Tetesi: Kiwanda kipya cha sigara,Kingorwila Morogoro ukweli ni upi?

Tetesi: Kiwanda kipya cha sigara,Kingorwila Morogoro ukweli ni upi?

Yapaswe

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2016
Posts
322
Reaction score
240
Salaam wanabodi.....
Niende moja kwa moja kwenye Maada ya swali hili,Kiwanda kipya cha sigara Kingolwira Morogoro kilitoa nafasi za kazi tangu mwaka jana mwezi wa nane.

Pamoja na ukimya wote ule lakini juzi kapita mweshimiwa Rais Magufuli kuweka jiwe la msingi na kuruhusu rasmi kiwanda kufanya kazi ,katika hotuba ya Mwakilishi wa kiwanda alisema wametoa ajira 200 na tayari majina ya wahusika yamebandikwa!!!!

Sasa swali ni wapi haya majina yalipo? Kiwandani kule hakuna majina na hakuna taarifa yoyote ya wafanya kazi waliopo mle kuhusu majina hayo ya ajira mpya.

Najua humu wapo baadhi ya wahusika naomba mtupe ukweli hapa!!
 
Salaam wanabodi.....
Niende moja kwa moja kwenye Maada ya swali hili,Kiwanda kipya cha sigara kingolwira Morogoro kilitoa nafasi za kazi tangu mwaka jana mwezi wa nane. Pamoja na ukimya wote ule lakini juzi kapita mweshimiwa Rais Magufuri kuweka jiwe la msingi na kuruhusu rasmi kiwanda kufanya kazi ,katika hotuba ya Mwakilishi wa kiwanda alisema wametoa ajira 200 na tayari majina ya wahusika yamebandikwa!!!! Sasa swali ni wapi haya majina yalipo? Kiwandani kule hakuna majina na hakuna taarifa yoyote ya wafanya kazi waliopo mle kuhusu majina hayo ya ajira mpya... Najua humu wapo baadhi ya wahusika naomba mtupe ukweli hapa!!
Labda yapo kwa meneja ofsin kwake
 
Nchi za dunia ya kwanza wanafunga viwanda vya sigara na bidhaa za tumbaku ndio maana huoni vkiruhusiwa kujitangaza.
Sasa hawa wauwaji wameamua kuhamishia sumu zao Shithole countries.
 
yamebandikwa ofcn kwa afsa mwajir
Sasa si watoe copy wayaweke huku public area? Kuingia humo ofisi unaanzaje na utapita wapi maana wale walinzi nao utadhani wanalinda ikulu hata kuongea hawataki
 
Kuna barabara ya Dodoma Iringa iliishajengwa tokea 2016 sehemu ya kuzindulia uwanja pale iringa imeota miti mikubwa nadhani anasubiriwa mheshimiwa aje aifungue 2019. Saizi kuna walinzi wanalinda ule uwanja ng"ombe wasiingie kula majani. Mwezi uliopita Mama Samia alienda kuweka jiwe la msingi la utalii pembeni kidogo ya huo uwanja anasubiriwa JPM kuja kufungua. Najiuliza ile siku aliyokuja makamu wa Raisi kwa nn asingeunganisha na ufunguzi wa Barabara? Mama Samia nae kaja kuweka jiwe la msingi pori tu usanii kibao eti kitakua kitovu cha utalii. Nimegundua hii ni serikali ya kiki sana
 
Nchi za dunia ya kwanza wanafunga viwanda vya sigara na bidhaa za tumbaku ndio maana huoni vkiruhusiwa kujitangaza.
Sasa hawa wauwaji wameamua kuhamishia sumu zao Shithole countries.
Hata Tanzania sigara hazitangazwi. Tukifika dunia ya kwanza tutazuia ngoja kwanza tuuze tumbaku yetu na kufanya kazi(ajira).
 
Ile ilikua ni funika kombe mwana haramu apite..... Akisha pita... Utajiongeza
 
Ninachojua mimi kiwanda kile wanachokiita MOIL ni cha PMI_Philip Moris Inc(Wamarekani)
Kilianza kufanyakazi mwaka wa jana kama mtakumbuka vizuri mbio za mwenge kiliweka jiwe la msingi na pia Prime Minister alishakitembelea na sigara zao nafikiri zimeingia sokoni (Marlborro)

Pale nilichojua mimi MOIL kama mtanzania ambaye ndio mbia wa kitanzania ndio anawafanyakazi hao 200.
kile kiwanda kimefungwa mitambo ya kisasa sana inaowezesha kuendeshwa na wafanyakazi wachache saaana kama tujuavyo zao la Tumbaku ni la msimu kwahiyo kitakuwa na wafanyakazi wachache waajiriwa na watakaobaki wa msimu kama wenzao wa Alliance One ambao wanawaajiri wachache wasiozidi 400,
waliobaki zaidi ya 2100 wa msimu kutokana na zao lenyewe.

Najua kwa sasa kiwanda kina wafanyakazi wasiofika 90 lakini wanalipwa vizuri saana kutokana na wateja walengwa
na wamelenga soka la Africa kwa ujumla.
Waajiriwa wengi ni watanzania ,wizara ya mambo ya ndani kwa sasa ipo makini saana na work permit kulinda soko la ajira kwa wazalendo


Wadau wanaojua zaidi watakuja kufafanua zaidi.
 
Back
Top Bottom