado tutategemea mafuta yanayosafishwa nje ya nchi! Hatutakuwa tofauti na Nigeria ambayo licha ya utajiri mkubwa wa mafuta, bidhaa hiyo ni adimu huko na bei yake haishikiki! Okay, karibuni tutaanza kuchimba chuma na makaa ya mawe mchuchuma na sehemu nyingine nchini; kwa hali ilivyo bado nchi yetu itaendelea kuagiza mashine toka nje kwa vile viwanda mama ambavyo vingeitumia malighafi hiyo vilishagawiwa kwa wajanja! Kuhusu Nyumbu ukweli ni kwamba hakikuwa kiwanda bali kituo cha utafiti ambacho kingepelekea nchi kuanza kutengeneza magari na mitaambo inayobuniwa na vijana wetu mahiri ambao hadi sasa wamebuni nakuvumbua mashine nyingi tu ambazo kwa vile hatuna viwanda kama kile cha Moshi au cha mang'ula kilichoendelezwa kidogo wameishia hewani na inasemekana imebidi wauze patents zao nje ili zitumike angalau kwa muda kwa vile hakuna uwezo wa kuzalisha kwa wingi bidhaa zao zikiwemo magari ya zima moto, mmagari ya aina ya Nyumbu, vifaru n.k.
Kuna kipindi Nyerere alivunja ukimya na kulaani hujuma zilizokuwa zikifanywa za kuuza ovyo viwanda na mashirika, na kwa muda zoezi hilo lilisinzia lakini alipokufa wahuni hawa walichangamkia si mashirika na viwanda tu; bali ata migodi, ardhi, bandari mpaka nyumba za serikali zilizojengwa hata kabla ya baba zao kuzaliwa. Matokeo ya hujuma hii sasa tuna viongozi waandamizi serikalini wakiwemo mawaziri hadi majaji wanaoishi kwenye mahoteli na kuigharimu serikali fedha nyingi wakati nyumba zilizokusudiwa kutumiwa na wao zimeporwa na wahuni hawa.
Hapa ndipo ninapoafikiana na Jenerali kwamba kujivua magamba hakusaidiii wala kutosha zaidi ya kumpata "Nyerere" mwingine; na ukipenda toka upinzani kwa maana kwa kutumia kanuni ya mwasisi wa hiyo hiyo CCM, hakuna kiongozi anayetokana na ufisadi anayeweza kuupiga vita ufisadi. Leo hii ni nani katika chama cha Magamba anaweza kudai hakutokana na ufisadi? Mukama tunayemjua vizuri alikotoka, aliko na anakoelekea? Au huyu kibwetere Nape anayenunuliwa hata kwa cheo cha kishemeji cha Ukuu wa wilaya na sasa sijui Naibu takataka gani vile! Mungu ibariki Tanzania, iepushe na wenye nguvu waishio gizani, ndiyo CCM.
 
No offense. Mzee unakoroma tu kwa sababu za kisiasa.

Katika engineering kitu ambacho anatumia mlaji kinakuwa kimepitia process nyingi sana. Process ya mwisho ni production.

Magari ya nyumbu yalikuwa kwenye hatua za mwanzo za research and development na hayakufikia kwenye production.
sasa wewe bwabwa au punga kwa jina lingine, tatizo lako ninini hata ukashifu hivyo? nilitoa wazo, kama basi tulishindwa yale ya nyumbu, basi hata kufanya joint partnership Toyota au HOnda etc waje waweke plant yao hapa si haba, wewe ungetoa wazo la aina hiyo ili hata kama hatutakuwa na branch yetu baasi tuwe na kiwanda walau cha kuassemble magari kama wanavyofanya south africa na kwingine....utasemaje nakoroma kwa kisiasa wakati nia yangu kuongelea hili sikuwa na nia mbaya, wewe unakuja kuongea kama unatoka kutafunwa kipunga..vipi wewe? kila kitu kwako ni siasa? hata tigo yako unaweza kusema ni ya kisiasa...eheee.
 
Back
Top Bottom